SI KWELI Iran imesababisha mlipuko mkubwa umetokea kwenye jengo la mahakama georgia Marekani

SI KWELI Iran imesababisha mlipuko mkubwa umetokea kwenye jengo la mahakama georgia Marekani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
659146287_947558794798495_3648674863573247240_n.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa kumetokea mlipuko mkubwa katika jengo la kihistoria la mahakama huko Georgia, Marekani.

Mathalani chapisho moja limekuwa likisambazwa kupitia makundi mbalimbali katika mtandao wa Facebook likiwa na ujumbe unaodai kuwepo kwa tukio hilo na nukuu inayosema "Kisasi cha Iran kimefika hatua mbaya zaidi kwa sasa."


Ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Moto mkubwa uliosababisha uharibifu mkubwa katika jengo la kihistoria la Mahakama ya Kaunti ya Floyd ulisababisha kufungwa kwa mahakama na kuvuruga shughuli za serikali katika kaunti hiyo. Inaelezwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo

Hali ya dharura ya kimahakama ilitolewa siku ya Jumatatu baada ya moto kuzuka katika jengo la mahakama lililopo West Fifth Avenue, jambo lililopunguza upatikanaji wa jengo hilo na kuzua wasiwasi wa usalama.

Chini ya amri hiyo ya dharura, mahakama ilifungwa siku ya Jumanne na kutarajiwa kufunguliwa tena Jumatano, isipokuwa kama amri hiyo itaongezewa muda. Kesi zote za madai na jinai zimeahirishwa, huku muda wa mwisho wa taratibu za mahakama ukisimamishwa kwa muda.

Tume ya Kaunti ya Floyd inatarajiwa kujadili utoaji wa fedha za dharura ili kuhamisha shughuli zilizokuwa zikifanyika katika jengo la kihistoria la Mahakama ya Kaunti ya Floyd, ambalo liliteketea kwa moto siku ya Jumatatu.

“shukurani zetu nyingi ziende kwa mwitikio wa haraka na kazi kubwa ya wahudumu wetu wote huduma ya kwanza,” alisema Mwenyekiti wa Tume hiyo, Rhonda Wallace.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kaunti ya Floyd, Jamie McCord, watu wote waliokuwa ndani ya jengo hilo walifanikiwa kuhamishwa salama baada ya moto kuripotiwa saa 2:12 mchana. Baada ya kutoka nje, wasimamizi walifanya ukaguzi wa majina ili kuhakikisha kila mtu ametoka salama.​

Similar Discussions

Back
Top Bottom