Itakuwa rahisi zaidi mzee Hashimu Rungwe kushinda urais 2020 kuliko mbunge/diwani msaliti wa upinzani kushinda kura za maoni ndani ya CCM

ISRAEL JR

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
1,439
631
"Amani iwe nanyi"
__________________
Mwandishi nguli Wa Vitabu Terry Pratchett amewahi kusema namnukuu " If you do not know where you come from, then you don't know where you are, and if you don't know where you are, then you don't know where you're going. And if you don't know where you're going, you're probably going wrong "
_____

Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema "Kama hujui ulikotoka basi hujui uliko na kama hujui uliko basi hujui unakokwenda na kama hujui unakokwenda basi huenda umepotea" Kabla ya kuamua kufanya jambo lolote kubwa kama kuhama chama na kuacha ubunge/udiwani lazima ujihoji sawasawa,Na wajomba niwahakikishieni na hili nalisema toka ndani ya moyo wangu ninyi hamtarudi kwenye hizo nafasi zenu 2020 na kama yupo atakayerudi basi aende akatambike.
____________________
Kunadhana ogofi toka kwa CCM na mawakala wake kwamba 2020 wagombea wote Wa CCM watatangazwa kwa nguvu ya dola/polisi kama wanavyofanya sasa ila nawahakikishia ninyi si tu hamtatangazwa na NEC bali hamtatangazwa na CCM kugombea hizo nafasi kwani kamwe hamtashinda kura za maoni ndani ya hii CCM-Mpya na nirahisi zaidi kutangazwa aliyeshinda kuliko aliyeshindwa kwenye uchaguzi mkuu Wa 2020, wajomba tumieni mafao yenu vizuri hii picha yenu mwisho wake ni 2020, Nirahisi zaidi mbunge/diwani atakayesalia Upinzani hadi 2020 kurudia nafasi yake 2020 kuliko yule atakayesaliti na kwenda CCM kushinda tu kwenye kura za maoni.
_______
Kwanini nasema wapinzani tutashinda na tutatangazwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Sikia, Tanzania kwa sasa kuna watu mil 54.2, Kwa mujibu Wa NBS huku wastani wa ongezeko la watu kwa mwaka likiwa ni wastani wa watu mil 2 wakati vifo vikiwa ni wastani watu laki 4 hivyo ongezeko taslimu la kila mwaka ni watu mil 1.6 sawa na watu mil 57.4 ifikapo 2020,Huku Idadi Wa watu waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2015 wakiwa 23,161,440 japo kuna watu zaidi ya 740,031 sawa na 4.1% hawakuandikwa.
____________________
Taifa la Tanzania kwa mujibu Wa taarifa ya IGP Sirro kwa Rais lina askari wapatao elfu 40,taarifa hii aliitoa alipokuwa Arusha kwenye uzinduzi Wa nyumba za askari,Hii ni sawa na 1:355 yaani askari mmoja Wa Tanzania analinda mali na watu 1,355 huku wengi Wa watu hao wakiwa ni vijana, Hivi kweli polisi mmoja mwenye SMG yenye risasi 30 anaweza kuwathibiti watu zaidi ya elfu moja ili wasitangazwe baada ya kushinda?JIBU NI HAPANA MSHINDI LAZIMA ATANGAZWE 2020 na dola lazima iende Upinzani na hii sawa na kupishana na gari la mshahara.
____________________
Kwa mujibu Wa tume ya uchaguzi (NEC) mwaka 2015 kulikuwa na vituo rasmi vya kupigia kura 65,105 huku kila kituo kikiwa na wapiga kura kati ya 400/500.
_______
Katika Taifa lenye askari elfu 40 na vituo 65,105 sawa na askari mmoja kulinda/kusimamia vituo 2 huku kila kituo kikiwa na watu 500 yaani askari mmoja mwenye SMG moja yenye risasi 30 tu adhibiti wapiga kura 1,000 na wafuasi wengine walioshinda wasitangazwe ili atangazwe aliyeshindwa, nadhani ni kichaa na mwendawazimu pekee ndio anaweza kuamini haya kutokea katika uchaguzi mkuu Wa mwaka 2020.
____________________
Si hilo tu pia tunamajimbo 264 na kata 3,953 nchi nzima zinazofanya jumla ya maeneo ya uchaguzi kuwa jumla yake 4,217 kwa haohao Polisi wetu wapendwa elfu 40 ni sawa na kusema Polisi wetu 10 wasimame katika kila eneo la uchaguzi na wahakikishe aliyeshinda akiwa ni mpinzani hatangazwi, Nasema ni kichaa pekee ndio anayeweza kuamini haya kutokea 2020 kwa msaada Wa Polisi wetu hawa hawa wapendwa tena hawa kiduchu wana wa wazawa masikini Wa Kitanzania.Jeshi naamini wao hawataweza kufanya haya na si tu kujaribu ila kuona raia wakinyanyaswa na polisi wao wapendwa
_________________________________
Maswali haya yawatakafarisheni ninyi mlioko kwenye foleni ya kuhama Upinzani
( i ) Je Mh, Unatamani huo udiwani/ubunge wako udumu nao kwa vipindi/mihula mingapi? Je ni hiki kimoja kimekutosha au tano tena, tena kwa CCM mpya?
_____
( ii ) Je Mh, Umewahi tafakari kwa kina kabisa ukifika CCM hasa 2020 unayo misuli/nguvu ya kupambana na wazawa kwenye kura za maoni au umeahidiwa kupitishwa tena 2020 bila kupingwa?
_____
( iii ) Je Mh, Umewahi kudodosa kwenye hiyo nafasi wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni Wanaccm kindakindaki wangapi waliipigania ,Je kwa sawa wameongezeka au wamekufa wote? Kama bado wapo wanawaza nini juu ya uchaguzi mkuu Wa mwaka 2020 je watakuacha tena wewe mpakwa mafuta upite bila kupingwa kwa mara ya pili?
_____
( iv ) Je Mh, Umewahi kuzibaini fursa zote ulizozipata kwa kipindi hiki cha miaka mitatu ukiwa kama diwani/mbunge ukazilinganisha na thamani ya hizo pesa/ahadi unazopewa leo ili ukihame chama chako ulichokipigania kwa nguvu nyingi.
_____
( V ) Je Mh, Umewahi kudodosa popote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 1992 ni mgombea yupi Wa Upinzani ukiwemo wewe amewahi Kutangazwa na tume ya Uchaguzi kirahisirahisi tu kama hayupo Unahofu gani juu ya 2020?
___________________________________ Sikilizeni makamanda kamwe Upinzani hakuna wakuufuta/kuua wala kuufifisha, "Upinzani" sio mtu wala sare za chama,"Upinzani" sio Ubunge wala Udiwani "Upinzani" sio Mbowe wala Mashinji sio Lissu wala Heche sio Mnyika wala Mwalimu sio Zitto,Lemma wala Sugu sio Msigwa,Kubenea,Komu wala Lowassa au Wenje sio Sumaye wala Mbatia sio Mzee Seif wala Silinde sio Millya wala Halima Mdee,Upinzani Sio Bulaya wala Matiko, Upinzani sio Ryoba wala Mwakajoka sio Peter wala Prof J,Sio Bwenge wala Suzan,Upinzani sio Nassari wala Haonga au Dickson,Upinzani sio Jaffary wala Paulina au Mkunti, Upinzani sio magwanda ya kaki wala kofia za zambarau UPINZANI NI "FIKRA"
______
'Wapinzani wapo mpaka Ikulu ya Magogoni,Wapo Usalama Wa taifa,Wapo JWTZ,Wapo jeshi la Polisi,Wapo jeshi la Magereza,Wapo serikalini na kwenye taasisi zake mbalimbali,Wapo JKT yaani ,"Opposition is all over" Wanadamu tumeumbwa wa mitazamo miwili ya left & right hemispheres,Opposition is inevitable. Huwezi amini baada ya CCM kuangushwa na Upinzani kuna watu siku hiyohiyo baada tu ya kusheherekea ushindi ule watawahama na kujiunga tena na chama cha upinzani na haraka wataanza kuwaharakatieni ninyi because we are of the left & right hemispheres in nature, Huwezi hata kwa sekunde moja kuufuta "Upinzani " ila unaweza kufuta baadhi ya Wapinzani wanaoonekana
LEO UKIUPOTEZA UBUNGE/UDIWANI WAKO ITAKUCHUKUA MIAKA 20 NDANI YA CCM ILI KUSHINDA KURA ZAO ZA MAONI
___________________________________
 
