PreGE2025 Iringa Mjini wamtaja Daudi Masasi ubunge 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
403
Reaction score
676
Anaitwa Daudi Masasi. Huyu ni mzaliwa wa Iringa pande za Nyanda za Juu Kusini.
Mbali na kuzaliwa na kukulia Iringa pia ni mfanyabiashara kwa muda mrefu akiwa pia mdau wa habari.
Alianza kuvuma mwaka 1996 alipoanza kutoa Jarida la Burudani lililojulikana kwa jina la Tabasamu.
Jarida la Tabasamu kwa wale wanaokumbuka vizuri lilitingisha sekta ya burudani kupitia content (mahudhui) ya maneno na michoro ndani ya jarida hilo lililoshika namba moja kwa ubora na umaarufu.
Baadaye, Daudi aliingia kwenye uwanja wa siasa hasa baada ya kuona ndiko mahali ambako ataweza kusimama na kusema ukweli kwa kile ambacho alikiona hakiendi sawasawa katika ustawi wa maisha wa wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake.
Chama alichokielewa sera zake ni Alliance for Democratic Change (ADC).
Ndipo mwaka 2015, Daudi Masasi akaamua kujitumbukiza kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho cha.
Lakini isivyokuwa bahati, kura hazikutosha akibwagwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Kwa sasa Mchungaji Msigwa yupo Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukihama Chadema na siyo mbunge.
Lakini Daudi Masasi hakukata tamaa, mwaka 2020 alitia tena mguu lakini alipigwa 'ovateki' na mbunge wa sasa wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM, Jesca Msambatavangu.
Hata hivyo, Daudi Masasi anasema uchaguzi wa mwaka 2020 haukuwa sawasawa kwa vyama vya upinzani kwa sababu ya mazingira yaliyojitokeza.
Sasa mwaka huu 2025, 'za ndaaani kabisa' zinaeleza kuwa, Daudi Masasi ataingia tena mzima mzima kugombea ubunge wa Iringa Mjini kupitia chama chake hicho hicho cha ADC ikielezwa kuwa, 'inshala', atatoboa.
Wananchi wengi wa Iringa wamesema wanaamini kama uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa huru na haki kama inavyosema serikali, Daudi Masasi atatoboa kwa sababu
FB_IMG_1750751707977.jpg
anaijua Iringa kindakindaki.
Huyu mwagito (mwagito ni mwanaume wa Kihehe) ni mzaliwa na mkazi wa hapa Iringa. Anajua vitongoji vyote. Utamdanganya na nini? Anajua mahitaji gani wana-Iringa tunataka, mahitaji gani hatuhitaji kwa sasa.
"Kwa mwaka huu wana Iringa hebu tumpe mitano tuone mambo makubwa kutoka kwake. Tusichague kwa mazoea. Tusichague kwa kufuata urafiki au undugu. Tumwangalie mtu ambaye atatufaa. Huyu Masasi naamini atatufaa," alisema Mwamuyinga, mkazi wa Miyomboni Iringa.
 
Anaitwa Daudi Masasi. Huyu ni mzaliwa wa Iringa pande za Nyanda za Juu Kusini.
Mbali na kuzaliwa na kukulia Iringa pia ni mfanyabiashara kwa muda mrefu akiwa pia mdau wa habari.
Alianza kuvuma mwaka 1996 alipoanza kutoa Jarida la Burudani lililojulikana kwa jina la Tabasamu.
Jarida la Tabasamu kwa wale wanaokumbuka vizuri lilitingisha sekta ya burudani kupitia content (mahudhui) ya maneno na michoro ndani ya jarida hilo lililoshika namba moja kwa ubora na umaarufu.
Baadaye, Daudi aliingia kwenye uwanja wa siasa hasa baada ya kuona ndiko mahali ambako ataweza kusimama na kusema ukweli kwa kile ambacho alikiona hakiendi sawasawa katika ustawi wa maisha wa wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake.
Chama alichokielewa sera zake ni Alliance for Democratic Change (ADC).
Ndipo mwaka 2015, Daudi Masasi akaamua kujitumbukiza kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho cha.
Lakini isivyokuwa bahati, kura hazikutosha akibwagwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Kwa sasa Mchungaji Msigwa yupo Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukihama Chadema na siyo mbunge.
Lakini Daudi Masasi hakukata tamaa, mwaka 2020 alitia tena mguu lakini alipigwa 'ovateki' na mbunge wa sasa wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM, Jesca Msambatavangu.
Hata hivyo, Daudi Masasi anasema uchaguzi wa mwaka 2020 haukuwa sawasawa kwa vyama vya upinzani kwa sababu ya mazingira yaliyojitokeza.
Sasa mwaka huu 2025, 'za ndaaani kabisa' zinaeleza kuwa, Daudi Masasi ataingia tena mzima mzima kugombea ubunge wa Iringa Mjini kupitia chama chake hicho hicho cha ADC ikielezwa kuwa, 'inshala', atatoboa.
Wananchi wengi wa Iringa wamesema wanaamini kama uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa huru na haki kama inavyosema serikali, Daudi Masasi atatoboa kwa sababuView attachment 3381446 anaijua Iringa kindakindaki.
Huyu mwagito (mwagito ni mwanaume wa Kihehe) ni mzaliwa na mkazi wa hapa Iringa. Anajua vitongoji vyote. Utamdanganya na nini? Anajua mahitaji gani wana-Iringa tunataka, mahitaji gani hatuhitaji kwa sasa.
"Kwa mwaka huu wana Iringa hebu tumpe mitano tuone mambo makubwa kutoka kwake. Tusichague kwa mazoea. Tusichague kwa kufuata urafiki au undugu. Tumwangalie mtu ambaye atatufaa. Huyu Masasi naamini atatufaa," alisema Mwamuyinga, mkazi wa Miyomboni Iringa.
Ni haki yake kikatiba kugombea Hongera zake
 
Back
Top Bottom