neo1
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 576
- 843
IRGC imesema imekamata meli ya mafuta ya UK Stena Impero
Habari zinasema Stena Impero iliacha maji ya kimataifa na kwenda kwenye visiwa vilivyopo Iran
Meli ilikuwa inaelekea Saudi Arabia.
Hatua hii inafuatia baada ya UK kuikamata Meli ya Iran Grace 1 na Iran iliahidi kulipiza kisasi.
My take mashariki ya Kati inakalibia kulipuka .Hekima,burasa na Maombi vitumike kuepusha balaa.
Link
www.rt.com
UPDATES
Uingeleza imethibitisha Iran imekata meli yake nyingine.
Ivyo Irani imekamata meli mbili za mafuta za Uingeleza.
MAONI YA WADAU
Kilatha said
(1)Kabla ya kuporomoka kwa bei ya mafuta yalikuwa yamefika $120 per barrel if not $125.
Unajua sababu ni nani? US kuamua ku encourage shale drilling ndani kwao na kupunguza import reliance.
US pekee waliweza kufanya kuwe na oversupply ya mafuta yakashuka mpaka $20 dollars per barrel.
Waarabu walijaribu kushusha bei wakitegemea shale drilling watawashinda kwenye cost of production kwa kufurisha soko kwa mafuta wakashindwa uwezi shindana na marekani akiamua kwenye maswala ya uchumi.
Tatu siasa za mafuta zimebadilika sana since Yom Kippur war, Israel tu pekee alikuwa keshafika mpaka Cairo atoe uongozi wote wa Middle East kilichowaokoa waarabu ni S.A kukata mafuta kwa West na madhara yalikuwa makubwa, kiasi kwamba US wakawasii waache kwanza kibano, since then somo lao West walilipata hapo ndio chanzo cha kuanzisha IEA.
Hiyo 3 months reserves usidhani imewekwa kwa bahati mbaya lengo lake ni kujipa muda ikiwa wakipambana tena na waarabu au ikitokea conflict kwenye hiyo region wawe na mafuta ya kutosha kuweza kubadili logistics na sera nyingine ilikuwa kutafuta vyanzo nje ya hizo nchi ambavyo kwa sasa ni vingi.
Watumiaji wa mafuta yanayopita hapo Strait of Hormuz ni Asia kwa asilimia kubwa sio West, yes mafuta yatapanda lakini sio kuwa na madhara makubwa kwao na watu makini kwa sasa wanajipanga kwa logistic kwa hiki kinachoendelea.
Na mwisho seven sisters wa 1930’s sio wa leo, duniani sasa hivi largest oil companies ni host nations corporates like Aramco, China Oil, Petrobas etc.
Bado kuna madhara lakini west washajua namna ya ku minimise risks zao likitokea lakutokea hiyo region, it is not ideal kuivamia Iran. Lakini ukishaleta ubabe kwa hawa watu aminitishi na ukawapa sababu expect hell to follow.
(2) Malcom Lumumba said
Bwana Kilatha nakupa hongera kwa kujenga hoja nzuri na iliyotulia. Lakini bado nachelea kusema kwamba hoja yako haina usahihi sana hivyo tusipoiangalia kwa makini inaweza kupoteza mwelekeo mzima wa huu mjadala wetu:
Mosi, umetoa takwimu kwamba mafuta kabla ya The Shale Revolution yalikuwa ni dola $120-125 kwa pipa, mimi nakanusha maana katika takwimu za miaka kumi hakuna sehemu mafuta yaliwahi kufika bei hiyo. Bei za juu kabisa za mafuta katika kipindi cha nyuma ni hizi hapa. Mwaka 2008 pipa moja lilifika dola 145, mwaka 2011 pipa moja lilifika dola 133, mwaka 2013 pipa moja lilifika dola 118. Katika hili naomba tuweke kumbukumbu sawa kabisa.
Pili, OPEC huwa hawaamui kujipandishia tu bei za mafuta kama wewe unavyosema hapa, huwa kuna sababu ambazo zinahalalisha upandishwaji wa bei za mafuta. Mara nyingi sababu kubwa huwa ni hali ya kisiasa ya eneo au majanga mbalimbali. Hebu tuangalie sasa kwanini bei za mafuta zilikuwa juu sana kabla ya The Shale Revolution ya mwaka 2014.
Mwaka 2008 mafuta yalipanda hadi kufika dola 143 kwa pipa kwasababu ya mtikisiko wa kiuchumi: Mwaka 2011 mafuta yalipanda hadi kufika dola 113 kwa pipa kwasababu ya machafuko yaliyoikuta nchi ya Libya: Mwaka 2013 January mafuta yalipanda bei sana hadi kufika dola 119 kwa pipa kwasababu jeshi la Iran lilikuwa linafanya mazoezi kwenye mfereji wa Hormuz: Mwaka 2013 July mafuta yakapanda tena bei na kufika dola 109 kwa pipa kwasababu ya machafuko ya Misri ya kumtoa Raisi Morsi ambayo yalileta hofu ya kufungwa kwa mfereji wa Hormuz.
Kiufupi kile kilichoitwa The Arab Spring and The Rise of ISIS kilipelekea mlipuko wa bei za mafuta kwa kiwango cha juu sana kwasababu gharama za uzalishaji zinakuwa juu na nchi wazalishaji hujikuta kwenye machafuko. OPEC huwa hawamki tu na kuamua kupandisha bei ya mafuta, japo upandishaji mara nyingine upandishaji wao huibua maswali.
Sasa hivi umejiuliza, siku Iran, Saudi Arabia, UAE na Marekani wanaingia vitani yale mapipa milioni 17 yanayopiya Hormuz kwa siku nani atayafidia ???
Tatu, umeongelea nchi za Magharibi kuwa na sera ya kutunza mafuta kwa miezi mitatu, mimi nasema vyema kabisa lakini nadhani hujalitazama hili jambo katika ukubwa wake. Mafuta kazi yake siyo kuendesha mitambo tu, Asilimia 13% ya mafuta huenda kwenye Petrochemicals ambazo hutumika kuzalisha mbolea, madawa ya binadamu na plastiki. Ndiyo maana mafuta ya kutoka Ghuba ya Uajemi yanaenda kwa wingi barani Asia.
Gharama za uzalishaji wa mafuta zikiwa juu na za shida inamaana gharama za usafirishaji lazima zitakuwa juu tu, hivyo mbolea na vyakula lazima vitapanda bei, hapo bado hujagusa sekta ya afya. Unadhani hayo mafuta ya miezi mitatu yatasaidia ??? Sidhani hata kidogo.......
Nne, hoja yako ya kusema kwamba makampuni ya Magharibi hayana nguvu tena na kwamba makampuni ya nyumbani kama Saudi Aramco ndiyo habari mpya, nadhani haijafanyiwa uchunguzi wa kina. Saudi Aramco ni kampuni kubwa sana duniani lakini kitu ambacho hukijui ni kwamba lipo kwenye ubia mkubwa na haya makampuni ambayo wewe umesema biashara yake iliisha mwaka 1930's, hebu tuangalia kwa undani kidogo:
SAMREF ndiyo kinu kikubwa cha mafuta kule mashariki ya kati ambacho ni sehemu ya Saudi Aramco, lakini ambacho wengi hamjui ni kwamba ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na Exon Mobil ya Marekani.
SATORP nayo ni mkono wa kampuni la Saudi Aramco lakini ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na Total ambalo linamilikiwa na Serikali ya Ufaransa.
SASREF nao ni mkono mwingine wa kampuni la Saudi Aramco lakini ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na The Royal Dutch Shell la Uholanzi.
YASREF nao ni mkono mwingone wa kampuni la Saudi Aramco lakini ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na Sinopec la Uchina.
Hapa utaniambiaje kwamba makampuni ya Magharibi habari yake iliisha miaka ya 1930's ??? Hebu naomba tulijadili hili vizuri.
NB: Kuna kitu kwenye sheria kinaitwa Anti-Trust Law au The Law of Competition, ambapo makampuni makubwa kama Saudi Aramco huwa hayaruhusiwi kutawala biashara ya mafuta peke yao kwasababu ya kuogopa kutengeneza Monopoly ambayo ni hatari kwa afya ya biashara za kimataifa. Refer case ya Standard Oil mwaka 1911...
Makampuni ya Magharibi bado yako kule Mashariki ya kati yakishirikiana na makampuni ya wazawa, katika kuchimba mafuta. Hili linamaanisha yakitokea machafuko pale basi lazima na yenyewe yatatetereka sana.
Mwisho kabisa, kwa siku mapipa milioni tano yanapita mfereji wa Hormuz kuelekea barani Ulaya pekee, utasemaje mtumiaji wa ule mfereji ni Asia peke yake ??? Hebu nieleweshe....

Iran confiscates British tanker in Strait of Hormuz – IRGC
The Islamic Revolutionary Guard Corps has seized the British oil tanker Stena Impero in the Strait of Hormuz, Iranian media reported. UK authorities said the tanker had ‘veered off course’ before capture.