wewe ni muongo, tunaishi na waislamu na wanashabikia wakristo kuuawa eti ni makafir, Kwa hiyo uislamu ni ugaidi kabisa, si ndo nyie mkiuwa kafir Kwa kujilipua mnaenda peponi na kupewa wabikra 72 na juice tamu?
Uislamu Unasemaje Juu ya Ugaidi?
Uislamu, Dini ya rehma, hauruhusu ugaidi. Katika Qur-aan, Mwenyezi Mungu Amesema:
“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni
makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu Huwapenda wafanyao uadilifu.” (Qur-aan, 60:8)
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakataza askari dhidi ya kuwaua wanawake na watoto,[ 90 ]na alikuwa akiwashauri:
((...Msisaliti, msizidishe sana, msimwue mtoto mchanga.))” [ 91 ]
Alisema pia:
((Mwenye kumuua mtu aliye katika mkataba na Waislamu, hataipata harufu ya Peponi, ingawa harufu yake hupatikana mpaka katika umbali wa mwendo wa miaka arubaini.))[ 92 ]
Kadhalika, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kutoa adhabu ya moto.[93 ]
Kuna wakati aliorodhesha dhambi ya kuua kuwa ya pili miongoni mwa madhambi makubwa,[ 94 ]
hata akatahadharisha hilo juu ya Siku ya Hukumu, (( Kesi za mwanzo kuhukumiwa baina ya watu ka tika Siku ya Hukumu zitakuwa ni zile za umwagaji damu. 95 )) [ 96 ]
Waislamu huhimizwa hata kuwa wakarimu kwa wanyama na wamekatazwa kuwadhuru. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema siku moja:
((Mwanamke aliadhibiwa kwa sababu alimweka paka kifungoni mpaka akafa. Kwa minajili hii, aliangamiziwa Motoni. Wakati alipomweka kifungoni, hakumpatia paka chakula wala kinywaji, wala hakumwacha huru ale wadudu wa ardhini.)) [ 97 ]
Pia alisema kuwa kuna mtu alimpatia kinywaji mbwa aliyekuwa na kiu kikali, hivyo Mwenyezi Mungu Alimsamehe madhambi yake, kwa kitendo hiki. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je, sisi hulipwa kutokana na ukarimu wetu kwa wanyama?” Alijibu:
((Kuna malipo kwa ukarimu kwa kila mnyama hai au mwanaadamu.))
[ 98 ]
Zaidi ya hayo, wakati wa kuchinja mnyama kwa ajili ya chakula, Waislamu wameamrishwa kufanya hivyo katika namna inayopelekea hofu ndogo na mateso madogo sana kwa mnyama, kadiri itakavyowezekana. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mnapomchinja mnyama, fanyeni katika njia iliyo bora zaidi. Mchinjaji akinoe kisu chake kwa ajili ya kupunguza mateso ya mnyama.)) [99 ]
Kutokana na mwangaza wa haya na mafundisho mengine ya Kiislamu, kitendo cha kuchochea khofu katika nyoyo za raia wasio na ulinzi, uharibifu wa majengo na mali, ulipuaji mabomu na kuwalemaza wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia, yote haya yamekatazwa, tena ni matendo ya kuchukiza kwa mujibu wa Uislamu na Waislamu. Waislamu wanaifuata Dini ya amani, huruma na msamaha, na wengi hawahusiani na matukio ya vurugu ambayo baadhi yamehusishwa na Waislamu. Ikiwa Muislamu mmojawapo atajihusisha na kitendo cha kigaidi, mtu huyo atakuwa katika hatia ya kukiuka sheria za Uislamu.
[90 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1744, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 3015
[91 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1731, na
At-Tirmidhiy, Na, 1408
[92 ]Imeandikwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy, Na. 3166, na Ibn Majah, Na. 2686
[93 ]Iko ndani ya Abu Daawuud, Na. 2675
[94 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 6871, na Swahiyh Muslim Na. 88
[95 ]Hii inamaanisha kuua na kujeruhi
[96 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1678, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 6533
[97 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 2422, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 2365
[98 ]Hadiyth hii ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imeelezwa kwa kirefu hapo nyuma. Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim
Na. 2244, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 2466
[99 ]Imeandikwa katika Swahiyh Muslim, Na. 1955 na At-Tirmidhiy,
Na. 1409