Kitwango Mikazo Miguno
JF-Expert Member
- Apr 9, 2023
- 242
- 418
TRUE STORY.
Maisha hua yanatupa fundisho sana lakini hilo fundisho huwezi jua utalipata lini na wakati gani kwa muda gani.
Back then wakati niko chuo mkoa X kuna baridi kinyama sana huko sasa wakati ule nilikua playboy sana hivyo sikuwahi kuumia na mapenzi kabisa na niliwahi sema aah mapenzi kitu kidogo mno kwangu.
Baada ya miaka kwenda niliwahi kumpata dada mmoja hivi hapo ilikua kati ya (201_ - 202_) basi kiutani utani nikawa namfurahisha sana mpaka yeye mwenyewe akawa ananimiss pindi nosipomtafuta.
Hapo sikuwa serious naye bali ilikua kama jokes tu za hapa na pale ila kuna muda moyo unasema huyu namtaka sana maana alikua ni binti mzuri Mashallah yaani white sura nzuri na shape ilikua kwa mbali sana maana mimi hua sipendi mizigo mikubwa yaani portable ndo mambo yangu.
Wakati nakutana nae nilikua na demu mwingine ambaye sikuwa nampenda sana ni ile minjegeka tu ndo ilikua inanipelekesha kwasababu ya baridi. Basi siku zikapita nikasema acha nifanye kweli huyu binti awe wangu kumbuka wakati huo mimi niko mkoa X kwaajili ya mosomo yeye alikua kwenye jiji la kitapeli Daslama japo hata mimi kwetu ni Dar pia.
Fast forward Baada ya miezi kadhaa alikubali kua wangu peke yangu na mimi nikaamua kuachana na michepuko yote nifocus na huyo binti. Baada ya miaka ya furaha na amani mambo yalikuja kubadilika sana ikaanza miaka ya maumivu makali mpaka kupata vidonda vya tumbo.
Maisha yalibadilika kama vile (wana wa Israel walivyotoka Misri wakati wakiwa jangwani wakaanza kukumbuka walipotoa kua walikua wanakula vizuri bila wao kujua kua Mungu anakusudi ndani yao) ilifika mahali binti alibadilika sana baada tu ya kupata kazi.
Niliumia sana maana niliwekeza kila kitu changu kuanzia akili, mawazo mpaka nyegele zangu zote ila yeye akaanza vitimbwi mara leo hili mara kesho hili nikasema fresh tu. Miaka ikapita nikamaliza chuo nikarudi jijini sasa rasmi.
Nilifikiri labda umbali wetu ndo ulikua unapelekea ugomvi kumbe sio maana baada ya kurudi hali ilizidi kua mbaya nikakubaliana na yote. Siku moja tulikua na miadi sasa tukasema sababu yeye anakua kazini muda mwingi ngoja niongee nae anipe ratiba yake halafu tujue tunameet vipi.
Siku hiyo nilimpigia simu sana toka asubuhi mpaka usiku wa saa 6 yaani calls nyingi bila yeye kupokea wala kujibu meseji nilizokua nimemtumia ile iliniuma sana. Kama inaenda saa 7 hivi night nilipiga tena ghafla akapokea jamaa akasema "Oya mbona unapiga simu sana, tumelala bana".
Nilihisi kuchanganyikiwa mwili wote ukakosa nguvu nikaanza kumpigia simu dogo langu huku namtukana as if yeye alikua kitakachoendelea baada ya muda akili ikakaa sawa. Demu akaanza kunicheki na kuniomba msamaha kua aliepokea simu sio jamaa yake ila ni co-worker mwenzie and i was like WTF are you talking about.
Nilipata shida sana wakati ule maana akili yangu ilimuwaza yeye tu, hivyo nikaamua kumove on japo kwa maumivu makali sana ila sikua na namna zaidi ya kukubaliana tu na hali nikasema siji kumpenda mwanamke sana hata iweje yaani ni heri moyo wangu ukajaa kuhusu familia yangu ila demu au mke.
Mwisho: Usimuamini mwanamke yeyote yule maana mwishowe utakua kuumia sana na kujuta. Hakika majuto ni mjukuu baada ya miaka 5.