Is kikwete a genius? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is kikwete a genius?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwame Nkrumah, Apr 27, 2012.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Huwa ninajiuliza kila siku , kama Kikwete amepewa ripoti ya CAG iliyo chafu namna ile, madudu yanayoendelea kila kona ya nchi hii, kashfa za bandari , ATC, mawaziri wezi, rushwa, halmashauri zilizojaa mafisadi na yeye anayajua yote haya na hafanyi chochote, ni kwa nini?
  Lengo lake kuu ni kutuamsha Watanzania, sisi bado tumelala. Sisi ndiyo hatumujaelewa. Anatumia udaktari wake kutupa somo ambalo tumeshindwa kuelewa, kuna msemo " there is a method in my madness". May be this is what Dr. Kikwete is trying to teach us. Kutuamsha kwenye usingizi mzito tuliolala.
  Utafafanuaje picha ya kubembea Jamaica, kutembelea ufugaji wa kuku Brazil na kutetea watu kama akina Ngeleja?
  Rais wetu mpendwa JK anataka kutufundisha Watanzania kudai haki. Baadhi yetu tumeanza kuelewa.
  There is no other explanation on what is going on in this country.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Hata Elijah Muhammad alipokuwa anavipiga mimba kwa mfululizo vi katibu muhtasi vya "Nation of Islam" kuna watu walisema anatimiza unabii.

  Ukitaka kumu excuse mtu hata akisimama kwenye mimbari mkutanoni Jangwani na kuwakojolea wananchi utamwita jini wa utambuzi anayeona zaidi yetu mithili ya majini ya hadithi za "Alfu Lela U Lela".

  Kikwete muoga tu, anaogopa kivuli chake mwenyewe. Na huo kamwe hauwezi kuwa u "genius".
   
 3. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  An arse
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika Mkuu binafsi uwa naona tumelala sana yani,woga wa viongozi na sie wanachi dhidi ya watawala na issue nzima ya kitu kinaitwa Serikali.Yani kuna aina fulani ya kizazi wao Seriakli na watendaji wake ni MIungu watu!!Hawapaswi kuulizwa wala kuhojiwa chochote,ukionekana unaohoji au uanfanya udadisi kuhusu jambo linaloendelea Serikalini au mradi wowote wa Serikali kwa niaba ya wanachi,wahusika wanajua kuwa ni haki yako kujua lakini watakuijia juu na kukupa vitisho mpaka utafyata na kuwaambukiza wengine wenye uthubutu huo,matokeo Taifa zima linageuka kuwa Taifa la watu wenye hofu ya kutokuhoji Maswala ya Msingi juu ya Taifa lao.


  Kilikuwa kitu kizuri kwa watawala wa miaka hiyo au zama hizo za kina Mzee Mkapa na siasa za wivu wa kike,lakini kwa kizazi hiki cha sasa kuendeleza mfumo huo ni kuunda Taifa la watu kunguru/waoga wasio jua kutetea Taifa lao kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa Taifa na pia ni hatari kwa hao watawala waliokuwa wakifikilia kuwagandamiza umma kwa kuwatisha umma kuhoji/dadisi/dadavua/ibua/fichua/lalamika/hoji/tuhumu na hata kushitaki pale inapobidi.

  Wakati mwingine yaweza kuwa kweli uenda tumeitajika kujifunza kupitia the hard way.Haya mambo yaliyojili kwenye utawala wa Kikwete umewafungua macho watanzania wengi sana,moja ya kitu ambacho uwa nasema na madudu yote haya lakini uhuru wa Watanzania kujieleza hakika kwa hilo Jakaya Mrisho Kikwete anastahiki heshima.Ilikuwa ni juzi tu hapa utawala wa Mzee Mkapa uhuru huu tulionao ulikuwa ni adimu sana.Ukweli leo Mtanzania yuko wazi kujieleza na kusema pasipo vyombo vya dola kupenyeza nguvu ya kumzuia na kumuadhibu,japo bado kwa wanasiasa na baadhi ya watu wanakumbana na baadhi ya mikono ya baadhi ya vyombo vya dola kama Polisi na vyombo vingine.
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hakuna kosa kubwa wanalofanya watanzania ukiwemo wewe ndugu uliyeanzisha thread hii kama kufikiri kwamba ukishapiga kura kitendo cha sekunde mbili basi wajibu wako umekwisha unakwenda nyumbani kulala na kusubiri maendeleo yaje bahati mbaya sana hiyo siyo reality ya uongozi. viongozi wengi duniani wanafanya mambo magumu kutegemea na jamii iliyowazunguka. ukiwa na jamii ya waliomka na wasio taka mchezo they are going to hold you accountable for your actions or inaction. watahakikisha wanatia pressure na kukumbusha madai yao usiku na mchana na mpaka kiongozi anaamua kuchukua hatua. bahati mbaya watanzania tumeangukia ktk kundi la watu wale wa kwanza wa kupiga kura na kwenda kulala nyumbani kusubiri kiongozi atekeleze ahadi hawezi kutekeleza kwa kuwa hakuna mtu au kikundi cha watu kinachompa pressure ya kumfanya achukue hatua. chadema walijalribu kwy katiba wakafanikiwa. jk ni aina ya kiongozi anayefanya kitu kwa pressure tu na hakuna kingine kwani tumemuona mara nyingi aki act under pressure. amini usiamini tukiandamana siyo kwa wiki bali siku mbili mfululizo mawaziri wote utaona wanatimuliwa kwa sababu jk hana hoja ya msingi ya kwenda mbele ya wananchi na kuwatetea watu hawa. kwahiyo wito wangu kwa wananchi wenzangu wewe kama mtanzania wajibu wako usiishie kwenye kupiga kura tu bali kibarua kingine kizito kinakuja cha ku hold mtu/kiongozi accountable kwa yale aliyoyahaidi na siyo kwenda kulala nyumbani kutegemea vitu vitakuja tu vyenyewe.
   
 6. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280


  Kwa hiyo unataka kutumbia kuwa Dr. Kikwete anataka tumpindue? Kwa sababu haiwezekani wewe kama raisi unatawala nchi huku uozo umejaa kila sekta na idara wewe raisi unachekelea kuonyesha umeridhika na kuona wananchi wako ni wajinga mjanja ni wewe tu. Huyu yanki kwa kweli yuko useless as a leader na inabidi apinduliwe tu that's the only choice!.
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  He he hee , sijawahi sikia hiyo ya Elijah Muhammad
  Unakumbuka Gorbachev and Perestroika? Kiwete is trying to create one here, a major social, economical and political changes the likes of which has never been seen....Anataka tu mapinduzi hayo yatokee chini, siyo juu.
   
 8. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Sawa utafafanuaje yanayoendelea nchini?
   
 9. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha u-genius hapa na mimi na emphasize thread ya "Saint Ivuga" jamaa ni chanzo cha matatizo yetu ni mjinga, muoga, si muelevu, mpumbavu, Kanichi na mengineo mengi, halafu tumempa almost absolute powers through our history ya azimio la arusha eti tukitegema loyalty na heshima za kuombana kwa mapendekezo.

  Pakistani wamesha muhukumu kiongozi wao kwa kuzuia upelelezi, though his punishment looks like a slap on the wrist. But we know the intention is to open up the wider investigation, sasa sijui uzembe unaotendeka unazuilika vipi under Kikwete na power zake considering ni mpumbavu.
   
 10. M

  Mzee Kipara Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Mtajitahidi kutafuata sana namna ya kumpamba kikwete lakini ukweli utabaki palepale, the man is dumb, period. Kwa taarifa hata hiyo ya kujiita Dr kwa PhD ya heshima ipo Tanzania tu.
   
 11. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeamini uzee dawa.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kumbuka ni huyohuyo Kikwete aliyeanzisha CAG. Na huyo huyo Kikwete anawaona wajinga mnaposhindwa kuzitumia sheria mlizotunga wenyewe. Alishasema, yupo hapo kuijenga demokrasia na utawala wa kisheria si kuibomoa demokrasia na si kutawala kidikteta.

  Mmezowea kutawaliwa kama manamba kwa kusukumwa kila kitu na kungoja Rais atowe tamko, mnashindwa kujiendesha wenyewe, inabidi mbadilike muanze kutumia mifumo ya kidemokrasia iliyowekwa, sijaona mmoja wenu akienda kumshtaki mtu anemuona anaiba na anao ushahidi wa kutosha.

  Mna macho lakini hayaoni, mna masikio lakini hayasikii, mna midomo lakini mabubu.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe usie dumb mbona huna ulichokifanya? zaidi unalalamika kama mtoto mwenye njaa.

  Kikwete anaondokana kwenye udikteta mliouzowea na mnashindwa kumuelewa kwa kuwa mu watumwa ndani ya damu zenu. Hamuendi mpaka mswagwe!
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia tu juu juu, mtu anaweza asikuelewe but deep down you have a point mkuu!
   
 15. v

  vicmal New Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa madaraka tuliyo mpa huyu jamaa ts olmost Kama dictecta. Anawajibika kutoa tamko siyo sababu 'tumezoea kutawaliwa' Bali kwakua yupo hapo kwa kutuomba kura Na kutuhakikishia kwamba ata 'discharge the duties of the office of the president to the best of his abilities' lakini kumbe kuna utata hapo kwenye 'his abilities' Kama atashindwa kuwawajibisha walio chini Yake kwa mujibu wa sheria itabidi njia mbadala zitafutwe kumuwajibisha yeye.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  He is not a "genius" bali ni mwizi anaewatumia mawaziri wake kuiibia nchi yake period!!
   
 17. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280

  Ni kweli uliyoyasema, tatizo bongo utapanga mikakati na wenzako ili mfanye cha maana kwa manufaa ya umma mfano maandamano...utashangaa siku ya siku polisi wanakuja kukushika kuwa wewe ni mkorofi au wazee (Kikwete huyo huyo) akakutumia watu wakumwagie tindi kali kisha anajifanya kuja Muhimbili kukupa pole ili akupoteze malengo. Si kama bongo watu hawataki mapinduzi tatizo ni kama wanavyosema wenzetu humu ndani 'uwoga.'' Na mtu kukuuza kwa pilato hapa bongo si jambo la kushangaza, sasa utafanyaje? Mnapanga wote kisha anakugeuka ili akucheke eti unajifanya mjuaji. Kweli tunataka mapinduzi na utawala wa huyu kijana ni mbovu mno. Kama kweli mambo yakiwa mabaya itatulazimu kuwa recruit wahindi/waarab waje kujitoa muhanga kwa niaba yetu. Kikwete has to go, period!
   
 18. n

  nyantella JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hapo kwa red, jana kuna marine officer wa jeshi la marekani kamtukana Obama kwamba ni muoga, akafukuzwa kazi mara moja na kupoteza haki zake zote. humu ndani JK anatukanwa kila kukicha, tuseme Z ni more democratic country kuliko USA?
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unapanga maandamano wakati njia za kisheria zipo na hujazitumia? hata mimi nikiwa FFU ntakulamba virungu.
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  JK ana macho ila yamefungwa asione (yana uwezo wa kuona warembo tu), ana masikio lakini hayasikii, (uwezo wake ni wakusikia sauti nyororo za mziki na za warembo tu)
   
Loading...