Kumekuwepo na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, zikidai kuwa Jeshi la Iran kupitia Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limemnyonga Jenerali Esmail Qaani, ambaye ni kiongozi wa Kikosi cha Quds.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyochapishwa na ukurasa wa Smart tv habari sambamba na Wadada Na Mastory's ya viongozi ndani ya Iran walianza kumtilia shaka Jenerali Qaani baada ya kuokoka mashambulizi kadhaa yaliyodaiwa kufanywa na Marekani na Israel, ilhali baadhi ya makamanda waliokuwa karibu naye walifariki katika mashambulizi hayo.
Ripoti hizo zinaeleza kuwa tuhuma zilianza kuibuka zikidai kwamba huenda Jenerali Qaani alikuwa akishirikiana kwa siri na shirika la ujasusi la Israel, Mossad. Madai hayo yalisababisha taharuki na sintofahamu ndani ya uongozi wa kijeshi wa Iran.
Je ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalosambaa kwa kasi mitandao wa facebook?

- Tunachokijua
- Esmail Qaani ni brigedia jenerali wa Iran katika Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC) na anahudumu kama kamanda wa IRGC Quds Force, kikosi maalum cha operesheni za kijeshi kinachohusika na shughuli za nje ya mipaka ya Iran.
Madai
Kuanzia Machi 05, 2026 kumekuwa na Taarifa zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikidai kuwa Brigedia Jenerali Esmail Qaani ameuliwa na jeshi la Iran kwa sababu ya usaliti.
Uhalisia wa madai hyao ni upi?
Baada ya ufuatiliaji imebainika kuwa Taarifa hiyo si ya kweli na haina msingi wowote wa uhalisia.
Taarifa hiyo imesambazwa na vyanzo ambavyo si vya kuaminika ama akaunti za watu binafsi tu, na hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.
Kumbukumbu zilizopo zinaonesha kuwa bado Brigedia Jenerali Esmail anahudumu katika nafasi yake ya Kamanda wa jeshi la mapinduzi la kiisalamu kikosi cha Quds.