IPTL yamdai Zitto bilioni 500 mahakamani

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,643
Reaction score
164,790
Hiyo ni taarifa ya magazeti ya leo kupitia TBC 1.

Hivi katika kesi za aina hii ni nani aliwahi kuhukumiwa kulipa hata sh moja?!

Hizi huwa ni kesi hewa tu na za kisanii!
===================

KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakimtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe awalipe fidia ya Sh bilioni 500 kutokana na kutoa kashfa dhidi yao.

IPTL, Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo mawili, Harbinder Seth wamefungua kesi dhidi ya Zitto, Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics.

Washitakiwa wengine wameshitakiwa kwasababu makala yenye maneno ya kashfa na kuwachafua, iliyochapishwa Agosti 13 mwaka huu katika ukurasa wa 7 na 14 wa gazeti lao, ikiwa na kichwa cha habari cha "Fedha za IPTL ni Mali ya Umma" na Kampuni ya Flint Graphics kwa kuchapisha gazeti hilo.

Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru makala hayo, yalikuwa ya upotoshaji na kuwachafua kwa kudhamiria, pia wadaiwa waombe radhi kwa kuchapisha habari ya kuomba msamaha kwenye kurasa za mbele katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo.

Wadaiwa hao waliiomba Mahakama, itoe zuio kwa wadaiwa, watumishi wao, wafanyakazi, washirika, wawakilishi au watu wengine wanaofanya kazi chini ya wadaiwa, kuchapisha au kuandika makala yoyote ya kuwachafua.

Wanadai makala hayo yalikuwa na maneno "kwa mara nyingine Serikali kupitia viongozi wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba dola milioni 250 za Kimarekani zilizopaswa kuendelea kuwepo katika akaunti ya "Tegeta Escrow Account' si mali ya Serikali na hivyo si mali ya umma….

Akaunti hiyo ilifunguliwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Tanesco pamoja na IPTL".

Ilidaiwa kuwa kabla ya kusambaza habari hizo, wadaiwa walitakiwa kufanya juhudi za kuthibitisha ukweli kutoka kwao au kwa maofisa husika wa Serikali, ambao wangethibitisha ukweli kuwa fedha zilizowekwa kwenye akaunti ya Escrow, zilikuwa ni dola milioni 122 za Kimarekani na siyo dola milioni 250, kama walivyodai.

Aidha, wangejua fedha ziliwekwa katika makubaliano ya Escrow ;na siyo kama fedha za umma, lakini ni kutokana na mgogoro wa malipo, yaliyotakiwa kufanywa na Tanesco kwa IPTL.

Wadai hao walifungua kesi hiyo Septemba 4, mwaka huu kupitia kwa Wakili Melchisedeck Lutema na Kay Felician Mwesiga.

Chanzo: Habari leo
 
Hiyo ni taarifa ya magazeti ya leo kupitia TBC 1.

Hivi katika kesi za aina hii ni nani aliwahi kuhukumiwa kulipa hata sh moja?!

Hizi huwa ni kesi hewa tu na za kisani!

Hata gaezti moja hulijui jina???!!!
Umesikia hilo jina tu???!!!
 
Sasa amefunguliwa kesi na kampuni ya IPTL akidaiwa fidia ya Tshs Bilioni 500.

Chanzo. NIPASHE.
 
Wanatamani sana wawazibe watu midomo ili waendelee kutafuna nchi sawa sawa....
 
Wiki chache baada ya kumshtaki Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wenzake wawili, sasa imemgeukia Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa kumfungulia kesi ya madai ya fidia ya Sh. bilioni 500 Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

IPTL pamoja na wadai wenzake wanaiomba mahakama imwamuru Zitto kulipa fidia hiyo kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kimaandishi.Wadai wengine katika kesi hiyo ni Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sing Seth.

Kesi hiyo ilifunguliwa katika mahakama hiyo, Septemba 4, mwaka huu, kupitia Wakili Melchisedeck Lutema kutoka Kampuni ya Mawakili ya Asyla Attorneys na Kay Felician Mwesiga kutoka Kampuni ya Mawakili ya Bulwark Associates Advocates.

Pamoja na mambo mengine, wadai hao wanataka Zitto aamriwe kulipa fedha hizo.

Mbali na Zitto, wadaiwa wengine katika kesi hiyo, ni Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics.

Wote wanatakiwa kulipa fidia inayodaiwa kuwa inatokana makala ya kuwachafua iliyochapishwa kwenye gazeti hilo iliyosababishwa na wadaiwa hao.

Wadai pia wanataka mahakama hiyo itamke rasmi kwamba, makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Fedha za IPTL ni Mali Ya Umma” iliyochapishwa katika ukurasa wa saba na 14 za gazeti hilo la tarehe 13 Agosti, mwaka huu, ilikuwa ni ya kupotosha.

Wanadai kuwa na kupotosha, makala hiyo pia ilikuwa ni ya kuchafua kwa kudhamiria na kuhitaji wadaiwa kuomba radhi kwa kuandika na kuchapisha katika kurasa za mbele kichwa cha habari ya kuomba msamaha katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo.

