VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kwanza nawaomba radhi wana JF kwa kuchelewa kuleta tathmini kuhusu mikoa tajwa hapo juu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Nilipatwa na dharura ya kimaisha iliyonifanya nirudi nyumbani Arusha. Kabla ya kuja huku, nilitembelea mikoa ya Iringa na Mbeya. Nitarejea Moro na tena Njombe kuendelea na ziara zangu.
Pamoja na hali ya kisiasa iliyokuwepo tangu 2015, CHADEMA bado ina nguvu kubwa sana kwenye mikoa hiyo. Kwa Majimbo ya Iringa Mjini na Mbeya Mjini, ni kupoteza nguvu na rasilimali kushindana na CHADEMA. Hata Tunduma na Momba, CHADEMA haina mpinzani.
Kwa upande wetu CCM, viongozi na wanachama wetu wakiwemo watia-nia wanategemea nguvu za Rais Magufuli na dola katika kushinda majimbo na kata. CCM inajiaminisha kuwa upepo wa mwaka huu ni ushindi tu hata kama wagombea wetu hawana nguvu yoyote.
Vyama vingine kama ACT, CUF na NCCR havina nguvu za kutosha kwenye mikoa hii. Kwa kusisitiza, wananchi wa jimbo la Kalenga wanahitaji mabadiliko ya Mbunge. Wanamuita Mbunge wao 'pandikizi' na si chaguo lao. Hadi leo, Mbunge wao hawezi kuzungumza kwa ufasaha kihehe wala kiswahili.
CCM ina kazi kubwa Iringa na Mbeya dhidi ya wenye mikoa hiyo CHADEMA!
Wagombea wapitishwe na vyama, viongozi wachaguliwe na wananchi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)