Jana wakati naangalia BBC mtangazaji alikua ana mu interview askari wa serikali ya Iraq. Jamaa akawa anasema silaha walizoahidiwa na NATO bado hazijaja hivyo wanawashindwa IS fighters ambao wana superior weapons.
Na kila nikiangalia news, hawa IS fighters wanazunguka na ma V8, Hilux za 2014 na ma landcruiser makali tu, achana na hizo silaha walizonazo ni hatari aisee.
Sasa nikawaza, Western world yote iko against wao, mpaka nchi zao wenyewe zakiarabu haziwataki hawa vichaa. Urusin naye hawezi kuwa support hawa extremists kwasababu naye walimletea fujo sana Chechneya. Na China haiwezi ikawa inawa supply ammunition hata siku moja wakati dunia nzima ambayo inategemea soko lake wako against IS.
Swali: Hawa jamaa wanapata wapi constant na dependable supply ya weapons, mafuta na silaha kuliko hata wanajeshi wa serikali wanaokua supported na dunia nzima?
Kipindi wanaanza harakati zao, target yao ilikuwa ni kuteka kambi za kijeshi, ambapo walipata silaha za kutosha. Pia walikuwa wanavamia mabenki, ambapo walichukua mpunga wa kutosha. Hivyo hawa jamaa fedha na silaha kwao si tatizo kabisa.
1. Kama waliteka kambi za kijeshi na kupora silaha, lazima patakua na storage areas ambazo ni rahisi kwa westerners kulenga. Na pia supply system ya kutoka storage hadi kuwa soldiers wa frontline inatakiwa iwe sophisticated sana.
2. Hio ya kuvamia ma benki aisee naya ngume kumeza, sawa tufanye kweli wameiba malori ya dollars. Nani anawauzia?
Kipindi wanaanza harakati zao, target yao ilikuwa ni kuteka kambi za kijeshi, ambapo walipata silaha za kutosha. Pia walikuwa wanavamia mabenki, ambapo walichukua mpunga wa kutosha. Hivyo hawa jamaa fedha na silaha kwao si tatizo kabisa.
HUU UONGO peleka chekechea,eti walipora maghala ya silaha na benki.
Silaha walipewa na NATO, this is not even a secret, refer 2-3 years ago, walivyoanzisha ugomvi na ASSAD utajua walipata wapi silaha.
Kuhusu PESA, zimetoka Western Countries na QATAR, hili liko wazi wala sio siri, sema kwa kuwa dunia imejaa watu wenye akili za kuku na kumbukumbu za sisimizi, ndio maana hawa CIA operatives wanaweza kucontrol naratives watakavyo.
Umesahau Kampeni za ku-free SYRIA, enzi hizo ilikuwa hip kusupport Arab Spring?Umesahau jinsi hawa jamaa walivyokuwa wanarecruit fighters mchana kweupe mitaani huku Ulaya?leo hii vijana wa kizungu wamegeuka wauaji, wanachinja watu hovyo kwenye TV wanajiuliza what happened.