Iringa municipal vs Shinyanga municipal

Iringa municipal vs Shinyanga municipal

Kadagala 1 hapo kuna picha za Mwanza,
Na hii post ya pili kuna picha ya Dodoma,
Hebu epuka kuwa mkurupukaji.

Post sent using JamiiForums mobile app
Hata mimi nimeshangazwa na huo mzunguko pale Uhindini Dodoma. Hii yote ni kwa faida ya nani?
 
Shinyanga ilidumaa baada ya kilimo cha pamba kufa , kifo cha shirika la reli , mikataba mibovu ya madini na kukosa elimu ya kutumia mifugo yao kujiendeleza. Ukame na mambo ya ushirikina vimeichelewesha sana Shinyanga.
Iringa panazidi kuendelea kwa kasi kwa sababu ya kilimo cha miti , chai , hali nzuri ya hewa , reli ya Tazara ( ingawa si kwa kiwango cha juu lakini imekuwa ikiendelea kipindi ambacho reli ya kati ilisitisha huduma zake ) , ni njia pia inayosafirisha mizigo kwa njia ya barabara kuelekea nchi za Zambia , Congo na Malawi.
Mambo ambayo wanashabihiana watu wa Iringa na Shinyanga uchapaji wa kazi.

Post sent using JamiiForums mobile app
Wewe hujaongea kishabiki mkuu
 
nafikiri Iringa inatakiwa kulinganishwa na Dodoma. hapo itakuwa fair kidogo. dodoma itakachoizidi iringa ni yale majengo ya bunge tu. vingine vyote wako sawa.
 
Ongeeni kwa vigezo, acheni porojo. Wekeni picha, au hata ramani za mipango miji
 
Kadagala 1 hapo kuna picha za Mwanza,
Na hii post ya pili kuna picha ya Dodoma,
Hebu epuka kuwa mkurupukaji.

Post sent using JamiiForums mobile app
We nae ni zwazwa hizo picha ilizoweka hapo zote ni za Shinyanga au ni kiki?
 
Mkuu sema pale kwenye vibanda vya ccm, yote ccm ile.

Ila kiuhalisia huwezi linganisha Shinyanga na Iringa. Iringa iko more decent kulinganisha na Shinyanga.
Yeah iringa ina vyuo vikuu vitatu mkwawa university, iringa university pamoja na Ruaha catholic university. ..sasa njoo shinyanga unitajie chuo kikuu kimojawapo

Post sent using JamiiForums mobile app
 
nafikiri Iringa inatakiwa kulinganishwa na Dodoma. hapo itakuwa fair kidogo. dodoma itakachoizidi iringa ni yale majengo ya bunge tu. vingine vyote wako sawa.
Hapana,hata Morogoro bado Iringa inapitwa. Unajua miji yetu hii ya size ya kati haipishani sana. Yaani Iringa,Mtwara,Morogoro,Kigoma,Moshi,Dodoma. Zipo factor zinazotofautisha lakini siyo kwa kiwango kikubwa.
 
Shinyanga inazidiwa na sumbawanga sembuse iringa?
 
nimeshaishi iringa sana, nimeishi pia shinyanga, lakini ajabu yake, sikuona kama pale shinyanga kuna hata mji, ni kijiji, pamepoaaa kama mji wa wachawi, na nilipendelea zaidi kuishi Kahama kuliko hata shinyanga. shinyanga ni pabaya sana. iringa ni kuzuri isipokuwa hamna hela, at least shinyanga pamezungukwa na migodi ya kahama na ule wa almas, pamoja na kwamba ni bahati mbaya kwao kwamba miners wote huwa wanaspend pesa Mwanza na sio shinyanga. pale wanapita tu kama mtu yeyote yule anayepita.
Kweli kabisa watu huwa wanaenda kuburudika MWANZA au KAHAMA. Ila Shinyanga ni mji MKUBWA kuliko Iringa

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mikoa ya TANZANIA inafanana karibia yote... watu waishio DAR ndio hupenda tabia za kufananisha miji.. nimetembea karibia mikoa yote sasa.. haina tofauti kabisa zaidi ya hali ya hewa.. yaan huku tropical, pale semi desert, kule equatorial etc... Lkn kwa majengo mikoa yote inafanana kwa kiwango kikubwa sana... mikoa yote hii majengo yako sctterd.. huwezi sema hapa ndipo hasa pameendelea...
Mikoa hii ifuatayo inafanana sana tofauti ni hali ya hewa...
IRINGA, MOROGORO, MOSHI, MARA, DODOMA, BUKOBA, MTWARA, RUKWA (SUMBAWANGA), SHINYANGA, SINGIDA NA PWANI...

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mikoa ya TANZANIA inafanana karibia yote... watu waishio DAR ndio hupenda tabia za kufananisha miji.. nimetembea karibia mikoa yote sasa.. haina tofauti kabisa zaidi ya hali ya hewa.. yaan huku tropical, pale semi desert, kule equatorial etc... Lkn kwa majengo mikoa yote inafanana kwa kiwango kikubwa sana... mikoa yote hii majengo yako sctterd.. huwezi sema hapa ndipo hasa pameendelea...
Mikoa hii ifuatayo inafanana sana tofauti ni hali ya hewa...
IRINGA, MOROGORO, MOSHI, MARA, DODOMA, BUKOBA, MTWARA, RUKWA (SUMBAWANGA), SHINYANGA, SINGIDA NA PWANI...

Post sent using JamiiForums mobile app
Somehow,
Mimi pia nimefika mikoa mingi ya Tanzania. Tofauti ipo, ndio maana hata uchangiaji wa pato la taifa unatofautiana toka mkoa mmoja hadi mwingine.
Sumbawanga haiwezi kuwa Sawa na Morogoro,
Pwani hawezi kuwa sawa na Moshi,
Ikumbukwe kuwa mikoa hii inakuwa defined na Shughuli za maendeleo na Kijamii katika kila mkoa husika,
Lazima kutakuwa na Regional Variations.


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Iringa nimekaa sana... Shinyanga nimepita tu.. Mikoa yote haina kitu cha ajabu sana though iringa inakua sana tofauti na shy... Ukiachana na infrastrucrure mpya. Iringa pale mjin n padogo sana..n pamekua scattered. Shinyanga mjin n pakubwa kiaina ila mji umepoa sana.. Bila kusahau baiskeel kama usafiri.. All n all Mikoa mingi ya nchi inafanana sana.. Interms of majengo.. Mengi ni yalijengwa miaka ya nyuma sana au Meng ni ya wahindi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Acha kuishushia hadhi Iringa.

Tafuta mji ulioendelea ndio uulinganishe na Iringa.

Shinyanga ndio kitu gani?
 
Nafikili mleta uzi ungekuwa wazi unalinganisha Iringa na Shinyanga kwa kigezo kipi, lakin hii mikoa haiendan Iringa ni zaid

Labda yaweza kufanana kwa uchangia wa pato la taifa Shinyanga kuna migodi na Iringa kuna wilaya ya Mufindi ambayo inachangia pato kubwa kwa sababu ya uwepo kilimo cha miti

Vinginevyo Iringa ni zaid, nakubaliana na mchangiaji aliyetangulia labda ungelinganisha Iringa na Dodoma au Moshi japo Dom itakua zaid kwa hili la majengo ya serikali, na Moshi miundombinu ya barabara za lami had migombani ndio cha zaid
 
Back
Top Bottom