Kuna kitabu kimeandikwa na mwanahistoria David Talbot kinaitwa The Devil's Chessboard:Allen Dulles, the CIA and the Rise of America's Secret Government. Humo ndani mwandishi anaelezea kwamba CIA ni chombo cha ajabu mno ambacho kiuhalisia hakiwajibiki kwa mtu hata kwa Raisi wa nchi.
Anasema The Dulles Brothers ni moja kati ya watu waliowahi kuwa na nguvu kubwa sana nchini Marekani na walimshinda hadi Raisi John F Kennedy. Mwanzoni mwa utawala wa Kennedy, 1961 kulikuwa na uasi mkubwa wa kijeshi kwenye koloni la Ufaransa la Algeria (Algiers Putsch) ambapo yalilalizimisha serikali ya Jenerali Charles De Gaulle kutii matakwa yao ya kutoruhusu Algeria iwe nchi huru kwa kuogopa ukomunisti.
Paris wakapiga simu Washington kuuliza kwanini majasusi wenu wanataka kuivuruga Ufaransa ??? Raisi Kennedy akashituka sana na kusema kwamba yeye hana ufahamu wowote ule kuhusu huo mkakati. Kumbe Mkurugenzi Allen Dulles ndiyo kauratibu mkakati mkubwa hivyo bila idhini ya Raisi. Sasa kama walifanya hivyo miaka ya 1961 leo hii watakuwa wanafanya nini ???
JF Kennedy alimfukuza kazi Allen Dulles, na kuahidi kuivunja CIA vipande vipande lakini kumbe Dulles alikuwa bado ni mkurugenzi kivuli (The Shadow Director) ambaye alikuwa anakaa kwenye nyumba ya siri ya CIA huku akiendelea kuendesha mfumo. Talbot anasema kwamba Lee Harvey Oswald alikuwa anapokea amri kutoka kwa wakina Dulles.
Sasa nini kilitokea: JF Kennedy kauwawa aliyekuwa mwenyekiti wa The Warren Commission iliyochunguza kifo cha Raisi unajua alikuwa nani ??? Allen Dulles, mtu yuleyule ambaye Kennedy alimfukuza kazi kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria za nchi.
Mwisho kabisa: Raisi wa Marekani Harry S Truman kwenye kumbukizi zake (Memoirs) aliandika majuto yake ya kutoridhishwa na mwenendo wa CIA na akasema hakutegemea kwamba ingegeuka kuwa vile. Anasema vyeo vya juu kabisa vya CIA vilijaa watoto wa matajiri wa WallStreet ambao walikuwa na ajenda zao wenyewe na wenye nguvu kubwa sana ya ushawishi na pesa.
Jambo hili Jenerali Dwight Eisenhower alikuja kuligundua baadae na kuna kipindi hadi yeye alikataziwa kufahamu nini kilichokuwa kinaendelea Area 51, akaamua kutishia kuvamia na nguvu ya jeshi ndiyo akaambiwa atume wawakilishi wa Ikulu ili wakakague kilichokuwa kinaendelea mle ndani. Haya siyo maneno yangu bali maneno ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Canada Paul Theodore Hellyer. (Japo wengi wanambishia)
Mwishoni kabisa anamaliza Uraisi wake mwaka 1961 Dwight Eisenhower naye alionekana kutoridhika na mwenendo wa The State of Security na aliwaonya sana Wamarekani kwamba " Be ware of the Military Industrial Complex".
Kitafute kitabu cha Talbot ni kizuri sana, kinafikirisha na kimejaa rejea za kutosha zenya kushawishi. Soma halafu toa hukumu yako mwenyewe.
NB: Jambo nalowaza ni kwamba tunasema Donald Trump ni mtu asiyependa vita lakini je kutopenda kwake vita kunaweza kubadilisha chochote kile nchini Marekani ??? Upande mwingine tusisahau kwamba Donald Trump ni sehemu ya mfumo wa Marekani unaopingana na mfumo mwingine wa Marekani lakini wote hao lengo lao ni moja na taasisi wanazozitumia ni zilezile tu.
TUJITEGEMEE,
Barbarosa ,
Red Giant