Iringa wapokea Tsh. Bilioni 6.8 za ujenzi wa madarasa

Mukua

Senior Member
Sep 30, 2021
156
202
Kazi inaendelea ujenzi wa madarasa 15,000 nchi nzima unaendelea, leo mkoa wa Iringa wamepokea fedha kwa ajili ya ujenzi huo.

Haya ni matokeo ya kazi na usimamizi mzuri wa makusanyo ya Kodi za wananchi.

Bado Kuna ufufuaji wa viwanda unakuja, hivyo ajira pia zitaongezeka. Kwa Kasi hii naona Tanzania ikiingia kwenye mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.

Tunawaomba wasimamizi wa miradi katika maeneo husika kuzingatia malengo ya kazi kwa manufaa ya Taifa letu.

KAZI INAENDELEA.
 
Mbona hujasema, Rais wetu mpendwa ametoa bilioni 6? Unamaanisha kuwa hizi ni makusanyo ya kodi, ila zile nyingine mlizokuwa mnasema Rais ametoa, zilikuwa pesa za Rais za urithi?
Jiwe ndo alikuwa na hizo tabia za kujichotea fedha bila ya kufuata taratibu.hizi nifedha za serikali sio za mtu binafsi hivyo Rais anajua jinsi ya kuzifikisha kwenye hiyo miradi kwa kufuata utaratibu.
 
Mbona hujasema, Rais wetu mpendwa ametoa bilioni 6? Unamaanisha kuwa hizi ni makusanyo ya kodi, ila zile nyingine mlizokuwa mnasema Rais ametoa, zilikuwa pesa za Rais za urithi?
Bora raisi na serikali wameonesha utu kwa hayo mabilioni ya shilingi. Wengine karibuni na sisi tutaenda mahakamani kufungua kesi nyingine ya mabilioni ya shilingi tulizochangishwa mkutanoni, kisha yakatafunwa na mwenyekiti afu baadae kusingizia kavunjwa mguu na wasiojulikana.

2528007_20200919_173148.jpg
 
Madarasa bila waalimu, Zahanati bila wahudumu. Kuna watu maamuzi huwa wanafanya kwa kutumia MAKALIO.
 
Madarasa bila waalimu, Zahanati bila wahudumu. Kuna watu maamuzi huwa wanafanya kwa kutumia MAKALIO.
Baraka21 mbona unashangaza Sana, ni miaka mingapi ilipita bila ya ajira.
Juzi tu sekta ya afya ajira zimefanyika , hata miezi minne haijapita, waalimu ajira zilimwagwa ,na bado ahadi za kuongeza ajira zinaendelea kutolewa.
Usimchukie mtu mbaya Bali uchukie ubaya. Penye pongezi toa pongezi.
Hauwezi linganisha na miaka mitano iliyo pita.
 
Sio kosa lake huyo, ni kosa la mwenyekiti wake kwenda jela na akili zake. Kila siku tunawaonya kuwa wasimkabizi mwenyekiti wao akili zao. Sasa ona anachoandika jamaa hakiendani na hoja yako hata kidogo.
Hana hoja ye kwake Kila Jambo ni kupinga, hizo ni akili zinazo elekea jioni karibu Zina Zama, zenyewe hazioni lolote Lilo zuri, na bila Shaka zimeathirika na Zina hitaji msaada wa tiba.
 
Huo ni ubinafsi kumbuka kuwa haya Mambo yanakwenda kwa awamu, au we unadhani b 6.8 inaweza kujengwa vyumba vingapi vya madarasa .
Mkuu hivi vyumba vya kujenga kama box ni madarasa au ujinga nenda shule za zamani uangalie ubora wa madarasa uje hapa unambie tunajenga madarasa au ujinga!
 
Back
Top Bottom