Israel mambo yamewafika hapa. Watishia kuipiga Lebanon kama dunia itashindwa kuwaondoa Hizbullah mpakani. Je, wataweza?

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,194
10,929
Mmoja ya waziri katika baraza la vita la Israel, Benny Gantz ameweka wazi kuwa muda wa majadiliano unakaribia kuisha na kwamba nchi yake itaingia kuipiga Lebanon yote iwapo Serikali ya nchi hiyo na dunia kwa ujumla watashindwa kuwaondoa wapiganaji wa Hizbulah kutoka mpakani kaskazini ya Israel.

Kauli hiyo imekuja baada ya jana HIzbullah kunyesha mvua nyIngine ya makombora ndani ya Israel.
Suala ni jee IDF wana uwezo huo tena huku wakiwa hawajafanikiwa kwa malengo yake ya kuivamia Gaza ikiwa ni kujpigana na jeshi ambalo lina silaha zaidi kuliko Hamas?

Kauli kama hiyo tayari wameshaitoa kwa wanamgambo wa Houth walio kusini yake japo mbali na mpaka. Bado hawajatekeleza kitisho hicho.

Israel Gaza war: Israel warns Hezbollah and Lebanon over border fighting

Ukiona Israel anaomba mazungumzo na nchi wapate muafaka wa kisiasa basi ufahami hali mbaya kwake, huo ni mkwala tu anaishambulia Lebanon na yeye miji yake itachaka kwa makombora siyo mara ya kwanza vita vya mpaka UN akaingilia kati.
Watu wanataka kurudi makwao hawawezi tena.Kachanganyikiwa na vita.
idadi kubwa ya raia wapo maeneo ya kati kama wakimbizi.Wao na wapalestina hawachekani sana.
 
Hizbullah kamatieni hapo hapo msiachie hata robo
Israhell haiwezi kuingia tena vitani na Hizbullah hawawezi
Mwanzo walijua watu watakurupuka tu huku hamas kule Hizbullah pale houthi waingie kwapamoja
Kwanza kaachiwa ghaza ahangaike nayo na bado inamhenyesha
Huku kuna mti mwengine umeanza kuchepua
Amalizane na hamas kwanza Hizbullah haiwezi
 
Hezbollah inao uwezo wa kupigana na jeshi la Syria hii ya sasa iliyodhoofika?

Hezbollah ina uwezo wa kuipiga Misri?

Hezbollah ina uwezo wa kuipiga Jordan?

Hizo nchi tatu zote Hezbollah haina uwezo wa kuzipiga. Na zote hizo hakuna ya kuipiga Israel.

Tufanye hivi, Lebanon wasiiguse Hezbollah. Israel iivamie Lebanon, wewe waombe Hezbollah wasije peke yao waje na jeshi la Lebanon kwa pamoja uone kama watashinda.
Mambo ya story za six deiz war, na operation entebbe.
Mkuu Israel haina uwezo kupambana na Hezbollah, Hezbollah ni powerful asikuambie mtu.
 
Israel iliyopigana na mataifa 10 ya kiarabu ndo washindwe na vikundi hivyo 3 kweli! Alizichapa nchi 10 hatimaye wakichukuliwa Jerusalem, Golan na Sinai. Hao hezibolla ndo wanawasha moto, watapigwa mpaka wachakae
Wanadhani Hezbollah hapigiki. Uzuri wa Lebanon kuna serikali inayotambulika kimataifa, tofauti na Gaza. Kule Gaza unaweza sema Hamas ni kundi la kigaidi hivyo ukalaumiwa kuingia. Kule Lebanon utasema ni nchi halali inayoruhusu watu wake kuivamia Israel.

Unaingia Lebanon jeshi lao likikuzuia unapigana nalo, hakichukui muda sababu halijifichi shuleni na hospitalini. Hezbollah wakirusha makombora unarusha makombora mazito. Israel haijatumia cruise missiles wala MLRS dhidi ya Hamas sababu ni magaidi wamehodhi eneo la raia ila kwa Lebanon zinatumika vizuri.
 
Hezbollah inao uwezo wa kupigana na jeshi la Syria hii ya sasa iliyodhoofika?

Hezbollah ina uwezo wa kuipiga Misri?

Hezbollah ina uwezo wa kuipiga Jordan?

Hizo nchi tatu zote Hezbollah haina uwezo wa kuzipiga. Na zote hizo hakuna ya kuipiga Israel.

Tufanye hivi, Lebanon wasiiguse Hezbollah. Israel iivamie Lebanon, wewe waombe Hezbollah wasije peke yao waje na jeshi la Lebanon kwa pamoja uone kama watashinda.
Israel kwenye vita ita focus sana kwenye air force hilo kila mmoja analifahamu. Lakini kwa ground watachakazwa mno.
Lakini hawatoweza kuzuia rocket attacks kutoka kwa Hezbollah.

Point ya kushinda vita ni kufanikisha objectives zako, kufanikisha malengo flani, sasa hapo Israel atashinda vita vipi?
Israel haina huo uwezo, inapigana na warusha mawe hadi leo hamna kitu, wameshindwa kurudisha mateka wapo pale pale Gaza.
 
Wanadhani Hezbollah hapigiki. Uzuri wa Lebanon kuna serikali inayotambulika kimataifa, tofauti na Gaza. Kule Gaza unaweza sema Hamas ni kundi la kigaidi hivyo ukalaumiwa kuingia. Kule Lebanon utasema ni nchi halali inayoruhusu watu wake kuivamia Israel.

Unaingia Lebanon jeshi lao likikuzuia unapigana nalo, hakichukui muda sababu halijifichi shuleni na hospitalini. Hezbollah wakirusha makombora unarusha makombora mazito. Israel haijatumia cruise missiles wala MLRS dhidi ya Hamas sababu ni magaidi wamehodhi eneo la raia ila kwa Lebanon zinatumika vizuri.
Nilichojifunza kwenye migogoro ya hivi karibuni watu wanazani Hivi vikundi vya ugaidi vinanguvu kushinda Israel kisa vinarusha makombora ovyo.
 
Mambo ya story za six deiz war, na operation entebbe.
Mkuu Israel haina uwezo kupambana na Hezbollah, Hezbollah ni powerful asikuambie mtu.
Mnakuja na mambo ya kijinga kila siku huku mnachakazwa tu pamoja na kobazi wenzenu.
Kwa taarifa yako hizbollar ni kiporo tu atapigwa mpaka anye.
Kwanza waliingilia ugomvi huu wa Ghaza mapema tu oct 7,wakafurushwa mpk kwao.
Sasa kuna jipya hapo.
Wazayuni wanaenda kote huko ndo mana wamesema vita sio leo wala kesho itaisha.
 
Back
Top Bottom