Nafikiri hujajua dunia inapoelekea ila kama u mfatiliaji mzuri kuna nabii mmoja T. B. Joshua ametabiri kuwa kuna vita ya tatu ya dunia itatokea mwaka huu ambayo itaanzishwa na Israel na washirika wake Marekani na Uingereza dhidi ya Iran na washirika wake ambao ni China na Urusi na Japan. Niliangalia unabii huo Emmanuel TV.
Haya Mkuu sijui unaihsi dunia gani, by the way mimi si mlokole kwa hiyo huyo unayemwita nabii T.B. simfuatilii hata kidogo. By the way kwa sasa hakuna Urusi dunia hii, Urusi ilisambaratika karibu miaka 20 iliyopita imebaki nchi moja inayoitwa Russia, na jamhuri nyingine ndogo ndogo. Halafu ukumbuke pia kuwa China, Russia na Japan si washirika wa Iran, ni nchi zinazoangalia economic interests zao.
Osirak reactor ilikuwa moja na open air, lakini Iran ina sites 17, nyingi ziko deep under ground some of which are already operational. Not even the heaviest bunker busters can bust some of these. Kwa hiyo kuzulinganisha sites hizo na Osirak ni ufinyu wa mawazo.
Kelele zote za Israel ni vitisho tu, yenyewe haiwezi kuanzisha vita inajua fika kuwa kijeshi haiwezi kudeal na Iran bila msaada wa nchi nyingine kubwa.
Kama kweli unafikiri kuna nchi sasa ina interest na vita utakuwa wa ajabu sana, Japan, UK uchumi wake una matatizo, vita haiwezi kuwabenefit, China imeanza kuyumba, Russia haina uchumi wenyewe kuweza kuisupport kuanzisha vita, angalia shape ya uchumi wa dunia kwa sasa uone kama ina support vita unayosema ameisema T.B. joshua.