Mimi naona uwezekano upo kwa kuwa wamewahi kupiga maeneo yaliyosadikiwa kuwa ni nuclear facilities huko Iraq mwanzoni mwa miaka ya themanini na vilevile waliwahi kufanya hivyo kwa upande wa Syria!
shame on you man!!!!!,unashabikia ujinga huku ukidhani kwamba wale wasioamini katika imani yako basi wanastahili kufa.kumbuka nguvu za kijeshi walizonazo mataifa ni kwa ajili ya maangamizi ya watu,tena mbaya zaidi wahanga huwa ni maskini wasio na hatia.Siungi mkono Iran kuwa na silaha za nyuklia,lakini ningeona maana zaidi kama wanomzuia kuwa na silaha hizi nao wangekuwa hawana nyuklia.AMERICA(USA),ISRAEL.UNITED KINGDOM,FRANCE.GERMAN AND CHINA.zoote hizo zina silaha za nyuklia lakini ni wao ndio wabeba bango wakubwa dhidi ya mwenzao Iran kumiliki kile ambacho wao wanacho,.
Kumbuka.NYUKLIA ni technology ya juu kabisa kupata kutokea duniani.Ni teknologia mkombozi kwa nchi husika kwani hutoa fursa ya kupata nishati ya uhakika bila kuharibu mazingira.Mataifa yaliyopiga hatua kubwa kiuchumi na technology hayataki kuona wengine wakijikomboa,kwani wanajua ukombozi wa kiuchumi huwa ni ukombozi wa kifikra na ukijikomboa kifikra basi hutaweza kuvumilia ukoloni.
Iran hata kama inaongozwa na wendawazimu, haiwezi kuweka rehani uhai wa taifa lao eti tu kwa kujifurahisha kwa kuishambulia israel.huku ikijua dunia nzima itakuwa against nao.wao wanatafuta technology ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia(mohammed albaradei kathibitisha hilo)
Nawapa pole wote wenye fikra za kitumwa mnaoamini maendeleo yataletwa na wageni bila nyinyi wenyewe kujituma kama walivyofanya wachina na wahindi na sasa wanavyofanya wairani.
Kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia , kule Urusi walikuwa wakipokea wanafunzi wengi miaka ya 50s na 60s kutoka China. Machina walikuwa hawana girl friend wala birthday celebrations . Kazi yao ni kitabu tu . Hakuna Jumamosi wal Jumapili.
Machina hawa ndio walio-sacrifice starehe zao na ndio waliokuja kuiinua China hii ya leo.
Kinyume na waafrika wao kila weekend lazima wafanye parties. Waaalikwe wasichana ,Pombe ndio ushindwe mwenyewe. Kila mwezi walikuwa na Birthdays kama vile huzaliwa kila mwezi.
Afrika kweli inaweza kupata maendeleo????
Uwezekano wa mitambo ya Iran kushambuliwa ni mdogo kwakuwa wamejifunza kutokana na makosa ya Saddam aliejenga mitambo yake yote sehemu moja. Iran wamejenga sehemu 12 tofauti nchi nzima na nyingi ziko chini ya ardhi zimefunikwa na zege nzito.Mabomu yanayoweza kupenya zege hilo yapo Marekani na Urusi tu na Bush alishakataa kuwapa Israel mabomu hayo.Kitu kingine mashambulizi lazima yapite anga ya Iraq ambayo ni vigumu bila ruhusa na msaada wa Marekani na pia Iran imeshasema ikishambuliwa itachukulia imeshambuliwa na Marekani kwa hiyo majeshi ya Marekani yalio mashariki ya kati wajiandae kushambuliwa.
Kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia , kule Urusi walikuwa wakipokea wanafunzi wengi miaka ya 50s na 60s kutoka China. Machina walikuwa hawana girl friend wala birthday celebrations . Kazi yao ni kitabu tu . Hakuna Jumamosi wal Jumapili.
Machina hawa ndio walio-sacrifice starehe zao na ndio waliokuja kuiinua China hii ya leo.
Kinyume na waafrika wao kila weekend lazima wafanye parties. Waaalikwe wasichana ,Pombe ndio ushindwe mwenyewe. Kila mwezi walikuwa na Birthdays kama vile huzaliwa kila mwezi.
Afrika kweli inaweza kupata maendeleo????
Tuna endekeza siasa ktk kila kitu hata pale pasipo hitaji siasa.