Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 766
- 1,536
Wiki yangu mpya imeanza na kusoma habari za Yusufu kwenye Biblia:Jinsi alivyokuwa na ndoto kubwa lakini baada ya kuwaambia ndugu zake walimchukia na kutaka hata kumuua.Jinsi ambavyo alijikuta akiwa mfayakazi wa ndani na mfungwa.Hata hivyo mwishoni alikuja kuwa mtu mkubwa sawasawa na ndoto yake.
.
Nimefurahishwa sana na pale aliposema -“Ninyi MLINIFANYIA yote haya mkitaka NISIFANIKIWE,kumbe katika hayahaya MUNGU alikuwa ananiandaa KUFIKA alipokuwa ameniandalia ili NIWASAIDIE na NINYI PIA”(Mwanza 50:20).
.
Kuna watu wengi sana tangu wameisikia ndoto yako kubwa wanatamani kuona HAUFIKII,wengine wanakufanyia HILA za chini kwa chini ili UISHIE NJIANI.Kuna wengine watakufanyia mizengwe ili UFUKUZWE KAZI au watakusemea MABAYA ili UPOTEZE sifa yako na uonekane hauna MAANA.
Kuna kitu hawakijui: Chochote wanachojaribu kufanya wakiamini WANAKUKOMOA kitatumika KUKUSAIDIA kusogea zaidi katika MAFANIKIO YAKO. Kwa kila baya watakalojaribu wiki hii amua kusema-“Mungu, naomba utumie na hili KWA FAIDA yangu”. WALIOKUSUDIA MABAYA wiki hii, watashangaa jinsi WALIYOPANGA YANAVYOKUINUA ZAIDI badala ya KUKUANGUSHA.
Kitakachitokea ni kuwa MBELE ya safari WATAKUJA Kukuomba MSAADA tena. Usiwachukie kwani WANAKUSAIDIA kutengeneza USHUHUDA MKUBWA.
#Nanauka