R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,578
| [TD="bgcolor: #ffffff"] MWENYEKITI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Ismail Aden Rage, Jumapili iliyopita alipata wakati mgumu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, baada ya kuandamwa na nyimbo za kejeli zilizoambatana na zomea-zomea ya chinichini kutoka kwa kikundi cha hamasa maarufu kama Wakali na Mnarani. Rage alikumbwa na zahama hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mkoa, Fatma Mwassa, Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini, Suleiman Kumchaya, wakati timu ya Simba ikicheza mechi ya kirafiki na timu ya Rhino Rangers ya hapa. Hatua nyimbo hizoo kuanza kuimbwa ilianza baada ya Rhino Rangers kupata bao katika dakika ya 15, hivyo kundi kuanza kuimbanyimbo za kejeli dhidi ya Rage huku wakimtaja kwa jina lake kwa nguvu. Nyimbo ambazo kundi hilo ambalo nalo linafanana na kundi maarufu la Muchacho la jijini Dar es Salaam, waliaanza kuimba mbunge wetu timu mbovu aibu kwako, mbunge wetu ingia ucheze. Aidha nyimbo hizo za kutunga papohapo nyingine zilisikika hivi mbunge timu mbovu ingia ucheze wewe kama hali ndo hii 2015 itakuwaje,huku wakidai tuachie Simba yetu ubaki na ubunge wako, .na mara nyingine walisikika wakitamka kila jambo hawezi aaaa! Wakati hayo yakiendelea, mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa na mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Suleiman Kumchaya waliokuwa wakiingia uwanjani kwa nyakati tofauti, Mwassa aliimbiwa mamaa mamaa huyo mamaa.huku Kumchaya akiimbiwa baba..baba baba karibu. Aidha vijana hao ambao muda wote walikuwa wakiimba nyimbo za kumkejeli Rage walikuwa hawachoki kiasi mara kadhaa watazamaji waliacha kuangalia mpira na kuanza kuwangalia vijana hao kwa vicheko. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge Rage kujikuta kwenye hali hiyo, baada ya mwezi jana mbunge huyo na baaadhi ya viongozi wa CCM kukumbwa na zomezomea kwenye mkutano wao wa hadhara. Hata hivyo wakati vijana hao wakiendelea na nyimbo zao Rage alionekana kutokuwajali. Katika mechi hiyo, Simba ilishinda 3-1 yakifungwa na Nassor Masoud Chollo na Edward Christopher aliyecheka na nyavu mara mbili huku bao la Rhino Rangers likipachikwa wavuni na Said Kipanga. |
[TD="bgcolor: #ffffff"]
| |
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
[/TD]