Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,626
- 46,270
Bila kwenda mbali kuhusu Historia ya mgogoro na vita inayoendelea sasa kati ya Israel na Hamas ukanda wa Gaza ni wazi Utawala wa Netanyahu umekosea pakubwa kimkakati katika hii vita.
Kuanzisha vita mara nyingi huwa ni jambo rahisi sana ila kuimaliza na kutimiza malengo huwa jambo gumu sana na la kutoa jasho kila sehemu. Ni mara chache sana vita huwa zinaenda jinsi mikakati na malengo yalivyopangwa.
Baada ya ugaidi wa September 11 US walienda kwa pupa katika vita vya Afghanistan na Iraq. Kilichotokea ni kwamba utawala wa Taliban ulianguka ndani ya miezi miwili ya uvamizi ila US wakaendelea na vita visivyoisha kwa miaka 20 na matumizi ya zaidi ya Dola Trillion 2 wakitumia kila siku ya vita hiyo $million 300. Hatimaye US wakaondoka Taliban wakatoka milimani na kwenye mapango wakaingia Kabul na sasa wanaendelea kuitawala Afghanistan.
Mfano mwingine wa karibuni kabisa ni jinsi Urusi waliivamia Ukraine wakijua watafanya Operation ya wiki moja Kyiv ianguke waweke kibaraka wao, sasa kwa miaka miwili bado wanaendelea na vita visivyoisha huku majirani zake wakizidi kujiunga NATO, huku ni hesabu kwenda mrama kabisa.
Israel nayo imeingizwa kingi kwa Hamas. Ni kweli kitendo cha Hamas kuvamia na kuua raia 2000 upande wa Israel kisingeweza kuvumilika bila kujali kiini cha huo mgogoro wa muda mrefu, ila Israel kuingia Gaza na kuua raia mara kumi zaidi(20,000) nacho hakiwezi kuvumiliwa hata na washirika wake.
Matokeo yake sasa ni kwamba Israel imewaweka katika hali ngumu washirika wake wa magharibi. Japo West hawakubaliani kabisa na Hamas pia hawakubaliani na jinsi Israel inavyoendesha vita hiyo japo hawasemi kwa sauti kubwa. Baadhi ya maseneta na wanaharakati wa US wanapinga kabisa nchi yao kuendelea kupia Israel silaha, wanasiasa wengi wa Ulaya wenye ushawashi wanapinga pia jinsi hali ya vita Gaza inavyoendelea.
Israel japo ni kama wanakaribia kuisawazisha kabisa Gaza kwa mabomu bado inaonekana vita haitaisha na suluhu haitapatikana kwa muda mrefu sana kwa sababu kwa kuanzia wenyewe hata hawana mpango wowote kabisa wa maana wa jinsi ya kudilia na Wagaza zaidi ya milioni 2 baada vita hii. Ile huruma waliyopewa na sehemu kubwa ya dunia baada ya uvamizi wa Hamas inaishilia na mahusiano yao na Waarabu yaliyokuwa yameanza kuwa mazuri sana kuna uwezekano mkubwa yakaharibika kabisa kwa sasa.
Vita mara nyingi ni kama kuingia katika kichaka cha miba ya michongoma, unaweza kuwa unajichomoa upande mwingine kumbe upende mwingine unajiingiza, kutoka huwa sio rahisi sana.