Iran wazindua drone yao mpya waipa jina la "GAZA" inakaa angani masaa 35 bila kutua

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
6,026
2,000
Iran yazindua droni yake ya Ghaza na mafanikio yake mapya ya kijeshi.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mafanikio matatu makubwa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ikiwemo droni (ndege isiyo na rubani) ya Ghaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, wakati huu wa kukaribia Khordad 3 kwa kalenda ya Kiirani ya Hijria Shamsia ambayo ni "Siku ya Muqawama, Kujitolea na Ushindi" Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limezindua mafanikio matatu muhimu na ya kiistratijia ya kiulinzi na kijeshi, katika sherehe zilizohudhuriwa na Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la SEPAH na Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran.

Miongoni mwa sifa maalumu za ndege isiyo na rubani ya Ghaza ni uwezo wake mkubwa wa kiulinzi na kijeshi, utafiti na ugunduzi na kuruka angani kwa muda wa masaa 35.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la SEPAH katika sherehe za uzinduzi wa mafanikio mapya ya kiulinzi ya Iran

Droni hiyo ya Ghaza ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ina uwezo pia wa kubeba mabomu 13 na kuruka umbali wa kilomita 2000. Ina uwezo wa kubeba kilo 500 za zana za kijeshi na pia kukusanya taarifa za kijasusi na za kiishara. Kuingia droni hiyo ya kisasa katika orodha ya ndege zisizo na rubani za SEPAH kumezidisha sana uwezo wa ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mbali na matumizi ya kijeshi, droni ya Ghaza inaweza kutumika pia katika tafiti mbalimbali zikiwemo za kwenye misitu, operesheni za misaada, uokoaji na ufikishaji misaada nyakati za ajali na majanga ya kimaumbile kama vile mafuriko, mitetemeko ya ardhi n.k.

4by1922af2b6bc1vkbs_800C450.jpeg
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,923
2,000
Hivi sayansi na engineering wanazosoma wenzetu na sisi watanzania tunafundishwa hizo hizo? Kama Hilo taifa linaweza kufanya hayo yote sisi tunashindwa nini?


Kuna kusoma (learning ) na kuchukua (acquisition), sisi tunachukua elimu na hatujifunzi elimu, unapojifunza elimu ndipo unapoweza kufainyia kazi zaidi ya kile ulichojifunza kitu ambacho wenzetu ndivyo wanavyofanya.
 

Sela Son

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
1,025
2,000
Vikwazo dhidi ya Iran vimeendelea kuleta athari chanya kubwa kwa Iran na kuzifanya nchi Ile kuwa miongoni regional powers zenye ushawishi mkubwa kuanzia Afghanistan, Lebanon, Syria , Iraq nk.

Wairan walishagundua bila wao kujifunza mbinu za kutengeneza AK-47 hakuna atakaewasaidia Hilo. Pia wakaigundua bila kusomesha mainjinia wakubwa hawataweza kutengeneza chochote si silaha, so madaraja Wala majumba.

Walipogundua pia wasipojitengenezea dawa watakufa wakichekwa na Wamagharibi wakaamua kujenga viwanda vikubwa vya madawa huko middle East.

Walipogundua Marekani na Urusi Ni baba zao kijeshi wakaanza kuiba teknolojia za kijeshi Leo wao si wa mchezomchezo.. world powers huja kwa upole wazungumze na sio kuwatisha ili wasarende.

Watanzania Kuna haja ya kujitegemea kama taifa . Kwani so tunafeli wapi kuwa n teknolojia hata Kama kule walipo waturuki na wairan?
Nb. Vikwazo pia vimeendelea kuwa na athari mbaya zaidi kiuchumi kws wairan wengi
 

Ausar

JF-Expert Member
Mar 19, 2021
308
500
Ndo maana kafadhili hamas yale maroketi inawezekana alikua anasoma hesabu za ile iron dome......hadi drone kaipa hili jina........Iran anajifua kupitia hizi proxy wars na Marekani na Israel.........Syria kasaidia huku anatest mitambo yake....huku palestina ndo hivo tena, acha zirudi enzi za Persia
Screenshot_20210522-224012_Samsung Internet.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom