figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
IRINGA: Polisi inamshikilia aliyekuwa M/Kiti wa CCM Iringa, Jesca Msambatavangu kwa tuhuma za kuratibu tukio lililopelekea majeraha makubwa mwanamke mmoja.
Amekamatwa na jeshi la polisi mchana wa leo.
=======
Iringa. Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, amekamatwa mchana wa leo Alhamisi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Julius Mjengi, ameliambia gazeiti hili kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita.
Akifafanua, Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta.
"Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu, tumemkamata leo saa nane mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake," alisema Mjengi na kuongeza:
"Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa, walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwanamke huyo hajui ni ya kitu gani," alisema Mjengi.
Alipohojiwa zaidi, Mjengi alikataa kuweka wazi jina la mwanamke na idadi ya watuhumiwa wengine kwa maelezo kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu upelelezi unaoendelea.
Chanzo: Mwananchi