Iran wazindua drone yao mpya waipa jina la "GAZA" inakaa angani masaa 35 bila kutua

Hivi sayansi na engineering wanazosoma wenzetu na sisi watanzania tunafundishwa hizo hizo? Kama Hilo taifa linaweza kufanya hayo yote sisi tunashindwa nini?
Mkuu hivi huna habari kwamba huku kwetu ukibainika tu unatengeneza hata bunduki (gobole) Unafungwa?.
 
Iran yazindua droni yake ya Ghaza na mafanikio yake mapya ya kijeshi.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mafanikio matatu makubwa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ikiwemo droni (ndege isiyo na rubani) ya Ghaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, wakati huu wa kukaribia Khordad 3 kwa kalenda ya Kiirani ya Hijria Shamsia ambayo ni "Siku ya Muqawama, Kujitolea na Ushindi" Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limezindua mafanikio matatu muhimu na ya kiistratijia ya kiulinzi na kijeshi, katika sherehe zilizohudhuriwa na Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la SEPAH na Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran.

Miongoni mwa sifa maalumu za ndege isiyo na rubani ya Ghaza ni uwezo wake mkubwa wa kiulinzi na kijeshi, utafiti na ugunduzi na kuruka angani kwa muda wa masaa 35.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la SEPAH katika sherehe za uzinduzi wa mafanikio mapya ya kiulinzi ya Iran

Droni hiyo ya Ghaza ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ina uwezo pia wa kubeba mabomu 13 na kuruka umbali wa kilomita 2000. Ina uwezo wa kubeba kilo 500 za zana za kijeshi na pia kukusanya taarifa za kijasusi na za kiishara. Kuingia droni hiyo ya kisasa katika orodha ya ndege zisizo na rubani za SEPAH kumezidisha sana uwezo wa ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mbali na matumizi ya kijeshi, droni ya Ghaza inaweza kutumika pia katika tafiti mbalimbali zikiwemo za kwenye misitu, operesheni za misaada, uokoaji na ufikishaji misaada nyakati za ajali na majanga ya kimaumbile kama vile mafuriko, mitetemeko ya ardhi n.k.

View attachment 1794193
Magufuli angekuwa hai, jeshi la Tanzania lingetengeneza bomu zuri na bora kuliko hili.
 
Nadhani ingekuwa ni kipimo kizuri sana kama wataitest kwa kuipitisha kwenye anga la israel.tuone je yaliyomo yamo
 
Hiyo ndege imecopy drone ya Israel na marekani so hadi spare parts wataagiza tu huko huko walupocopy kwa njia zile zile za Magendo watu wa dini hao katika ubora wao
Nyinyi nchi yenu imeishindwa kukopi hata mbinu za kutengeneza toothpick, shame on you.
 
Hivi sayansi na engineering wanazosoma wenzetu na sisi watanzania tunafundishwa hizo hizo? Kama Hilo taifa linaweza kufanya hayo yote sisi tunashindwa nini?
Huko mashuleni wanafunzi wenu wanalishwa ugali na maharagwe mabovu plus makande, hizo akili za ugunduzi watazitoa wapi ?
 
Vikwazo dhidi ya Iran vimeendelea kuleta athari chanya kubwa kwa Iran na kuzifanya nchi Ile kuwa miongoni regional powers zenye ushawishi mkubwa kuanzia Afghanistan, Lebanon, Syria , Iraq nk.

Wairan walishagundua bila wao kujifunza mbinu za kutengeneza AK-47 hakuna atakaewasaidia Hilo. Pia wakaigundua bila kusomesha mainjinia wakubwa hawataweza kutengeneza chochote si silaha, so madaraja Wala majumba.

Walipogundua pia wasipojitengenezea dawa watakufa wakichekwa na Wamagharibi wakaamua kujenga viwanda vikubwa vya madawa huko middle East.

Walipogundua Marekani na Urusi Ni baba zao kijeshi wakaanza kuiba teknolojia za kijeshi Leo wao si wa mchezomchezo.. world powers huja kwa upole wazungumze na sio kuwatisha ili wasarende.

Watanzania Kuna haja ya kujitegemea kama taifa . Kwani so tunafeli wapi kuwa n teknolojia hata Kama kule walipo waturuki na wairan?
Nb. Vikwazo pia vimeendelea kuwa na athari mbaya zaidi kiuchumi kws wairan wengi
Tutaendeleaje wakati akina kingwala wanaiba mabilioni bila kuchukuliwa hatua, hatua kubwa wanayochukuliwa ni kusimamishwa miezi 6 wanasema kupitisha uchunguzi thn wanateuliwa nafasi nyengine kama kwamba hakuna wasomi vijana amabao wamehitimu masomo yao vizuri, vijana wanabaki na bodaboda mitaani na elimu degrees zao, sasa hapo maendeleo yatatoka wapi wakati ukiangalia nchi kama Iran juu ya vikwazo vyao wanapokuona au kushtukia kama ni fisadi wa mali ya umma wanakumyonga mojakwamoja
 
Ah kiukweli hatua tunazochukua leo kuekekea maendeleo yetu zilipaswa kuanza 1961, Ila kwa sababu ya rushwa, kujuana, na kukatiana pande Leo bado tuko nyuma. Kisingizio kikubwa kwanini bado tuko nyuma utaskia mabeberu! Aibu! Aibu!
Huyo beberu ndo anakuuzia dawa za ARV!
Huyohuyo silaha!
Huyohuyo dawa!
Sijawahi kuacha kushangaa Jambo Hilo la ovyo
 
Hivi sayansi na engineering wanazosoma wenzetu na sisi watanzania tunafundishwa hizo hizo? Kama Hilo taifa linaweza kufanya hayo yote sisi tunashindwa nini?
Sisi tumeaminishwa kuwa hivyo vitu wanatengenezewa na rafiki zao aliens kwahiyo sisi hata tusivisumbukie.
 
Back
Top Bottom