STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,638
- 16,568
- Thread starter
- #81
Hawa sasaivi watapigwa kuanzia Asia mpaka EuropeMambo yalianzia hapa iran walisema israel na marekani watalipa na watajibu na wamejibu kweli
Mambo yalianzia hapa
IRGC: Israel italipa gharama ya kuua shahidi Wairani wawili huko Syria
Mar 09, 2022 10:24 UTC
IRGC: Israel italipa gharama ya kuua shahidi Wairani wawili huko Syria
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema hakuna shaka utawala wa Kizayuni wa Israel utalipa gharama kubwa kwa jinai yake ya kutekeleza shambulizi lililopelekea kuuawa shahidi askari wawili wa SEPAH nchini Syria.
Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano Mwema ya IRGC imeeleza kuwa, shambulizi la kombora la utawala haramu wa Israel viungani mwa mji mkuu wa Syria, Damascus juzi Jumatatu liliua shahidi mashujaa wawili wa jeshi hilo, ambao ni Kanali Ehsan Karbalaeepour na Kanali Morteza Saeednejad.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limesisitiza kuwa, hakuna chembe ya shaka kuwa litalipiza kisasi kwa jinai hiyo iliyofanywa na Wazayuni maghasibu.
Hii si mara ya kwanza kwa utawala huo khabithi kufanya hujuma dhidi ya washauri wa kijeshi wa Kiirani, ambao wako nchini Syria kwa mwaliko rasmi wa Rais halali wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.