Iran kununua ndege 118 kutoka Boing na Airbus

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,826
1,730
Gazeti la New York times na Aljazeera news wanaripoti kuwa Serekari ya Marekani imetoa kibali kwa Boing na Airbus kuwauzia ndege Iran. na Tayari serekari ya Iran imesaini mkataba na makampuni hayo kununua ndege zipatazo 118 zikiwemo ndege zenye sifa ya kuitwa '' Super Jumbo''

Na tayari mzigo wa ndege 17 ziko tayari

Dah!! mdogo mdogo nasisi tutafika tu

Ni hayo tu.
 
Ukiwa na ndege 20. Ambapo 15 zikiwa zinaoperate regional na domestic na 5 nyingine international itakuwa ni hatua Kubwa Sana sio tu katika ajira Bali hata uchumi wa nchi .
Tayari sisi tunazo mbili, Rwanda wanazo 11, Uganda shirika kama limekufa vile na wenzetu kenya wanazo kadhaa. EAC tuongeze jitihada.
 
Gazeti la New York times na Aljazeera news wanaripoti kuwa Serekari ya Marekani imetoa kibali kwa Boing na Airbus kuwauzia ndege Iran. na Tayari serekari ya Iran imesaini mkataba na makampuni hayo kununua ndege zipatazo 118 zikiwemo ndege zenye sifa ya kuitwa '' Super Jumbo''

Na tayari mzigo wa ndege 17 ziko tayari

Dah!! mdogo mdogo nasisi tutafika tu

Ni hayo tu.
Tanzania tutanunua moja to toka Boing na airbus....na matarumbeta juuu kama vile tumenunua dunia nzima....hahaha.
 
Hapo ndio utakapo jua wenzetu wanapotofautisha siasa na biashara.Siasa zao zinabaki kuwa siasa na biashara inabaki kuwa biashara.Kwetu siasa na biashara zote zinachanganywa mbaya zaidi mfanyabiashara anaonekana adui mpiga madili lazima aishi kishetani
 
Mungu jaalia tusije pata vikwazo kama Iran, jamaa wamesimama kweli kiuchumi, nadhani kuna sehemu tunakosea kama Taifa. Ukiwa Irq Taxi nyingi made in Iran, wanatengeneza machine nyingi hizi za small scale, machine za juice, machine za kuisaga nafaka, Fridge, in fact electronics wako mbali sana hawa jamaa, ukigia super markets nyingi kule Bagdad an miji mikubwa Iraq na Lebanon bidhaa nyingi ni Made in Iran, alafu hawana mbwembwe kabisa , wana nidhamu ya hali ya juu, mimi nafikiri ni vyema tusimame kama taifa badala ya kumwachia Mheshimiwa Rais peke yake
 
Iran wamewekeza kwenye teknolojia wana vyuo vizuri vya teknolojia

Angalia budget yao kwenye science na teknolojia ni mabilioni ya pesa

Nchi mpaka inatengeneza ballistic missiles nk ujue kweli wamewekeza kwenye teknolojia

Nchi za Africa haswa Tanzania hatujawekeza kwenye teknolojia ,wanasayansi wa TZ wana impact gani

Budget ya serikali kwenye teknolojia ni kiasi gani wanatoa

Tz bado sana tujikite kwenye kilimo basi

Ni hayo tu
 
Kilimo chenyewe hatukiwezi,tuna mito mingi na maziwa ya kutosha,cha kushangaza neno NJAA limekuwa ndio wimbo katika nchi.
 
Nafikiri sera ya viwanda ingewekwa kwenye Sera na ikapewa Muda wa kutosha , na isiwe agenda ya Chama au kingozi ila iwe ni ya kitaifa ambayo yampasa kila kigonzi kuitekeleza, hata kama anatoka Upinzani
 
Back
Top Bottom