Kama siyo Jeshi la Iran basi sahivi USA na Ulaya ingetawaliwa na magaidi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Kama siyo Jeshi la Iran basi sahivi USA na Ulaya ingetawaliwa na magaidi

Rais Ebrahim Raisi wa Iran amepongeza nafasi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika kukabiliaina na ugaidi katika eneo la Asia Magharibi na kueleza kuwa, bila jitihada za SEPAH, nchi za Ulaya hivi sasa zingekuwa zimetamalakiwa na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).

Rais Raisi alisema hayo jana Ijumaa akihutubia Kongamano Kuu la 24 la Makamanda wa Jeshi la SEPAH hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, "Iwapo IRGC na wapiganaji shupavu wa umma wa Kiislamu wasingelichukua hatua dhidi ya Daesh, Ulaya hivi sasa ingekuwa imetawaliwa na kundi hilo la kigaidi."

Amesema amani inayoshuhudiwa hivi sasa barani Ulaya ni matokeo ya juhudi za IRGC, lakini kwa bahati mbaya wanawaua mashujaa waliopambana na magaidi, huku wakidai kuwa SEPAH ambayo iliongoza vita dhidi ya ugaidi, eti kuwa ni kundi la kigaidi.

Huku akiitaja IRGC kama mwana mbarikiwa wa Mapinduzi wa Kiislamu, Rais wa Iran ameeleza bayana kuwa, jeshi la SEPAH limekuwa na majukumu mengi, lakini muhimu zaidi ya yote ni kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

[https://media]Sayyid Raisi na makamanda wa IRGC

Kabla ya hapo, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran juzi Alkhamisi alisema kuwa, kuasisiwa, kukuwa, kustawi na kuwa imara katika kupambana na migogoro sambamba na kazi nyingine za Jeshi la SEPAH katika upande wa kijeshi, kutumikia wananchi, kutoa huduma na kazi za ujenzi wa taifa, kumelifanya jeshi hilo kuwa la kipekee na la kujivunia.

Vilevile alisema, kupungua na kutorudiwa kusemwa na maadui kwamba "chaguo la kijeshi dhidi ya Iran liko mezani," kunatokana na nguvu za kuzuia mashambulio za IRGC.

Jeshi la SEPAH liliundwa mnamo Aprili 22 mwaka 1979 na Muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (MA), huku jukumu lake kuu likiwa ni kulinda Mapinduzi ya Kiislamu.

4c3oa942f53a352cj21_800C450.jpg
 
Wavaa kobazi bhana. Magaidi ndiyo hao hao waislam kutoka Iran sijui unawaongelea magaidi gani.
Islamic state (IS), Al Qaeda, Boko Haram, Al Shabab, Daesh (ISIS) n.k hivi vyote ni vikundi vya kigaidi vya kiislamu.
Ukisikia Takbir, ujue kuna gaidi amevaa mabomu
 
Back
Top Bottom