Is President Kagame behind General Imran Kombe's assasination?

Huyu kagame, ni balaa, kwani mauaji yote yaliyo tokea Rwanda chanzo chake ni yeye. Unajua waandishi tena wa nje na ndani ya TZ wakisha pewa hela huandika uongo, mfano huandika hivi:
Watusi wenye itikadi kali walio husika na mauaji ya watusi! Huu ni uongo wa waandishi wa habari, ukweli ni kwamba kagame ndiye aliye injinia mauaji hayo na mpaka sasa anaendelea kuua wahutu wachanga ili wasiwe askali
 
Kagame ali operate na ku accomplish hiyo mission bila serikali ya Tanzania kujua?

Polisi waliomuua Kombe walihukumiwa kunyongwa baada ya ukutwa na hatia ya kuua. Lakini wiki chache zilizopita kuna gazeti [I guess ni Mwananchi] liliripoti kwamba polisi hao walishasamehewa kwa msamaha wa Rais. Siku mbili baadaye Salva Rweyemamu alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Kikwete hajawasamehe hao wauaji.

Kombe aliuawa zama za utawala wa Mkapa, na ni Mkapa huyo huyo akiwa Rais aliwasamehe hao wafungwa. Je, ni kwanini Mkapa aliwasamehe hao wafungwa?

So, lazima serikali ilikuwa inajua kilichokuwa kikiendelea na hata hao polisi walioua, inawezekana waliua kwa amri kutoka juu na ni hao hao wa juu ndio walioamua kuwasamehe baada ya kusoma gerezani for some years.

Kagame ana mkono mrefu na siyo mkono mrefu tu, ameishi Tanzania na Uganda so anajua mengi sana na anafahamiana na watu wengi tu. Kwa hiyo akitaka kufanikisha chochote ni rahisi sana na wala sio lazima atumie mashushu wake wa ubalozini, mtaani anaweza kuwa ana informers wengi sana ambao ni watanzania.
 
.. Kagame ana mkono mrefu na siyo mkono mrefu tu, ameishi Tanzania na Uganda so anajua mengi sana na anafahamiana na watu wengi tu. Kwa hiyo akitaka kufanikisha chochote ni rahisi sana na wala sio lazima atumie mashushu wake wa ubalozini, mtaani anaweza kuwa ana informers wengi sana ambao ni watanzania.

AND

That being the Case???!!

I repeat ...!! I never Trust President Kagame and will never trust Him against the safety and sovereignty of my Country! I have never felt safe with ... HIM OR HIS COUNTRY AS A NEIGHBOR!!
 
Polisi waliomuua Kombe walihukumiwa kunyongwa baada ya ukutwa na hatia ya kuua. Lakini wiki chache zilizopita kuna gazeti [I guess ni Mwananchi] liliripoti kwamba polisi hao walishasamehewa kwa msamaha wa Rais. Siku mbili baadaye Salva Rweyemamu alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Kikwete hajawasamehe hao wauaji.

Kombe aliuawa zama za utawala wa Mkapa, na ni Mkapa huyo huyo akiwa Rais aliwasamehe hao wafungwa. Je, ni kwanini Mkapa aliwasamehe hao wafungwa?

So, lazima serikali ilikuwa inajua kilichokuwa kikiendelea na hata hao polisi walioua, inawezekana waliua kwa amri kutoka juu na ni hao hao wa juu ndio walioamua kuwasamehe baada ya kusoma gerezani for some years.

Kagame ana mkono mrefu na siyo mkono mrefu tu, ameishi Tanzania na Uganda so anajua mengi sana na anafahamiana na watu wengi tu. Kwa hiyo akitaka kufanikisha chochote ni rahisi sana na wala sio lazima atumie mashushu wake wa ubalozini, mtaani anaweza kuwa ana informers wengi sana ambao ni watanzania.
[h=1]JK AWAACHIA HURU POLISI WALIOMUUA JENERALI KOMBE[/h]

-WALIHUKUMIWA KUNYONGWA NA MAHAKAMA KUU, RUFAA
ASKARI Polisi wawili waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe wameachiwa huru.Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku, ambao wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais Jakaya Kikwete ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.

Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

Akizungumza na Mwananchi jana, Matiku alisema walitoka gerezani Mei mwaka huu walikokuwa wakisubiri kutekelezwa kwa adhabu yao ya kunyongwa, kabla ya Rais Kikwete kuwaonea huruma na kuwapunguzia adhabu.

"Unajua baada ya jaji kutuhukumu kunyongwa tulikata rufaa, Mahakama ya Rufani ambayo iliona ile hukumu ilikuwa ni sahihi ikasema tuendelee nayo hadi tulipoomba huruma ya Mheshimiwa Rais," alisema Matiku na kuongeza:

"Jopo lililomshauri Rais lilipendekeza tupunguziwe adhabu kutoka kunyongwa hadi kifungo cha miaka miwili na kwa kuwa tulikuwa mahabusu tangu 1998, kifungo hicho kilitosha."

Alipoulizwa wanachofanya sasa yeye na mwenzake Mswa, Matiku alisema anajishughulisha na shughuli za kilimo wakati mwenzake anajishughulisha na biashara.

Maisha gerezani
Konstebo Matiku aliliambia alisema katika miaka yote 16 aliyokuwa gerezani (1996 – 2011), aliishi katika magereza matatu tofauti, Karanga, Kilimanjaro; Maweni, Tanga na Ukonga, Dar es Salaam.

"Kwanza tulikaa Karanga kwa miaka miwili hadi tulipohukumiwa na Mahakama Kuu mwaka 1998, tukahamishiwa Gereza la Maweni kwenda kusubiri kunyongwa, lakini mwaka 1999 mimi nilianza kuumwa hivyo nikahamishiwa Ukonga ili niweze kupata matibabu," alisema Matiku.Alisema kuanzia wakati huo alitengana na mwenzake, Mswa hadi walipoachiwa kwa huruma ya Rais Mei mwaka huu.

Alisema katika kesi hiyo walikuwa washtakiwa sita wakiwamo askari polisi watano na raia mmoja. Alidai kwamba raia huyo aliyekuwa akiitwa Ismail Katembo alifariki dunia akiwa gerezani mwaka 1997, huku askari wengine wakiachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kutopatikana na hatia.

Matiku alisema katika kesi hiyo walikuwa wakitetewa na mawakili watatu tofauti na kwamba wakili wake anamkumbuka kwa jina moja tu la Sande... "Alikuwa akiitwa Sande, lakini kwa bahati mbaya mimi sina mawasiliano naye hadi sasa, wale wengine walioachiwa walikuwa wakitetewa na Profesa Msenga na huyu Mswa alikuwa akitetewa na wakili mmoja hivi ni profesa naye lakini jina lake limenitoka."

Matakwa ya Katiba
Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

Ibara hiyo inatamka "Bila kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote ikiwamo kuibadilisha adhabu yeyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote ili iwe adhabu tahafifu."

Kisheria, huruma hiyo ya Rais inatambulika kama 'Presidential Amnesty' wakati madaraka hayo ya Rais yakifahamika kama 'Prerogative Mercy' na hata Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kuitumia wakati wa utawala wake.

Madai ya familia
Baada ya polisi hao kupatikana na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kile Jaji Buxton Chipeta alichosema: "Uzembe wa hali ya juu", mjane wa Kombe, Roselyne Kombe alifungua kesi ya madai dhidi ya Serikali.

Mjane huyo na watoto wa marehemu, walifungua kesi Mahakama Kuu wakiidai Serikali fidia ya Sh690 milioni kwa msingi kuwa kifo cha Kombe kiliifanya miradi iliyoanzishwa na marehemu kupoteza mwelekeo na kufa.

Oktoba 4, 2001, Jaji Lawrence Mchome ambaye sasa amestaafu, aliiona Serikali kuwa inawajibika kuilipa familia hiyo fidia kutokana na vitendo vya watumishi wake hao wawili lakini ikaiamuru ilipe fidia ya Sh300 milioni.

Hata hivyo, Serikali haikuridhika na hukumu hiyo na ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo kimsingi nayo iliafiki Serikali kulipa fidia isipokuwa ilipunguza kiwango cha fidia hadi kufikia Sh200 milioni.

Adhabu ya kifo
Hatua ya Rais kuwapunguzia adhabu polisi hao imekuja katika kipindi ambacho wanaharakati wa haki za binadamu wakipaza sauti kutaka adhabu ya kifo ifutwe na badala yake iwe kifungo cha maisha.

Tangu Rais Kikwete aingie madarakani 2005, hajawahi kusaini hukumu yoyote ya kifo kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Benjamin Mkapa na hadi sasa zaidi ya watu 500 wanasubiri kunyongwa.

Kwa mujibu wa hotuba ya aliyekuwa msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Fatma Maghimbi (CUF), mwaka 2008, Mkapa alibadilisha hukumu za watu 100 waliohukumiwa kunyongwa na kupewa adhabu mbadala.

Maghimbi ambaye sasa ni mwanachama wa CCM, alisema Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ndiye pekee aliyesaini utekelezwaji wa hukumu ya kifo kwa watu 21 ambao walinyongwa mwaka 1994.

Adhabu ya kifo ni kati ya zile sheria 40 ambazo Tume ya Marekebisho ya Sheria chini ya, hayati Jaji Francis Nyalali ilipendekeza zifutwe, kwa kuwa haimsaidii aliyeua, aliyeuliwa wala Serikali kuzuia kosa kama hilo kutokea.

CHNAO MWANACHI

Kutoka adhabu ya kunyongwa hadi kifungo cha miaka 2 , mi nilijua kifungo cha maisha ndio mbadala wake?
 
ASKARI Polisi wawili waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe wameachiwa huru.

"Unajua baada ya jaji kutuhukumu kunyongwa tulikata rufaa, Mahakama ya Rufani ambayo
iliona ile hukumu ilikuwa ni sahihi ikasema tuendelee nayo hadi tulipoomba huruma ya Mheshimiwa Rais," alisema Matiku na kuongeza:

"Jopo lililomshauri Rais lilipendekeza tupunguziwe adhabu kutoka kunyongwa hadi kifungo cha miaka miwili na kwa kuwa tulikuwa mahabusu tangu 1998, kifungo hicho kilitosha."

Matakwa ya Katiba
Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote
aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

Ibara hiyo inatamka "Bila kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote ikiwamo kuibadilisha adhabu yeyote aliyopewa mtu yeyote
kwa kosa lolote ili iwe adhabu tahafifu."

1. Thread inaongelea uwezekano wa kuhusika kwa Rais Kagame kwenye mauaji ya Gen. Kombe
2. Taarifa za kuachiwa kwa wahusika wa maauji zinaonyesha wazi kuwa walipatwa na HATIA kwa hiyo ni kweli walikusudia kwa makusudi kufanya uhalifu kama taarifa inayvyoonyesha.
3. Uwezakano wa Kagame kuwa nyuma ya mauaji haya hafutwi kwa kuwa Rais wa Kikwete amewapa msamaha!
4. Kikwete katoa msamaha kwa sababu zake na Kagame anaweza kuwa na sababu zake amabazo pia Kikwete hazijui! Inagawa namshauri asome uzi huu na kufuatia jambo hili!
 
Kama Kagame alihusika kwenye mauaji ya Kombe basi alishirikiana na Serikali ya Tanzania kukamilisha hayo mauaji, manake polisi waliofyatua risasi ni wa Tanzania, na baada ya mauaji Serikali ya Tanzania ilikiri kwa kupitia Polisi kuwa walimfananisha na Jambazi sugu.. Hivyo kama ni lawama bado zinapaswa kuelekezwa kwa Serikali ya Tanzania hata kama ulikuwa mpango wa Kagame (kitu ambacho siamini, anyway)

Umeniwahi mkuu,hili ndiyo jibu nilitaka kumpa Jmushi.nadhani tuna mawazo yanayofanana katika hii inshu!
 
Sitetei mauaji ya aina hii lakini kama ni kweli yanatekelezwa na Kagame, basi jamaa wacha nimpe nishani ya "techinical sniper!" Yaani anakuwa na usongo na Former TISS Boss na bado anatumia polisi wetu kummaliza?! By the way, kama hivyo ndivyo; ni kwanini basi wauaji wa Kombe wameachiwa huru?! Ina maana wameachiwa kwa maslahi ya Rwanda au Kagame aliitumia serikali yetu kumuondoa mmbaya wa serikali yake?! Hapa, one of the two inaweza kuwa ndio jibu sahihi.....ama Kombe aliuawa na serikali ya Tanzania kwa "maslahi" ya Tanzania au aliuawa na Serikali ya Tanzania kwa maslahi ya Rwanda na kwa kuangalia tafsiri zote hizo bado utaona muuaji ni serikali ya Tanzania na si Kagame!
 
Hukunielewa

You mean kuhusu this?
NgumiJiwe said:
Kama Kagame kweli ameweza kumuua mtu mzito kama director wa TISS bila ya 'baraka' ya serikali ya Tanzania/bila ya serikali ya Tanzania kujua,aise tutakuwa na tatizo kubwa sana kiusalama kama nchi na vyombo vyetu vya usalama,kitu ambacho sitaki kukiamini
 
kagame anajua anachokifanya, usidhani TISS haina watu wenye akili, tatizo ni namna inavyowa-utilise, afisa wa usalama haendi na wakati, nchi hii inavichwa sema kubweteka kwa taasisi kutokana na kufanya kazi kwa mazoea:A S embarassed:
 
Nasikia hata vifo vya kina Sokoine, Kolimba na Nyerere, Kagame alihusika sana, huyu mtu ni hatari sana inabidi serikali imwangalie kwa karibu na ikibidi kufanya mipango ya kumwondoa pale, kale kanchi kadogo sana tukiamua kukachukua ni siku moja tuu.
UTANI wako ni mzuri sana KOBA, kama hatutaki aibu tusije dhubutu kumchokoza Kagame, atatuzaire mara moja, mnajua aliyeamua Mobutu Sese seko Ngbendu Wazabanga atimuliwe madarakani? ni Kagame, sisime mengi, lakini ukimgusa Kagame basi ujue umetangaza vita na Uganda, Ethiopia, Israel, Marekani, Uk, na nchi zote zilizoko katika mrengo wa kulia zaidi duniani, na udogo wa nchi yake si neno, Kwani Israel ikiwa na Raia milioni moja si ilipigana vita ya siku sita na mataifa 20 ya kiarabu na baada ya siku hizo Israel ilitanua boda zake na kupata eneo mara nne la nchi hapa awali kabla haijashambulia kwa kuvizia na hao waarabu kwa siri.
 
It is so easy to join the dots. Mkapa hates the opposition with a passion. That is one dot. Kombe was killed under Mkapa's Presidency,
that is another dot. It is said Kombe was going to join the opposition. Now, that is another dot.

That was very stupid of him. He was intelligent enough to realise that he would never get away with it. No wonder it costed his life.
 
Kweli tupu
Huyu kagame, ni balaa, kwani mauaji yote yaliyo tokea Rwanda chanzo chake ni yeye. Unajua waandishi tena wa nje na ndani ya TZ wakisha pewa hela huandika uongo, mfano huandika hivi:
Watusi wenye itikadi kali walio husika na mauaji ya watusi! Huu ni uongo wa waandishi wa habari, ukweli ni kwamba kagame ndiye aliye injinia mauaji hayo na mpaka sasa anaendelea kuua wahutu wachanga ili wasiwe askali
 
UTANI wako ni mzuri sana KOBA, kama hatutaki aibu tusije dhubutu kumchokoza Kagame, atatuzaire mara moja, mnajua aliyeamua Mobutu Sese seko Ngbendu Wazabanga atimuliwe madarakani? ni Kagame, sisime mengi, lakini ukimgusa Kagame basi ujue umetangaza vita na Uganda, Ethiopia, Israel, Marekani, Uk, na nchi zote zilizoko katika mrengo wa kulia zaidi duniani, na udogo wa nchi yake si neno, Kwani Israel ikiwa na Raia milioni moja si ilipigana vita ya siku sita na mataifa 20 ya kiarabu na baada ya siku hizo Israel ilitanua boda zake na kupata eneo mara nne la nchi hapa awali kabla haijashambulia kwa kuvizia na hao waarabu kwa siri.

watusi mnapenda kujifanya waisraeli? kweli bwana mna akili nyingi nyie sio wanadamu wa kwaida! hahahahahahahaha kazi tuanayo watu weusi!
 
  • Thanks
Reactions: UTC
Back
Top Bottom