Umeniwahi mtoa mada.Hili ndio naliona kwa Wachumia Tumbo.Watatupwa nje wengi kwenye kura ya maoni ndani ya CCM kama hawataendelea KUBAKA Katiba yao kama inavyofanyika sasa.Na utashangaa wanahama kwenye chama kengine mana ni Bendera hawa
 
Allute wewe jamaa unaakili mpaka unakera,Nakubaliana na wewe kabisa hawa jamaa watapata tabu sana 2020, Ni bora wangebaki CHADEMA waimarishe ulizi Wa kura wangetangazwa tu 2020.

Hakuna MTU anaweza kuua upinzani ni kweli huku mtaani wameichoka CCM balaaa,Kaka Mungu akubariki sana napenda wewe unajenga hoja tu hutukani wala hukashifu mtu!
 
Huu ni ukweli hata mbele ya Mungu. Nashangaa hawa binadamu vigeugue ambao hawajuwi hata kuhakiki akili zao hadi @ emmanuel allute afafanue.
Wangejuwa huko mbele wao ni pumba tu mbele ya ccm, wangejitafakari mapema.
Tatizo la kuangalia shida za leo lkn kesho hujuwi utaishi vipi. Akili fupi sana hizi.
 
Hizo ndoto za mchana watu washapiga hesabu wakaona zinalipa wamesepa na kijiji . Siku hizi hakuna biashara ya hasara kwa mtu anaetumia akili zake ...lakini kama wewe unasubiri akili za mwenzio zikuamulie maisha yako endelea kusubiri.
 
Umeniwahi mtoa mada.Hili ndio naliona kwa Wachumia Tumbo.Watatupwa nje wengi kwenye kura ya maoni ndani ya CCM kama hawataendelea KUBAKA Katiba yao kama inavyofanyika sasa.Na utashangaa wanahama kwenye chama kengine mana ni Bendera hawa
Wataenda kwenye chama cha lyatonga
 
Huo ndiyo ukweli mchungu kwa hao walioamua "kujipiga bei" kwa CCM



Tuendelee kuwaombea na kuwaelekeza zaidi, Wengine ni mkumbo tu ila 2020 itakuwa mbaya sana kwao wao na familia zao, Wasichezee kabisa pension zao kwani yajayo yanahuzunisha kwao.
 
Huo ndiyo ukweli mchungu kwa hao walioamua "kujipiga bei" kwa CCM



Tuendelee kuwaombea na kuwaelekeza zaidi, Wengine ni mkumbo tu ila 2020 itakuwa mbaya sana kwao wao na familia zao, Wasichezee kabisa pension zao kwani yajayo yanahuzunisha kwao.
 
Umeniwahi mtoa mada.Hili ndio naliona kwa Wachumia Tumbo.Watatupwa nje wengi kwenye kura ya maoni ndani ya CCM kama hawataendelea KUBAKA Katiba yao kama inavyofanyika sasa.Na utashangaa wanahama kwenye chama kengine mana ni Bendera hawa




Hawa jamaa Leo wanajiona mashujaa ila 2020 watalia na kusaga meno!
 
Back
Top Bottom