Habari za jumapili wanajamvi?? kwa upande wangu mie iko pouwa namshukuru muumba kwa hilo. kubwa nalowasilisha siku ya leo ni kuwa hapa mitaa ya home kuna jirani yangu mmoja ana mke na mtoto 1. Sasa imetokea tu kwamba huyo mke wa jamaa yangu kamzoea sana mke wangu kiasi ambacho hata kama anaenda dukani huwa anamuacha mwanae kwa mke wangu.
Hiyo sio ishu saaaana ila sasa amekuwa na tabia ya kuja kushinda kwangu saana hasa kupiga stori na my wife za hapa na pale na mie mara nyingi akija huwa nawaacha wao wawili. kinachoanzanikera sasa hivi anakuja na mwanae hana nepi wala chupi ya mkojo halafu anamuweka kwenye sofa zangu,basi naam zinakojolewa kama mie ndio nina kichanga kumbe sie hata kichanga hatuna. ukimwambia mbona mtoto havalishwi nepi utasikia "tumemuacha hivyo ili apumue ila tukiwa tunaenda kwa watu tunamvalisha." sasa hapo mie ndio huwa najiuliza kama sie ni ngedere au? mtoto mwenyewe anakuwa ni mchafu muda wote kiasi ambacho hata mtu kumshika waona tabu unabaki kucheza nae upo miles away!
Kali ya leo ni kuwa jana nimerudi kutoka safari ya kikazi na niliingia kama saa tano usiku so nilikuwa na uchovu wa hatari. nimelala hadi saa nne unusu hivi ila ile kuamka tu namsikia yupo sitting room kwangu na mke wangu kama kawa. sasa hadi muda huu yupo kwangu ni saa nane kasoro sasa mie nipo room sijatoka nae bado yupo tu hata dalili siioni ya kutoka.
Sasa najiuliza maswali kuwa leo ni jumapili na mumewe yupo home,je chai alimuandalia/wamekunywa saa ngapi?? shughuli zingine za ndani kamaliza saa ngapi?? nani anampa company mumewe huko ndani?? Je na maandalizi ya lunch yanaendaje? Is she a reponsible woman?? je wakiwa na watoto zaidi ya huyo mmoja atakuw aje?? she's really absurd.:confused2::confused2::confused2::confused2:
:confused2: