Uanachama wa BRICS umevunja sera ya US ya kuitenga Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Uanachama wa BRICS umevunja sera ya US ya kuitenga Iran

Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kupewa uanachama Iran katika kundi la BRICS kumesambaratisha sera ya Marekani ya kujaribu kuitenga Jamhuri ya Kiislamu.

Ali Akbar Velayati amesema hayo katika mahojiano na kanali ya habari ya al-Mayadeen ya Lebanon na kuongeza kuwa, kukubaliwa Iran kuwa mwanachama wa BRICS kumetikisa na kupunguza imani ya nchi za eneo kwa Marekani.

Dakta Velayati amefafanua kuwa, "Uanachama huu umefanya mwenendo wa Iran wa kujielekeza Mashariki na pia kuimarisha ushirikiano wake na mataifa ya eneo, kuwa sera kuu za nje za Jamhuri ya Kiislamu."

Velayati ambaye ni Mshauri wa Kiongozi Muadhamu katika masuala ya kimataifa ameeleza kuwa, kukubaliwa Iran kuwa mwanachama wa BRICS kumethibitisha kujitolea kwa nchi hii kuimarisha ushirikiano na nchi za dunia, na kufanikiwa kwake kuvunja mradi wa Marekani wa kulitenga taifa hili.

Iran pamoja na nchi nyingine tano zilikubaliwa kujiunga na kundi la BRICS katika mkutano wa 15 wa kilele wa jumuiya hiyo ya kiuchumi uliofanyika kuanzia Jumanne hadi Alkhamisi ya wiki iliyopita huko Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Rais wa Iran katika mkutano wa BRICS
Moja ya malengo ya BRICS ni kujitenga na sarafu ya dola katika miamala ya biashara ya kimataifa. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo ikiwa na lengo la kufubaza vikwazo vya Marekani, imeliweka katika ajenda zake suala kufanya biashara na sarafu za kitaifa au sarafu zinginezo lakini sio sarafu ya dola, inaweza kunufaika vyema na sera hii ya BRICS.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, "Sera ya kuitenga Iran bila shaka imefeli, na waliojaribu kuitenga nchi hii wameishia kujenga uzio (unaowatenga) wenyewe."

4c3o8f7ccc662d2co6i_800C450.jpg
 
Iran kwa propaganda tu hawajambo wako sawa tu na Russia, China na North Korea.
 
Napenda namna Iran inafukuzia ushirikiano wa kiuchumi na mataifa mbalimbali ukiondoa ushirikiano wa kijeshi, NK kuna kitu anakosa katika kutanua wigo wake kiuchumi na mataifa mbalimbali regardless ya vikwazo alivyo wekewa
na vikwazo yuko hapo hakuna kibaraka wa marekani anamuweza mashariki ya kati ,mambo yakifunguka atakua hatari zaidi
 
Wewe na Ayatollah hamuelewei vikwazo vya marekani na washirika wake vinavyofanya kazi. Iran kujiunga BRICS, AU au kokote kule hakutabadilisha kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom