Ishi na watu vizuri, vinginevyo pigia polisi simu wakusaidie

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
479
1,253
Unapokuwa unaishi kwenye jamii ishi na watu vizuri na changanyikeni na wanazengo katika matukio mbalimbali kama misiba na ulinzi usijione kwamba wewe ni mtu anayeishi dunia nyingine.

Kuna jirani yangu kavamiwa na kuibiwa kila kitu licha ya kupiga mayowe na kelele kuomba msaada badala yake kila aliyekuwa anaamka alikuwa anamjibu, "Pigia polisi simu wakusaidie" wanarudi kulala.

Wanazengo walikuwa wanapigiana simu ili kujua kelele za wapi na nini, wakijua ni kwa fulani wanarudi ndani huku wakisema, "Mwambie apigie polisi simu wamsaidie".

Nashauri hata kama upo vizuri kiuchumi na huku ukiwa na geti kali ishi na watu vizuri kwa kuchangamana nao na kushirikiana nao fresh.

Ukitaka kujua kama watu wanakupenda au lah! Gombea nafasi ya umma au patwa na shida.
 
Unapokuwa unaishi kwenye jamii ishi na watu vizuri na changanyikeni na wanazengo katika matukio mbalimbali kama misiba na ulinzi usijione kwamba wewe ni mtu anayeishi dunia nyingine

Kuna jirani yangu kavamiwa na kuibiwa kila kitu licha ya kupiga mayowe na kelele kuomba msaada badala yake kila aliyekuwa anaamka alikuwa anamjibu"Pigia polisi simu wakusaidie" wanarudi kulala.

Wanazengo walikuwa wanapigiana simu ili kujua kelele za wapi na nini,wakijua ni kwa fulani wanarudi ndani huku wakisema"mwambie apigie polisi simu wamsaidie"

Hii ni chai...

Hata kama jamaa angekuwa mtu wa watu hao majirani wasingetoka coz hawajui hao wezi wamejipanga vipi kisilaha na wako wangapi!
 
siamini swala la kuishi na waswahili vizuri...mswahili ishi nae vyovyote ila ni mshenzi tu.
 
Jidanganye. Nguvu ya nzengo hata ungeenda kuvamia na kifaru lazima watafanya counter offensive. Ukweli ni kuwa jichanganyeni na majirani zenu.
Sisi huku hata uje na mabomu lakini raia wajue kabisa kwamba msela wao amevamiwa....utakiona.
 
Hii ni chai...

Hata kama jamaa angekuwa mtu wa watu hao majirani wasingetoka coz hawajui hao wezi wamejipanga vipi kisilaha na wako wangapi!
Siyo lazima wapambane nao hata kuongeza kelele na purukushani angalau majambazi watashtuka na kuanza kupotea, wewe ishi kama upo sayari nyingne siku ukivamiwa utajua wew utakavyopambana
 
Unapokuwa unaishi kwenye jamii ishi na watu vizuri na changanyikeni na wanazengo katika matukio mbalimbali kama misiba na ulinzi usijione kwamba wewe ni mtu anayeishi dunia nyingine

Kuna jirani yangu kavamiwa na kuibiwa kila kitu licha ya kupiga mayowe na kelele kuomba msaada badala yake kila aliyekuwa anaamka alikuwa anamjibu"Pigia polisi simu wakusaidie" wanarudi kulala.

Wanazengo walikuwa wanapigiana simu ili kujua kelele za wapi na nini,wakijua ni kwa fulani wanarudi ndani huku wakisema"mwambie apigie polisi simu wamsaidie"

Nashauri hata kama upo vizuri kiuchumi na huku ukiwa na geti kali ishi na watu vizuri kwa kuchangamana nao na kushirikiana nao fresh.

Ukitaka kujua kama watu wanakupenda au lah! Gombea nafasi ya umma au patwa na shida.

Mimi nikiwa ndani kwangu, hata nikipiga kelele hakuna wa kuja nisaidia, hakuna mtu atathubutu kuja, ngumu sana.
 
Unapokuwa unaishi kwenye jamii ishi na watu vizuri na changanyikeni na wanazengo katika matukio mbalimbali kama misiba na ulinzi usijione kwamba wewe ni mtu anayeishi dunia nyingine

Kuna jirani yangu kavamiwa na kuibiwa kila kitu licha ya kupiga mayowe na kelele kuomba msaada badala yake kila aliyekuwa anaamka alikuwa anamjibu"Pigia polisi simu wakusaidie" wanarudi kulala.

Wanazengo walikuwa wanapigiana simu ili kujua kelele za wapi na nini,wakijua ni kwa fulani wanarudi ndani huku wakisema"mwambie apigie polisi simu wamsaidie"

Nashauri hata kama upo vizuri kiuchumi na huku ukiwa na geti kali ishi na watu vizuri kwa kuchangamana nao na kushirikiana nao fresh.

Ukitaka kujua kama watu wanakupenda au lah! Gombea nafasi ya umma au patwa na shida.
Kamwe usiishi kufurahisha watu. Maisha ni mafupi, waswahili unaweza kuishi nao kinafki na bado wakakuzingua tu, hawakosagi sababu za kumchukia mtu.
 
siamini swala la kuishi na waswahili vizuri...mswahili ishi nae vyovyote ila ni mshenzi tu.
Mku dem boy,
Kuishi si lazima uende kukaa nao vijiweni, haswa kwa maisha ya dar es salaam.

Unaweza ukasikia kuna msiba ukaenda, kuna sherehe ukaenda au ukatuma mtu wa kukuwakilisha au asubuhi ukiwa unaondoka ukionana na majirani kama upo ndani ya gari unafungua kioo unawasabahi.

Yupo mbaba alisusiwa msiba na majirani zake, yeye hajawahi hata kutoka kutoa hata pole acha mbali na kushiriki. Ikabidi mwanamke ndo aanze kulia pale aombe majirani wamsaidie.

Kuna utofauti kati ya kuishi na watu na kukaa nao kupiga umbea😂.
 
Back
Top Bottom