Israel Sasa inatosha

Hii ni dalili kuwa hii vita Israel vita imewashinda.
 
Hayo yote yanatokea, Je? Palestine hawana Jeshi?
 
Basi sawa wasiache kupigana
Suala la wao kuendelea au kuacha kupigana hilo ni juu yao mm na ww hatuna maamuzi juu ya hayo.

Lamsingi dunia nzima ime jua ya kuwa jeshi la Israel bila Marekani ni JWTZ iliyo chagamka, kwanza hata hapo nimewapendelea.
 
Vita kuisha inabidi hao hamas wadhibitiwe kisawasawa.

Kuuliwa hao watoto ni matokeo ya ujinga wa hao hamasi,wao ndo sababu.

Wakiachiwa wataendelea kufanya huo ujinga sana.
Sasa Hamas utaidhibitije hali ya kuwa uwaacha hao Hamas badala yake unaenda kushambulia watoto na wanawake?
 
Nimejiuliza hii thread sasa, jinsi kichwa cha habari kilivyoandikwa ni kwaajili yetu, au netanyahu. Na je! Kama ni kwaajili yake. Atapataje hizi salamu😂😂😂😂😂.
 
Sasa Hamas utaidhibitije hali ya kuwa uwaacha hao Hamas badala yake unaenda kushambulia watoto na wanawake?
Sidhani kama hao idf lengo lao ni kuwaua hao raia.

Hamas ndo mdudu anatakiwa aangamizwe ili palestina iwe sehem salama.
 
Kabisa mkuu, tena Israel imekuwa ikiitumia Hamas kudidimiza uhalali wa mamlaka ya kipalestina kule west bank na kama mamlaka inayowakilisha Wapalestina wote.

Ikiambiwa izungumze na PA ya Mahmoud Abbas inasingizia hiyo mamlaka haiwakilishi wapalestina wote maana inawatawala west bank tu na haipo Gaza.

Ikiambiwa izungumze na Hamas inasema ni magaidi hawawakilishi Wapalestina wote.

Hivyo uhasama wa Hamas na PLO ya Mahmoud Abbas umetumiwa na Israel kuzima ndoto za Wapalestina kuwa na taifa lao huru.
 
Sidhani kama hao idf lengo lao ni kuwaua hao raia.

Hamas ndo mdudu anatakiwa aangamizwe ili palestina iwe sehem salama.
Sasa mbona anawauwa hao raia anawaacha Hamas?
 
Lakini hilo taifa lilishindwa kupatikana kwa zaidi ya miaka 60 kabla ya hiyo hamas haijaitawala gaza.
 


Hao magaidi ndo wanaua hao watoto, sio Israel, hamas wamejenga mahandaki chini ya hizo shule na hospital, hakuna namna, watauwawa tu.
 

Kwa Sasa Hamas Hana uwezo wa kurusha roketi. Roketi anarusha Hizbollah. Kwa kuwa Israel kashamdhibiti Hamas , ni Bora wakubaliane wawaachie mateka na Hamas waliobakia waendee Misri au Lebanon.
 
Hapo wa kulaumiwa ni Hamas, kwa nini wanapigana vita halafu wanakimbilia kujificha hospitali?!
Ukute kuna lango la kuingilia kwenye mtandao wa mahandaki humo hospital.
Naunga mkono hoja kama tu Hamas wakiachia mateka, vinginevyo kipigo kiendelee

Hamas ni wajinga Sana. Na sidhani Kama wanawapigania wapalestina. Maana ni hao Hamas waliwatimua PLO au Fatah hapo Gaza ili wabaki wenyewe, na kujifanya Gaza kujitawala. Nadhani wakiondoka Palestina itakuwa huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…