KWELI ISLM, Islamic Coin: Cryptocurrency ya kiislamu yaidhinishwa na Fatwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Miaka ya 2000s imekumba na mabadiliko mengi ya kiteknolojia ikiwemo uwepo wa safaru za kidigitali ambazo haiziwezi kudhibitiwa na mamlaka za serikali (Benki Kuu). Sarafu za kidigitali zinazotambulika hadi sasa ni pamoja na BitCoins na OneCoin.

Sarafu nyingine ya Islamic Coin (ISLM) imeibuka. Hivi karibuni kumeibuka madai kuwa sarafu hiyo imetambuliwa na Fatwa kuwa ni halali kutumika na waislam.

2022_06_27_09_41_16_coin3.jpg_600_600_.png
 
Tunachokijua
Mbali na kuwa suala la Blockchain na Cryptocurrency kwa ujumla kuwa ni mjadala mkubwa kwa wachumi, baadhi ya wanazuoni wameonesha suala la fedha hizi linatambulika katika uchumi wa kiislamu.

Fatwa ni maoni au uamuzi wa kisheria unaotolewa na mwanazuoni mwenye sifa (mufti) kuhusu suala maalum linalohusiana na sheria ya Kiislamu (Sharia). Fatwa kwa kawaida inategemea tafsiri ya vyanzo vya Kiislamu kama vile Quran na Hadith, pamoja na mapokeo yaliyoanzishwa na wanazuoni wa kisheria wa hapo awali.

Tunachojua ni kuwa, ni wanazuoni watano wa kiislamu ambao wametajwa kutambua (endorse) sarafu hiyo. Wanazuoni hao ni Sheikh Dr. Essam Khalaf Al-Enezi, Sheikh Dr. Nizam Mohammed Saleh Yaquby, Sheikh Mohamed Abdel Hakim Mohamed, Sheikh Dr. Mohamed Zoeir, na Sheikh Mohamed Abdel Hakim Mohamed.

Wanazuoni hao ambao hawajatajwa kuwa na taasisi mahsusi inayojihusisha na masuala hayo wametajwa na website ya Islamic Coin kwa maana hakuna website nyingine yenye taarifa ya uhalali wa taarifa hiyo.

Aidha, duniani kuna taasisi nyingi za Fatwa na inawia vigumu kuangalia namna ambayo taasisi hukasimisha madaraka na kutoa nafasi ya wanazuoni kutoa mawazo ya vitu vya kitaalamu.

Crypto-Currency ambayo inachukuliwa kuwa ni aina ya uwekezaji na kufanya malipo hata hivyo kutokana na kukosa "Centralization" sarafu hizo zimekuwa na tabia ya kubadilika thamani kwa ghafla sana.
Nilisikia Saudi Arabia waliharamisha mambo haya, je hii haihusiani nao? Pengine hakuna uhusiano Kati ya Uislamu na Saudi Arabia pia, tueleweshane.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom