Is It Possible, Mgombea wa CCM kwa 2015 ni Nchimbi?!. Yule "Jamaa Yangu" ni "Yohana Mbatizaji Tu?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi,

Kwa wale wafuatiliaji wa siasa za nchi hii, na haswa harakati za kumpata mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, CCM, kumekuwa kukitokea mambo mengi ya kufurahisha, kustaajabisha na hata kushangaza, kwa karibu kila mtu kutajwa kuwa anawezekana kuwa ndiye mgombea wa CCM wa 2015, hali iliyopelekea kwa baadhi ya wana CCM kujitokeza na kutangaza nia zao za kugombea, kunakopelekea tuhuma kuwa Prof,. Dr., JK, ameifanya taasisi ya urais kuwa "very cheap!", na kushuka thamani sana, kwa karibu kila mtu sasa kujiona anaweza kuwa rais!, yaani kama JK ameweza kuwa rais, then every Tom, Dick and Harry, can be a president!.

Ni muda mrefu mimi nimekuwa nikimsupport mgombea fulani, ambaye namtambulisha kwa jina la "jamaa yangu", japo jamaa huyu hajawahi kutamka popote kuwa ana mpago wa kugombea urais!, kwenye sherehe ya mwaka mpya, alitangaza kuianza "safari ya matumaini", watu wakatafsiri ndio safari ya urais, hivyo wakaanza, kuogopa, kuweweseka, kutetemeka, kubabaika, na kutishika hadi kumshauri Pinda kuingiza karata yako, ili kuutumia ugombea wa Pinda, kama upanga wenye makali kuwili, kwanza kuanza kwa kumchinjia "jamaa yangu" katika hatua za awali, kisha kuja kumchinjia Pinda mwenye kwenye Mkutano Mkuu wa CCM!.

Tangu "jamaa yangu" huyu aanze kutajwa tajwa kuwania urais, niliwahi kuwaeleza humu, kuwa kuna uwezekano mkubwa, "jamaa yangu" siye mgombea halisi, bali anazifanya harakati hizi kama "Yohana Mbatizaji" kuyanyoosha tuu mapito ya yule, "yuajaye!" ambaye ndiye "the chosen one!".

Lengo la hitaji la uwepo "Yohana Mbatizaji", kuyanyoosha mapito ya mpakwa mafuta, ni kufuatia njia ya 2015, kuzongwa na wanyama wakali, msitu mnene wenye miiba, milima na mabonde, bila kuwepo mtu imara wa kuyanyoosha mapito, mpakwa mafuta, anaweza asifike mwisho wa safari.

Leo, nimekutana na mwana CCM fulani, sio kiongozi bali ni insider!, ndie akanipenyezea tetesi hii, kuwa "the chosen one" ni Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi!.

Could this be possible?!.

NB. Wale wapenzi wa yule "jamaa yangu", mistake kunirukia na kunirarua kwa kutishia uhai wa tumaini lenu, kwa sababu, aliyenipa jina la Nchimbi, sio mimi!, mimi ni mjumbe tuu, na mjumbe huwa hauwawi!, na vile hizi ni tetesi tuu, it's up to you kuziamini au kuzipuuzia! Kikawaida tetesi ni tetesi tuu, sio kitu cha kukiaminia sana!, ila nimeileta tetesi hii ili ikija kutokea kuwa kweli, then wewe mwana jf, just be the first to know!, "information is power!", having such info, you'll have everything to gain, and nothing to loose!.. Ikitokea ikawa ni uongo, then you have nothing to gain and nothing loose!.

Kwa wale wanaodhani Jina la Dr. Emanuel Nchimbi, ndio limechipuka kwa mara ya kwanza leo,

Karibuni mtembelee hapa.

[h=3]Kwanini John Nchimbi hatajwi kati ya watu walioanza mbio ...[/h]
Wanabodi,

Nimetafakari kidogo bila majibu kwa nini Serikali, baadhi ya Usalama wa Taifa na baadhi ya Wakuu ndani ya CCM wanakuwa wanafiki kiasi hiki juu ya wagombea watarajiwa ambao tayari wamepanga timu zao za maandalizi.

Kwa walio karibu na "corridor of power" hakuna asiyejua state inavyomuandaa John Emmanuel Nchimbi kama mteule mpya wa Mkuu wa Kaya kumrithi pale Magogoni. Mipango yake na harakati zote zinaratibiwa na State. Lowassa anajua, Pinda anajua, Membe anajua na wengine tumepata kujua. Sasa kwa nini kila kukicha wapambe wameng'ang'ana na Lowassa tu kama vile wengine hawafanyi?

Binafsi simaini kama kuna mtu anatarajia kufanikisha jambo lolote maishani bila maandalizi, mikakati na jitihada. Hawa wanaowaandaliawengine ufalme kwa nini hawataki kuona wala kusikia wengine wenye Uwezo wa kujiandalia wakifanya hivyo? Miujiza huonekana kama vitu vitokeavyo bila kutarajiwa lakini nayo ili mtu imtokee lazima afanye maandalizi i.e kutubu, kujitakasa, na kusali kwa imani. Kwa nini hawa "wenye mteule wao mfukoni" hawataki kusikia wenye uwezo wakijiandaa?

Kuanzia sasa nami natangaza kujiunga na timu Lowassa ili nikajue kwa nini anahofiwa kuliko wengine wote.
Wengine niliowaletea ni hawa
  1. Elections 2015 - Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa... Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
  2. Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 ameshapatikana
  3. Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"
  4. Upepo umegeuka, sasa ni Makongoro Nyerere!
  5. DR.BILAL ana nafasi kubwa zaidi kuwa mgombea urais wa CCM 2015
Jumapili njema.

Pasco.
 
This sounds a 1000 of a miracle voice

Is it possible for the sun to rise from west? may be as, for god 1-day might be 1000yrs and 1000yrs can be turned into a day.

Further more it looks easy for the camel to penetrate through a sewing neddle's hole than Nchinbi to become the next president . But with the almighty god anything can happen
 
Pasco,
Nadhani hukupata kupitia huu uzi wa toka August, 2014 Kwanini John Nchimbi hatajwi kati ya watu walioanza mbio za urais?
Wanabodi,

Nimetafakari kidogo bila majibu kwa nini Serikali, baadhi ya Usalama wa Taifa na baadhi ya Wakuu ndani ya CCM wanakuwa wanafiki kiasi hiki juu ya wagombea watarajiwa ambao tayari wamepanga timu zao za maandalizi.

Kwa walio karibu na “corridor of power” hakuna asiyejua state inavyomuandaa John Emmanuel Nchimbi kama mteule mpya wa Mkuu wa Kaya kumrithi pale Magogoni. Mipango yake na harakati zote zinaratibiwa na State. Lowassa anajua, Pinda anajua, Membe anajua na wengine tumepata kujua. Sasa kwa nini kila kukicha wapambe wameng’ang’ana na Lowassa tu kama vile wengine hawafanyi?

Binafsi simaini kama kuna mtu anatarajia kufanikisha jambo lolote maishani bila maandalizi, mikakati na jitihada. Hawa wanaowaandaliawengine ufalme kwa nini hawataki kuona wala kusikia wengine wenye Uwezo wa kujiandalia wakifanya hivyo? Miujiza huonekana kama vitu vitokeavyo bila kutarajiwa lakini nayo ili mtu imtokee lazima afanye maandalizi i.e kutubu, kujitakasa, na kusali kwa imani. Kwa nini hawa “wenye mteule wao mfukoni” hawataki kusikia wenye uwezo wakijiandaa?

Kuanzia sasa nami natangaza kujiunga na timu Lowassa ili nikajue kwa nini anahofiwa kuliko wengine wote.

Kama ilivyo Timu iliyochini ya uratibu wa Apson, ndivyo ilivyo Timu inayoandaliwa na JK. Ina kina Ngeleja wake na January wake-natumaini unanisoma. Apson wakija na wimbo wa "Ujana" Timu JK wanachomoa Kijana kuingia ulingoni, mkisema Waziri Mkuu vilevile wanaye. Lililo wazi katika safu ya Timu JK ni unafiki wa Mkulu katika kuwajaza matumaini wachezaji wake. Kama kawaida, kila mmoja anamuadaa na kumjengea mazingira kwamba ndiye chaguo lake. Pinda nasiki alikuwa mgumu kukubali ofa ya JK. Hata baada ya "NOVENA" imemchukua muda kusema "Niko Tayari" Gia za mwisho mwisho za JK zilizomu-win Pinda ni pale alipoambiwa Wawekezaji wakubwa na wafanyabiashata toka Mataifa makubwa wanataka kujua Rais mtarajiwa ili waweze kufanya maamuzi juu ya uwekezaji wa mitaji yao. Mkumbo huu unawahusisha Wamiliki wa Visima vya Mafuta a Gesi. Kwa hiyo JK akamjulisha Pinda kwamba jina lake tayari limepelekwa kwa Wakubwa wa dunia na hivyo ataanza kuandaliwa shughuli za ndani na ziara za nje kwenda kujiweka karibu na hao Mabwana. Kujua ukweli wa hili fuatilia ziara na Hotuba ya Pinda katika ziara yake Spain na UK. Sikiliza jinsi alivyokuwa anaongea na wawekezaji, akitoa muelekeo wa nchi na msimamo kama mtu mwenye mamlaka ya Serikali hii na ijayo. Anzia hapo.
 
Mkuu Omu, asante kwa hii kitu, ila kiukweli kuna kitu bado sikielewi kwenye hizi groupings!, nijuavyo mimi the main financial wa kambi ya "jamaa yangu", ni yule yule financial wa JK na mtandao wake!, ndio the same financial wa Januari, Ngeleja na Nchimbi!, how does this look?!. Mfadhili huyo ni none other than "the king maker!", 2005, he made JK!, now how many kings does he want to make?!.

Pasco.
 
Pasco,

Kwa CCM everything is Possible , Hata Rage , Maji Marefu , Lusinde Kibabaj, Yule bwe.ge wa Lindi, Komba, Makonda, Sadifa hawa wote wanaweza kupeperusha Bendera ya CCM 2015 Katika Ngazi ya u "Rahisi"
 
Back
Top Bottom