KAWETELE
JF-Expert Member
- Dec 11, 2015
- 681
- 1,611
salaamu wana JF
Serikali ya awamu ya tano chini ya Mtukufu Rais, imedhamiria kuhamia dodoma kutimiza ndoto ya muasisi wa taifa hili. ni jambo jema ingawa limekuja ghafla mno kiasi wachambuzi wa mambo wanahoji uharaka wa jambo nyeti kama hilo.
Ikumbukwe kwamba suala la kuhamia dodoma haikuwa hata miongoni mwa top 3 mwa vipaumbele vya serikali, pengine serikali imejiridhisha baada ya kuona viwanda na elimu vimefanikiwa sasa serikali imejikita kuhamia dodoma.
Maswali ninayojiuliza hapa.
Tayari watumishi wamelazimishwa kuhama, na imetangazwa yale majumba ya serikali yanayotazamana na bahari yatapigwa minada, na watakao kataa kuhama watakuwa wamejifukuza.,
1. Je, iwapo bunge litakataa kupitisha hiyo sheria, itawalazimu Serikali kurudi dar? gharama zote hizo nani atafidia?
2. Na kama serikali ina uhakika wabunge watapitisha, haioni kuwa serikali ipo juu ya Bunge, na zile lawama za serikali kuwa mmliki wa bunge hasa baada ya naibu spika wa bunge kuteuliwa na mkuu wa serikali aje agombee ili aje aisimamie serikali hiyo hiyo, zitakuwa zinajidhihirisha wazi wazi?
3. Mbona tukiwa shule tunaambiwa makao makuu ya nchi ni Dodoma, je mitaala ilikuwa inapingana na sheria?
Tafadhari naomba kufahamishwa hasa kisheria kwa wenye uelewa wa hili.