Kwa hiyo ina maana iran wanapinga jina la israel tu! maana Hata israel ya sasa ina wayahudi na waarabu.Hawa 24000 unaowasema sio waisrael, ni wairan wayahadi. Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa muyahudi na kuwa muisrael, kwa hiyo hawa jamaa ni wairan kama ambavyo usingewaita wamarekani weusi waafrika kwa sababu tu ya uweusi wao. Tatizo la Iran na Israel sio racial, ni national... wairan hawaamini kwamba Israel ni taifa, wanaamini ni kiotesho cha ukoloni wa marekani na uingereza mashariki ya kati. Kama inavyojulikana kabla ya mwaka 1948 hapakuwa na taifa linatitwa israel, limeanzisha kwa resolution ya UN 1948. Kwa hiyo Israel ilitengenezwa NYC ikabandikwa kwenye ardhi ya Palestine iliyokuwa koloni la Uingereza. Kama mnavyojua wakoloni wa kiingereza walijaribu hata Afrika kule Zimbabwe kubandika wajukuu zao wakina Ian Smith ambao baadaye tukawang'oa kwa msaada wa marafiki kama Cuba na baadaye Marekani baada ya supporters wao SA kuanza mipango ya nyuklia na bwana mkubwa kuwageuka.
Kwa hiyo kimsingi ugomvi uliopo kati ya Irani na Israeli upo katika hoja kwamba Israeli siyo taifa. Taifa ni Palestine, yenye waarabu na wayahudi (kama ilivyo Irani), yenye wakristu, waislamu, judaism nk. Kusema Israel isiwepo si sawa na kusema wayahudi wasiwepo, wanachodai hawa watu ni kuwa na taifa moja la Palestine kama zamani itakayokuwa na waarabu na wayahudi na kwamba wote kama wana wa Mungu wana haki sawa juu ya ardhi waliopewa na Mungu.
GZ
kwenye magari bado iran anasaidiwa na west-yupo anafanya utengenezaji na mjerumani,ndio maaana husikii mjeruman akizungumza juu ya swala la iran,maana wao wanjuana kwa terms zao,Iran si nchi dhaifu kama unavyofikiri. Marekani na Israel zinatapatapa kwani zinaona Iran imekuwa na uwezo mkubwa kuwashinda japokuwa wamewawekea vikwazo tokea mwaka 1979. Sasa hivi, hii ni industrialized country kwa kujitengenezea kila kitu kwa mahitaji yao ikiwemo matrekra, magari, treni za mafuta na zile za umeme, manowari za kivita, ndege za abilia na za kivita, ndege zinazokwenda bila rubani (drones), settellite, meli za kivita, makombora ya masafa mafupi, marefu na ya kati, boti za kivita zisizooneka kwenye mfumo wa rada au settellite na sasa wanajiandaa kutuma wanasayansi wao katika anga za mbali.
Wanapanga kuisambaratisha nchi hii lakini watashindwa kwani hii sio mara yao ya kwanza. Walijaribu mara kadhaa na kushindwa kuidhibiti kwani askari wa Iran waliwahi kuwadhibiti askari wao kabla hawajaleta madhara kwa nchi hii. Kwa taarifa yako vita vya siku 33 kati ya Hizbullah na Israel, vilikuwa si vyao hasa bali vilikuwa vita kati ya Marekani na Iran. Na Israel ilidhibitiwa vilivyo mpaka leo inawaheshimu vilivyo Hizbullah. kuthibitisha hilo marekani iliagiza Hizbullah wanyang'anywe silaha lakini wao walipinga wakasema hakuna jeshi lolote duniani linaweza kuwanyang'anya silaha na mpaka leo wanazo silaha zao.
It is interesting to note that the world countries supporting Iran and its nuclear program are countries with a history of denying basic human rights, religious persecution, subjugation of women, and a flat refusal to work constructively with the rest of the International community.
So the planned attack on Iranian nuclear facilities will be a solution for the oppressed?
Btw, the so called free world (International community) cannot even support freedom and peace for the Palestinian people from the oppression by the Zionist (Israel) regime...