Itakuchukua Miaka Mingapi Upinzani kuja kushika Dola

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,675
Tumeona mifano ya Nchi kama Gambia,Ghana wao wameweza ila kule Uganda ni kinyume Mzee Besigye amepambana mpaka basi nasidhani kama ana hamu na siasa tena na kwa upande mwingine Zimbabwe Mzee Morgan Tsangirai nahisi hata Siasa hataki tena.

Kwa upande wa Jirani Zetu mzee Odinga Amejitahidi kufurukuta ila wapi.

NA hapa kwetu JE kuna siku kweli Upinzani utakuja kushika Dola au ndio Ndoto za Alinacha au baada ya miaka kama 100 hivi wakiwa na sera nzuri za kimaendeleo naza kueleweka na wanachi?
 
Hata Kama Watu wameichoka CCM wanaendelea kuichagua kwa kuwa hakuna mbadala!

Hivi kweli Uchoke Ufisadi wa CCM umchague Lowassa?

Hivi kweli ukerwe na Ukwepaji wa Kodi umchague Mbowe?

Hivi kweli uchoke usanii wa CCM umchague Lipumba?

Hivi kweli uchoke ujanja ujanja wa CCM umchague Zitto?

Ni sawa na wale wanaoilaumu kila Siku Radio Clouds kuwa inanyonya Wasanii lakin ukitafuta Rafio isiyonyonya huioni.

Wapinzani watumie nguvu kubwa kuonesha kuwa wanafaa kuongoza Nchi sio kutumia nguvu zote kutuambia kuwa CCM haifai kwani si tunajua haifai?!,

Hivi kweli Unafunga Safari kutoka Mtaa Ufipa kwenda mpaka Ikungi Singida au Mbambabay Ruvuma kumwambia Mkulima kuwa Serikali imekutelekeza kwenye Baa la Njaa? (Yeye ndio wa kuwaambia Nyie kuwa katelekezwa sio Nyie kumwambia )

Tumieni Muda mwingi kueleza kwanini nyie mnafaa na sio kutumia Muda wote kuwaambia CCM haifai.
 
Wataweza ila wakianza kufanya siasa safi kama za akina martin luther sio hizi za kihuni za kihamasisha fujo....kuchafulia wengine wakati na wao madhambi wanayofanya ni hayo hayo.

Sent from SONY EXPERIA Z5 PREMIUM
 
hata kesho inawezekana wapinzani wakachukua dola lakini endapo tu nao wataamua kutumia mbinu ovu kama za CCM!
 
Hivi kweli Unafunga Safari kutoka Mtaa Ufipa kwenda mpaka Ikungi Singida au Mbambabay Ruvuma kumwambia Mkulima kuwa Serikali imekutelekeza kwenye Baa la Njaa? Tumieni Muda mwingi kueleza kwanini nyie mnafaa na sio kutumia Muda wote kuwaambia CCM haifai
Umeongea kitu mkuu tena siku hizi wamekuja na kambinu wanasubiri mkuu azungumze halafu wao waje kuchambua neno moja moja na kumkosoa kwa mfumo huu sidhani kama watafika

Hata ukimkosoa baba yako nyumbani ila atabaki kuwa baba tu na hata akiamua kukuchapa viboko bado atakuchapa.

Opposition parties they need to do something extra na sio siasa za Fb watu siku hizi wanaangalia nani ataleta maendeleo na sio blaa blaa
 
Wataweza ila wakianza kufanya siasa safi kama za akina martin luther sio hizi za kihuni za kihamasisha fujo....kuchafulia wengine wakati na wao madhambi wanayofanya ni hayo hayo.

Sent from SONY EXPERIA Z5 PREMIUM
Ukiuliza Gambia walijapanga kwa miaka mingapi watakwambia hawakua na haraka waliacha wanachi waone waone wenyewe na wafanye maamuzi sahihi.

Kwa maoni Yangu Wapinzani wasingekimbilia Urais wangejijenga kwanza ngazi za chini anzia udiwani mpaka Ubunge wahakikishe wanawabunge wa kutosha halafu ndo waje kwa Uraisi sasa,Wale wale waanzilishi wa vyama walikua wanatosha kabsa...wakataka yote kwa pupa mwishowe wakakosa yote..
 
hata kesho inawezekana wapinzani wakachukua dola lakini endapo tu nao wataamua kutumia mbinu ovu kama za CCM!
Mkiendelea na kauli hizi ni ndoto za mchana kuja kushika dola.
 
Upinzani utakuchukua nchi siku ambayo!

1. Siku ambayo upinzani wataungana na kuwa kitu kimoja..

2. Siku upinzani watakapo acha unafiki na kuwa wakweli..mfano: lowassa akiwa ccm alikuwa fisadi ila alipoenda ukawa akawa msafi..

3.siku upinzani wataacha kuchumia tumbo na waweke utz mbele

4.siku wakieleza kwanini wao wanafaa na sio Taabu ingine
 
Chama kinachojinadi kupendwa hakitaki Tume huru ya uchaguzi , hebu waza juu ya hilo kisha ujijibu mleta mada. Hebu kumbuka wakurugenzi wanaosimamia hizi chaguzi ni wakereketwa waliopo hapo kwa maelekezo maalum.

Upinzani unania njema watawala hawana bali wanajijali wenyewe
 
Dah... Upinzani ulikuwa unakuwa vizuri katika msingi imara.... Ila Mbowe kwa tamaa yake ya fedha akatujazia nzi
 
Chama kinachojinadi kupendwa hakitaki Tume huru ya uchaguzi , hebu waza juu ya hilo kisha ujijibu mleta mada. Hebu kumbuka wakurugenzi wanaosimamia hizi chaguzi ni wakereketwa waliopo hapo kwa maelekezo maalum.

Upinzani unania njema watawala hawana bali wanajijali wenyewe

Tume huru Pamoja na Sheria ya kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani ilpelekwa na Serikal ya Jakaya Bungeni mkagoma Na kususia Bunge la Katiba kwa kuwa tu mnataka Serikal tatu,

mngekuwa na Akili mngetumia hiyo Fursa ya kupata Tume huru ili kuitoa CCM Mamlakani halafu ndio Mleta hiyo Serikali tatu lakin mkawa na Nakisi ya akili na Maarifa na Mikakati ya Kisiasa.

Kuweza kupata yote unayotaka kwny Mijadala ya Kisiasa hasa dhidi ya Serikal ni uhayawani wa Kisiasa! Leo hii mnalilia Tume huru ya Uchaguzi bila ya Serikal tatu sasa si bora mngeipitisha ile ile Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi?!
 
Hadi hv naandika SIJAONA chama mbadala na CCM wa kutuongoza!..acha wanaojiita upinzani waendelee kuota ndoto na kuozea mahabusu!..ila ukweli utabaki wazi..hakuna UPINZANI hapa tz.

Itachukuwa miaka 100 na zaidi km wapinzani hawajaamua kuungana na kuacha UNAFIKI na MASLAHI binafsi.
 
Tume huru Pamoja na Sheria ya kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani ilpelekwa na Serikal ya Jakaya Bungeni mkagoma Na kususia Bunge la Katiba kwa kuwa tu mnataka Serikal tatu,

mngekuwa na Akili mngetumia hiyo Fursa ya kupata Tume huru ili kuitoa CCM Mamlakani halafu ndio Mleta hiyo Serikali tatu lakin mkawa na Nakisi ya akili na Maarifa na Mikakati ya Kisiasa.

Kuweza kupata yote unayotaka kwny Mijadala ya Kisiasa hasa dhidi ya Serikal ni uhayawani wa Kisiasa! Leo hii mnalilia Tume huru ya Uchaguzi bila ya Serikal tatu sasa si bora mngeipitisha ile ile Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi?!
Pohamba usiwe mnafiki kwa nafsi yako . Kikwete aliweka mazingira magumu ya kukubaliana, si neno hawakupata Katiba ya wananchi kipindi hicho Lakini CCM si Mungu kitafika kipindi Katiba na Tume huru vyote vitapatikana. Tanzania sio kisiwa
 
Hata Kama Watu wameichoka CCM wanaendelea kuichagua kwa kuwa hakuna mbadala!

Hivi kweli Uchoke Ufisadi wa CCM umchague Lowassa?

Hivi kweli ukerwe na Ukwepaji wa Kodi umchague Mbowe?

Hivi kweli uchoke usanii wa CCM umchague Lipumba?

Hivi kweli uchoke ujanja ujanja wa CCM umchague Zitto?

Ni sawa na wale wanaoilaumu kila Siku Radio Clouds kuwa inanyonya Wasanii lakin ukitafuta Rafio isiyonyonya huioni.

Wapinzani watumie nguvu kubwa kuonesha kuwa wanafaa kuongoza Nchi sio kutumia nguvu zote kutuambia kuwa CCM haifai kwani si tunajua haifai?!,

Hivi kweli Unafunga Safari kutoka Mtaa Ufipa kwenda mpaka Ikungi Singida au Mbambabay Ruvuma kumwambia Mkulima kuwa Serikali imekutelekeza kwenye Baa la Njaa? (Yeye ndio wa kuwaambia Nyie kuwa katelekezwa sio Nyie kumwambia )

Tumieni Muda mwingi kueleza kwanini nyie mnafaa na sio kutumia Muda wote kuwaambia CCM haifai.
Nimekuelewa sana mkuu.
 
Mpaka wajue kuongea kwa utaratibu badala ya kufoka kwa kila jambo; yaani hata kwenye mambo ya kufuraisha wao wanaongea kama watu wananena kwa lugha!
 
Tume huru Pamoja na Sheria ya kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani ilpelekwa na Serikal ya Jakaya Bungeni mkagoma Na kususia Bunge la Katiba kwa kuwa tu mnataka Serikal tatu,

mngekuwa na Akili mngetumia hiyo Fursa ya kupata Tume huru ili kuitoa CCM Mamlakani halafu ndio Mleta hiyo Serikali tatu lakin mkawa na Nakisi ya akili na Maarifa na Mikakati ya Kisiasa.

Kuweza kupata yote unayotaka kwny Mijadala ya Kisiasa hasa dhidi ya Serikal ni uhayawani wa Kisiasa! Leo hii mnalilia Tume huru ya Uchaguzi bila ya Serikal tatu sasa si bora mngeipitisha ile ile Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi?!
Mpuuz mkubwa
 
Back
Top Bottom