Ishu sio kufa, ishu nyumbani umejenga?

Notorious thug

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
2,817
10,594
Samaleko wana Jukwaa na Moderators kwa ujumla.

Unapotokea msiba wa mtu maarufu hapa nchini kuanzia Viongozi, Wafanyabiashara na Wasanii kumekua na mtindo kwenye mitandao hii Jamii watu wakitaka kufahamu mazingira na nyumbani kwa mfiwa kuna Nyumba nzuri? Amejenga?

Ni mtindo uliozuka baada ya kufa kwa Mama mzazi wa msaniii (sina uhakika kama ni msanii au mzugaji) Lulu Diva nimeona watu wakipasifia kwa Membe. Leo naona macho yataelekweza kwa Ndugu Marehemu "Le Mutuz" na wengi wameanza kuhoji kama amejenga?

tLbZCRM7jAKenya-small-mud-hut.jpg
 
Kwani ukifa unazikwa ndani ya nyumba?

Membe mnatafuta njia ya kumpa ujiko lakini ukweli umeonekana,yeye aende tu na hayo ma visasi yake.

Kwa ujumla ni kwamba Membe hatasimama tena!

Kama alivyowahi kusema yeye mwenyewe kuhusu magufuli kutosimama tena!

Na hili liwe fundisho kwa wapika sumu mlioko humu JF, mjifunze kuelewa.
 
Hii ishu ya kujenga iwahusu wote wale maarufu nchini ambao wakifa taifa zima litapata habari kutokana na umaarufu wao na hasa hao waliopo jijini dar. Siku wakifa wahakikishe makwao wamejenga kulingana na hadhi zao. Sio wanaonekana luningani wako smart kumbe kwao pamechoka, nyumba ya ajabu, choo paspoti size, pazia gunia. Somo pia kwa wengine wasio maarufu mazingira wanapotoka yawe safi na bora
 
Kwani ukifa unazikwa ndani ya nyumba?

Membe mnatafuta njia ya kumpa ujiko lakini ukweli umeonekana,yeye aende tu na hayo ma visasi yake.

Kwa ujumla ni kwamba Membe hatasimama tena!

Kama alivyowahi kusema yeye mwenyewe kuhusu magufuli kutosimama tena!

Na hili liwe fundisho kwa wapika sumu mlioko humu JF, mjifunze kuelewa.
Yule mungu wenu wa Chato mbona amezikwa ndani ya nyumba?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom