Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 735
- 1,464
Dale Carnegie aliwahi kusema kuwa *“If you want to Conquer Fear, Don’t Stay Home and Think About It, Go out and Get Busy* (Ukitaka kuishinda Hofu usikae nyumbani na kuendelea kuitafakari, toka na fanya kitu).
Kuna Hofu kubwa mbili zitakufuata kila siku unapoamka asubuhi:
1) Hofu ya kutokuwa na uhakika wa matokeo yajayo *(The Fear of Uncertainty).*
Hofu hii inawafanya watu washindwe kuchukua hatua kwa sababu hawana uhakika wa matokeo wa watakachokifanyaWanajiuliza-Nikiongea naye akikataa je, nikienda wasiponikubali, Vipi nisipopata matokeo ninayotarajia? Kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa matokeo mtu anajaa Hofu na anajikuta akiwa katika *“Freezing state”-* Hachukui hatua yoyote ile. Kumbuka UKIOGOPA KUFANYA kwa sababu hauna UHAKIKA utabakia ulivyo, AMUA Kufanya na uwe tayari kukabiliana na MATOKEO yatakayojitokeza.Mabaya mengi unayohofia kuwa yatatokea huwa mara nyingi hayatokei, USIHITIMISHE kabla HAUJAFANYA.
2) Hofu ya Mabadiliko *(Fear of Change)*
Hofu hii inatokana na mtu kutokuwa tayari kubadilisha kile alichokizoea. Watu wengi huwa wanaona hakuna maisha mengine nje ya walichonacho kwa sasa.
Wanaona wakipoteza kazi ya sasa kama watakufa, wakipoteza mtu fulani kama ndio mwisho wa dunia, wakibadilishwa cheo wanahisi kama pumzi itakata n.k wamejiaminisha kuwa hawawezi kufanikiwa nje ya WALIPO na WANACHOFANYA kwa sasa.
Sio kweli: Unaweza kufanikiwa tena hata kwa ZAIDI katika Kitu kingine tofauti na unachofanya sasa, usiogope KUBADILISHA.
Leo anza siku yako kwa kujivika UJASIRI na kufanya UAMUZI kuwa HAUTARUHUSU HOFU ikushinde. Kumbuka una uwezo Mkubwa ndani yako KUSHINDA Hofu inayokukabili, USISUBIRI hadi siku iende sana: ISHINDE HOFU MAPEMA LEO kwa KUCHUA HATUA bila KUCHELEWA. Nasubiria habari njema kutoka kwako.
Anza siku yako kwa FURAHA na KUJIAMINI, uishinde Hofu.
Nanauka