Itabidi tu nivunje. Hakuna namna!

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,140
2,000
Wakati Sikukuu zinakaribia labisa nimeona niwashirikishe wenzangu hasa wazazi.
Kesho nimekusudia kuvunja Kibubu ili nione kilichomo ndani, ila nina mashaka na kile nitakachokikuta humo. Kibubu kinakaribia miezi Sita sasa ila sitegemei kufikia lengo, hasa kuhusu mavazi na maakuli ya Sikukuu japo Mchele na Ng'onda kwa huku uswahilini si haba. Hapa nazungumzia kitimtim na rabsha za watoto bila Nguo mpya walau zile za kwenye Mbao/mabango maarufu wanayoranda nayo wauzaji wa urembo huku uswahilini
. Nipate japo hizo tu, wanangu wajisitiri nami nisitirike japo kwa siku hiyo moja mbele ya macho ya wapangaji wenzangu. Sijali hata kama najua aina hii ya nguo huwa zinaishia kwenye beseni zinapofuliwa tu kwa Mara ya kwanza.
Ukweli hali ni ngumu sana pamoja na kujitahidi kote kutosa Jerojero kila siku, ilifikia wakati fulani miezi ya hapo kati niliishia kupata hela ya kuwaachia watoto kesho yake, kiasi inaweza kupita wiki nzima sijaweka hata Jero. Watoto nao haweshi kuugia vihoma mvurugo hata sijui vinakotokea. Ukienda huko zahanati zetu za uswazi (Arafa) ndo balaa hutoki humo bila kuambiwa mtoto eti ana Malaria,U.T.I (sijui) na Taifodi... Kha! Hapo inabidi tena nirudi nyumbani nitafute ule waya Wa dirisha mwembamba na mgumu ili nianze shughuli ya kuchomoa Jerojero bila kusababisha uharibifu kwa kibubu.. Jamani!
Kazi yangu ni kufyatua matofali kwa wenzangu na mimi wasio na uwezo Wa kununua ile mitofali ya kutetemeshwa kwa umeme. Mfuko mmoja wa Saruji tajiri anataka matofali Sitini na kila mfuko mmoja analipa shilingi 5,000 tu! Inabidi kukaza msuli na kuvimba kiume ni kazi ngumu inayotaka ustahimilivu hasa. Mchana kutwa japo mifuko Minne ifanyiwe kazi na kisha tugawane na mwenzangu kwani si kazi ya mtu mmoja shilingi 10,000 kila mmoja wetu. Toa chakula 1,500 na nauli ya kurudi Nyumbani na kesho kurejea kibaruani, hapo fanya Buku mbili kwa nauli tu. Na kwajinsi hali ilivyo siku hizi watu hawajengi hata wale wenzangu na Mimi wanaojenga chumba kimoja kimoja hawajengi tena kama zamani. Hali ni kama imefungwa Makufuli na ndani kuna Pombe au Kifaru John.
Sikukuu ndo hiyo watoto wanne na mwingine yupo kwenye Oven anasubiri kuepuliwa.
Kesho ndo kesho na sijui kama Kibubu kinacho japo elfu Ishirini.
Nitarudi kuwapa mrejesho wadau..... Asanteni kwa kunisoma!

Mwendabure si mkaa Bure.
 
House of Commons

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,850
2,000
Vunja baba, vunja tu, hamna namna...

emmanuel mhecha

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
934
1,000

Sina muda wa kusoma gazeti lako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom