Is Lowassa again?

Nilizungumzia nyumba aliyokuwa anakaa Prof.Shaba na sio kilichokuwa kimeelezwa na thisday.

Hii issue imeingia hata kwenye cabinet kwani kuna me,mbers wa cabinet hawakubaliani nayo ila kwa nguvu za huyu mkoloni bado sijajua nini kinaendelea ndani kwa ndani hadi sasa ukizingatia ndio nimerudi jijini jana usiku.

Huyu mkoloni si ajabu anataka kumsogeza rais yule wa kwao karibu na ikulu yetu, kaeni macho .
 
Huyu mkoloni si ajabu anataka kumsogeza rais yule wa kwao karibu na ikulu yetu, kaeni macho .

Now you are talking...

mimi nimewaonya watu kuwa careful na huyu mwizi, mkwepa kodi, na mkoloni Rostam Azizi for a while now! ukifuatilia pesa zake na biashara zake, utaamini kabisa kuwa this guy ana ajenda.... bado ninafanya uchunguzi ila sitashangaa kufikia hiyo conclusion yako
 
Prime govt property sale saga takes new turn as: Private buyer now told to pay more

-From 440m/- to 1.85bn/-, in one cool twist




Source: ThisDay

Naona mafisadi wameanza kushituka baada ya moto wa akina Dr. Slaa. Huu moto ukiendelea na magazeti yakiendelea kupiga kelele, taratibu mambo yanaweza kubadilika maana hawa watu walikuwa wamezowea kujifanyia mambo yao kama wanavyopenda.
 
Ningekuwa mimi Hilal ningekataa.. "mkataba ushasainiwa, unless wako tayari kupitia mikataba yote ya real estate".. Kuiweka hiyo bei katika perspective... mchango wa mgodi wa Buzwagi kwa makato mbalimbali (ukiondoa kodi ya mrabaha) ni kama Shilingi milioni 600 hivi.. (nusu bilioni).. lakini kiwanja kimoja kinataka kuuzwa kwa bilioni mona na ushee ..
 
Naona mafisadi wameanza kushituka baada ya moto wa akina Dr. Slaa. Huu moto ukiendelea na magazeti yakiendelea kupiga kelele, taratibu mambo yanaweza kubadilika maana hawa watu walikuwa wamezowea kujifanyia mambo yao kama wanavyopenda.

Haiwezekani kilicho chetu kiwe chao na chao kiwe chao tu, wapi na wapi?



Good points Mwanakijiji huwezi leo hii ukauza plot kwa billions na kusema mgodi ni chini ya billion hawa jamaa lazima washughulikiwe tena kisawasawa.
 
Vizuri wamepandisha bei ila bado mchakato mzima katika uuzaji wa kiwanja hicho inabidi uangaliwe, je ulikiuka taratibu zilizopo kama tuhuma zinavyodai?
 
Jamani Lowassa tena yumo humu?

 
This is Lowassa Bwana, what goes around comes around.

Nchi hii itauzwa na kumaliziwa kwa kipindi hiki cha miaka mitano ya JK na mwenzake Lowassa , sasa hapa watu wanasema JK anapotoshwa ,asimamie walau hili ili kuweza kunusuru ardhi yetu basi .

Kibaya zaidi ni kuwa jamaa anauziwa kwa bei ya kununua kiwanja goba , ama nyingine zimeingia kwenye account ya mzee Lowassa .

Hapa kesho usishangae unamsikia Nguba mwandishi wa Lowassa anajitokeza na kusema kuwa hata JK alikuwemo kwenye dili kama alivyosema wakati wa Buzwagi na kulala Churchil Hotel.
 
deals mbove alizozisimamia Lowassa; na ambazo zimeigharimu nchi hii pesa nyingi: (hizi ni zile zinazojulikana tu hadi sasa)

Aliinfluence tenda ya Richmonduli

Kukabidhi DAWASA kuendeshwa na kampununi ya kigeni na hatimaye tukajitoa ktk mkataba huo - at agreat cost i beileve.

Haya na sasa hata kuuza viwanja vya nchi - yumo !!

Damn! Do we really need such a person as our leader!! Kazi yake madili ya kula kula tuu. sasa nimeanza kuelewa maana halisi ya nguvu na kasi mpya!!
 
Jamani Lowassa tena yumo humu?

Mie nashangaa! sioni tatizo hapa, jee tatizo ni nini? ni Hemed kumuona Lowasa? au Lowasa kuwaandikia psrc? na nnadhani Lowasa ameweka wazi kabisa kuwa sheria zifuatwe. Bado nnashangaa tatizo ni nini?

Sidhani kwa wale wanaosema kuwa awamu hii itaimaliza nchi walikuwepo wakati awamu ya kwanza inang'atuka, kwa kuwakumbusha tuu, hakuna awamu iliiwaacha nchi hii kavu na kwenye umaskini mkubwa kama awamu ya kwanza, awamu ya msifiwa nyerere.

NYERERE alivyong'atuka, benki kuu iliwashwa moto na kaikubakishwa hata dola moja ya kufutia machozi, Jee mnakumbuka? NYERERE alivyong'atuka,tulikuwa hata mafuta ya kwenye gari hatuna kwa kuwa tulikuwa hatuna fedha za nje za kununulia, kumbuka mzee ruksa alivyochukuwa nchi aliwaita wazee wa dar pale diamond akawaelezea kuhusu hili na ikambidi atumie mbinu za haraka za kwenda kuomba libya na imf na iran na kwingineko (hotuba ya mikuki miwili, mzee ruksa diamond.

Yaani hatukumbuki tulivyokuwa tunapangishwa foleni za unga, mchele, sukari, sabuni,viwembe, viberiti. KWA KIFUPI HATA WEMBE WA KUNYOLEA ilIkuwa hakuna BILA FOLENI

Nadhani wengi mnaoandika humu kusemasema hovyo, kama hii mada ya Lowasa, hata sijui tatizo nini? Nadhani wakati wa nyerere mlikuwa hampo au kwa waliokuwepo na wanachangia habari hizi zisizo na mantiki, basi ni wafupi wa kumbukumbu.

Sasa jamani mbona yeye (nyerere) hatumsemi alivyotuwacha pabaya kiuchumi! tunamsifu tuu?

Hebu waacheni hawa kina lowasa na kikwete wafanye vitu vyao, JEE, kwa ukweli wenu kabisa hamuoni kazi wanayoifanya? au ni chuki tuu za kibinafsi?
 
Sasa Wewe Zomba unapotaka kuturudisha nyuma unataka tujifunze nini?usitete upumbavu huo..watu tuna asila hapa
 
sioni tatizo hapo kwa EL,amesema waziwazi msaidieni katika sheria zilizopo....tuache majungu wakati mwingine.
 
?

Hongera sana,,, umepatia kila kitu wala ila umesahau tu kusema, "Nyerere aliwaonea wivu Boys 2 Men akwapiga stop akiwa na maana kwamba JK wakati ulikua bado na kwamba baadaye (yaani sasa) anaweza kuongoza nchi, lakini aliposema EL hafai kabisa, alikua akimuonea wivu" Nimeona tu nikusaidie na hapa unajaribu kuanzisha mjadala wa Nyerere, ili kuhalalisha anayoyafanya EL... kwamba kinachomsumbua sasa ni CHUKI NA WIVU wa wafuasi wa Mwalimu Nyerere.. ambao wakipungua basi EL atafanikiwa kuchukua nchi baada ya JK (sina hakika 2010 ama 2015).... Kweli sisi wengine tunamuogopa Mwalimu, bora umemtolea uvivu... Tuambie kila kitu SEMA USIOGOPE.... Sema pia kwamba kwa kuwa Mwalimu aliacha nchi pabaya, akaja Mwinyi ikawa nafuu kidogo, akaja Mkapa akainua uchumi lakini akainua na rushwa, na alipoondoka Mkapa sasa ni ruksa kwa yeyote kufanya lolote na tena bila hata kusemwa maana "AKINA NYERERE" walitusababishia maisha magumu... Hongera sana kaka na huo ni mwanzo mzuri wa KUMSAFISHA EL kutokana na ZIMWI LA MWALIMU NYERERE ALIYEMKATAA HADI DAKIKA YA MWISHO.... USIJALI UTAFANIKIWA MAANA SISI WATANZANIA NI WEPESI WA KUSAHAU. KARIBU SANA KAKA
 
Hivi huyo mtu alisikia PM ndie anahusika na kuuza viwanja? Kwa nini alikwenda kumuona PM kama sio kutafuta favour?
Kwa nini Pm alientertain kumuona na kudirect barua iandikwe, tena na katibu wake kwenda PSRC?

Angekwenda mswahili wa hapa hapa angerudishiwa reception kwamba ofisi ya PM haihusiki na viwnja hivyo.
Majungu hakuna alienayo .. huyo mtu wala hata hatumjui tuwe na majungu ya nini!
 
sioni tatizo hapo kwa EL,amesema waziwazi msaidieni katika sheria zilizopo....tuache majungu wakati mwingine.

Umepatia kabisa, "kwa sheria zilizopo" ambazo Meghji na Ngasongwa walikua hawazijui, PSRC walikua hawazijui, sheria zilizopo ambazo "Boss is always right" sheria zilizopo kuuza kiwanja kilichopo kati kati ya jiji kinachokadiriwa kihalali kuwa na thamani ya sh bilioni 2 (Bei ya mtaani hadi 4bn/-) kwa milioni 400.

Umepatia kabisa kaka, kama sheria zipo Kiwanja kilichokua kinamilikiwa na Msajili wa HAzina, kikapelekwa PSRC kinayouza mashirika ya umma, tena bila kutangaza zabuni... Sheria zilizopo baada ya kikao cha watu wawili pale MAGOGONI ama Sijui Oysterbay ama sijui huko LOndon???? Sheria zilizopo kuuza kiwanja ambacho kiko karibu na jengo la ubalozi wa Uingereza (na balozi nyingine za Ulaya) barabara moja na Majengo ya BOT, jirani kabisa na Wizara ya Afya, jirani kabisa na majengo ya Bima na mita chache kutoka ufukwe wa bahari ya HINDI kwa bei ya chee tena bila zabuni... Sheria zilizopo kuidharau sheria ya manunuzi.... heeee jamani, UMETUSAIDIA SANA kukumbuka kwamba alisema sheria zilizopo, tena bila kupiga simu kuwaambia "namleta mtu wangu hapo msikilize" heeeeee... yaani ukitaka kusaidiwa na mkuu wa polisi, unapewa karatasi iliyoandikwa "msikilize huyu Halisi kama taratibu na sheria zinaruhusu" hapo OCD akiona hata haangalii vitabu vya sheria, anaagiza, "hebu mtoeni huyo ndugu yake Halisi... asaini mahali kwamba atamleta hapa kesho saa mbili asubuhi" halafu nakwambia, "nyie nendeni wala kesho musije kama ikitokea jambo nitakupigia simu" hiyo ndio Bongoland sasa ndugu yangu tukumbushane hayo unayoyajua zaidi.. na pia mtu mwenyewe picha yake imeharibika hana tena hadhi kwa umma, kwa hiyo haaminiki, lakini tusaidie kutukumbusha na kutuelimisha alivyo SAFI
 
sioni tatizo hapo kwa EL,amesema waziwazi msaidieni katika sheria zilizopo....tuache majungu wakati mwingine.

Sasa kama sheria zipo huko kusaidia kunatoka wapi, kwa nini asiseme sheria zifuatwe?


Pole ndugu yangu, unatetea yasiyoteeka na kuhalalisha yasiyohalalishika, mna kazi kubwa!
 
Mie nashangaa! sioni tatizo hapa, jee tatizo ni nini? ni Hemed kumuona Lowasa? au Lowasa kuwaandikia psrc? na nnadhani Lowasa ameweka wazi kabisa kuwa sheria zifuatwe. Bado nnashangaa tatizo ni nini?


Kama huoni tatizo then you must be blind.

Mara ya kwanza walishindwa nini kununua? What changed when the PM wrote to PSRC? Huoni kuwa PM alishinikiza kwa namna moja au nyingine? Kama PM alitaka awa fair basi alitakiwa amwambie huyo afuate taratibu zilizopo bila ya yeye kuwaandikia PSCR. Kwa yeye kuwaandikia PSCR inaleta picha ya kuingilia process nzima.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…