I took it for granted utanielewa. Viti maalum Misingi yake ya kuanzishwa ilikua thabiti na tija sana kwa taifa tokana na kwamba it was believed it would be covered by Women who were qualified and of Potential output to the society. Tokana na kwamba vimechakachuliwa na vingi vimekaliwa na mahawara ama salient nyumba ndogo za wakubwa na wengi wenye hio nafasi kutoonekana Input yao mle ndani na output kwenye jamii HAPANA Havitakiwi viendelee kuwepo! Hopefully umenpata!
My theory kwanini Ukimwi uwepo zaidi hapo....
Katika eneo lililokua linaongoza kwa kutoa vijana wa kazi wake kwa waume wadogo wadogo maarufu kwa House gal na house boy Iringa ndio inayoongoza Tanzania. Ni wafanya kazi wenye adabu, wakarimu, sio wezi na wachapa kazi (hivo ndio sifa zao walizokua wanajulikana nazo); Wanakua ni wadogo na wanasambaa eneo kubwa la Tanzania. Wakienda hio mikoa kama Mbeya (Tunduma na Kyela zina UKIMWI Balaa sababu ya Boarders), Dar, Morogoro wanajenga mahusiano na wenyeji wa huko na ni rahisi kurubunika hasa wanawake.
Wengine wanapata mimba wanarudi majumbani... Wengine ile likizo kuja salimu homu vijana wanapapatikia kumpata for anakua amependeza (mabinti wengi ni maji ya kunde, hua wanarudi wamenawili na kua weupe walo wengi; na waelewa vilevi hivi kwa wanaume). Tokana na kwamba mji ni mdogo, yule binti akilala na vijana wawili tu ama hata mmoja.... Hio chain reaction itayokua hapo ni balaaa!
Katika kutafuta chanzo nimekuta kuwa unywaji wa pombe ya ulanzi unadaiwa pia kuwa chanzo cha kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi Iringa kama inavyosomeka hapo chini.
"KARIBU mchumba, karibu unywe ulanzi, unataka mtogwa (uliogemwa leo) au mkangafu (wa siku nyingi)? Njoo ukae nami hapa usiogope! Mama Anita, lete lita moja fanya haraka mrembo asije akaondoka," hivyo ndivyo nilivyopokewa katika klabu cha pombe cha Nyololo mufindi, Iringa.
Nilikwenda kufanyia kazi utafiti wa wataalamu unaosema kuwa moja ya sababu zinazochangia kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika Mkoa wa Iringa ni ulevi hasa wa pombe za kienyeji.
Mmoja wa wauzaji wa pombe hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe anasema wakati wa msimu wa pombe ya ulanzi, wanywaji wengi hushindwa kuzuia tamaa zao za ngono na kujikuta wakijiingiza katika vitendo hivyo bila kinga.
"Ulanzi ukiwa mwingi ngono pia huwa nje nje! Ndiyo maana msimu wa ulanzi ukiisha tu wanawake wengi huwa na mimba zisizotarajiwa. Ulanzi ni hatari, unasababisha watu washindwe kujizuia na hatuwezi kuuacha kwani ni asili yetu," anasema.
Pombe hiyo iligunduliwa wakati wa utawala wa machifu wa kabila la Wabena katika Wilaya ya Njombe baada ya mti mchanga wa mwanzi kukatika na kuanza kutoa maji matamu. Tangu wakati huo, pombe hiyo imekuwa ikithaminiwa na wakazi wa Mkoa wa Iringa na tayari imesambaa na kufika katika maeneo mengine mengi hasa kusini mwa Tanzania. Wanywaji wengi wa ulanzi wanasema bila shaka kwamba pombe hiyo inachangia kasi ya Ukimwi.
"Msimu wa ulanzi huwa unauzwa bei rahisi ambayo hakuna inayemshinda ndo maana watu wengi hulewa hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ngono bila kujiandaa kwani wanawake wengi wakishanunuliwa kinywaji hicho huwa wepesi kukubali," anasema Richard Mwenda mkazi wa Nyololo.
Mtaalamu na afisa maendeleo ya jamii wilayani Mufindi mkoani Iringa, DEOGRASIA LIGANGA anasema pombe hiyo ndiyo kichocheo kikubwa cha ngono zembe hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi.
"Ulevi hasa wa pombe ya ulanzi unachangia kuongeza hamu ya kufanya ngono zembe, wengi wamejikuta wakipata maambukizi kutoka na pombe hii ambayo inaheshimiwa na wenyeji," anasema LIGANGA.
Ulanzi siyo kichocheo pekee, Liganga anataja mila na desturi potofu ambazo jamii nyingi mkoani humo bado inaziendeleza. Miongoni mwazo ni kurithi wajane, kukosekana kwa usawa kijinsia, kutakasa wajane na wasichana, kuoa wake wengi, imani za kishirikina na kutotahiri.
Nyingine ni umaskini wa kipato. Maisha ya wananchi wengi ni duni. Anasema kutobadili tabia licha ya elimu ya ukimwi kuwafikia wananchi na wengine kuathiriwa kwa njia moja au nyingine na Ukimwi ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ugonjwa huo.
Anataja sababu nyingine kuwa ni muingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli nyingi za biashara na ongezeko la taasisi mbalimbali mkoani humo.
Hali ya maambukizi ikoje?
Katika wilaya ya Mufindi hali ya maambukizi inazidi kutishia amani kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI ambapo kwa takwimu za mwaka huu wilaya ya Mufindi pekee ina asilimia 15.9 ikilinganishwa na kiwango cha mkoa ambayo ni asilimia 13.5
Zaidi:
McDONALD MASSE: ULANZI NOMA KWA UKIMWI MUFINDI