Miss Kim, najua nimekushambulia kwa suala la ID, niwie radhi lakini nilitaka nitoe dukuduku langu na kuonyesha kutofurahishwa na hilo suala.
Hili suala lako halina suluhu moja kwa kila tatizo, kuna watu wamefahamiana mitandaoni wakaishia kuumia na wengine mambo yameenda sawa.
Binadamu tuko tofauti na hatutabiriki, laiti tungekuwa na uwezo wa kujua mioyo ya tu, pasingetosha.
Kuna watu wamefahamiana kwa kuonana ana kwa ana, hali kadhalika wapo walioumia na wapo mambo yameenda vizuri.
Kuna unafuu kidogo kwenye kuonana ana kwa ana kwa sababu inakupa fursa ya kupunguza baadhi ya maswali ya muonekano halisi wa mtu unayeanza nae mahusiano.
Watu watakushauri mengi lakini mwisho wa siku wewe ndio utakaebeba matokeo yeyote ya hili suala yawe mabaya au mazuri. Fuata moyo wako.
Huwezi kujihakikishia uhalisia wa mtu kwa mtandao.