Pia wadai wanaiomba mahakama hiyo kuweka vizuizi vya kudumu kwa wadaiwa, watumishi wao, wafanyakazi wa shirika, wawakilishi au watu wengine wowote wanaofanya kazi chini ya wadaiwa kwa uchapishaji, kuchapisha au usababisha kuandika na kuchapishwa kwa makala yoyote ya kuwachafua.

Wanadai IPTL iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa umeme unaozalishwa na mdai (IPTL) utakuwa ukinunuliwa na kusambazwa na Tanesco kwa bei waliyokubaliana.

Inadaiwa kuwa katika kurasa namba saba na 14 za Raia Mwema la Agosti 13, mwaka huu, Zitto aliandika wakati mdaiwa wa pili, wa tatu na wa nne walihariri, kuchapa na kusambaza makala, ambayo ilikuwa ni ya uongo na ya kuwachafua wadai.

Katika hati ya mashtaka, wadai wanadai kuwa makala hiyo ilikuwa na maneno yafuatayo yaliyokuwa si ya ukweli na ya kuwachafua wanaodai: “Kwa mara nyingine, serikali kupitia viongozi wake, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),

….wamedai kwamba, Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika “Tegeta Escrow Account’ si mali ya serikali na hivyo, si mali ya umma...Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Tanesco pamoja na IPTL.”

Inadaiwa kuwa pasingekuwa na nia ya dhati ya kumchafua mdai, mdaiwa asingechapisha na kusambaza maneno yaliyonukuliwa kama angefanya juhudi za kuthibitisha ukweli kutoka upande wa pili (kwa mdai) au kutoka kwa maafisa husika wa serikali, ambao wangethibitisha kwamba:

“Kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti ya Escrow kilikuwa ni Dola za Marekani 122,000,000.00 na siyo Dola za Marekani 250,000,000.00 kama ilivyodaiwa na mdaiwa,” ilisomeka sehemu ya hati ya madai.

Kwa mujibu wa wadai, Tanesco kamwe haikuwa sehemu ya makubaliano ya Escrow kama ilivyodaiwa na wadaiwa.

“Fedha ziliwekwa katika makubaliano ya Escrow na siyo kama fedha za umma. Lakini ni kwa kutokana na mgogoro wa malipo yaliyotakiwa kufanywa na Tanesco kwa IPTL,” sehemu ya hati ya madai ilisomeka.

Iliongeza: “Madai kuwa fedha hizo ziliwekwa kama fedha za umma ni ya uongo na kuupotosha umma na kuwachafua wadai kuwa ni wabadhilifu wa fedha za umma.”

Hatua hiyo imechukuliwa na IPTL na wenzake, wiki chache baada ya kumfungulia mashtaka ya kashfa Kafulila kwa madai ya kuituhumu kujipatia Sh. bilioni 200 kutoka katika Akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT) kwa njia zisizo halali.

Kesi hiyo imefunguliwa na IPTL, ambayo ni mdai wa kwanza kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited na Seth. Baadaye, IPTL na wenzake waliwasilisha maombi mahakamani wakiomba itoe amri ya kumfunga mdomo Kafulila.

Baadaye, Kafulila aliwasilisha mahakamani pingamizi la awali dhidi ya kesi hiyo.

CHANZO: NIPASHE
 
Yaani fidia wanayodai ni kubwa Mara mbili ya ile waliyokwapua! Billion 500! mh nchi raha sana hii!
 
Baada ya kusikiliza clip hii, dhana ya Uzalendo wa Zitto nimeishtukia vikubwa.

Maswi anasema "Zitto hawezi kuchangia mijadala ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa kuwa anajua kuna siri zake....."
 
Last edited by a moderator:
Kwani kama pesa ilifunguliwa a/c ili zisubiri uamuzi wa kesi zitakuwa ni zanani?kama sio mali ya umma?
 
ngoja tuone mwisho wa muvi hii maana ndio kwanza inaanza....
 
Tatizo ni Mahakama zetu kugeuzwa kuwa pango la Mafisadi.

Unakuta kesi ya Muhimu kama hii inakaa mwaka mzima bila kutolea hukumu na kwasababu hawa mafisadi wanalijua hilo na wanawatumia Majaji kutumia nafasi hiyo kuzima au kupooza Kesi kwa kuzipiga tarehe,na kwa sababu Pesa wamechukua na hakuna kinachowauma na wanaitumia kuwaumiza wanaopiga Kelele.

Mfano nzuri Prof. Tibaijuka amepewa Mchango wa 1.65 bilioni za Kitanzania unaweza kuona hii sarakasi ya kuwashitaki wawakilishi wa wananchi na magazeti husika ina malengo.

Hiyo haitoshi kama Serikali ni Sehemu ya huu uchafu ni wazi kuwa Kesi hii itapigwa danadana.

Raia yangu kwa Mahakama kutambua umuhimu wa Kesi hizi kwa masilahi ya Umma,hivyo Kesi hizi ziendeshwe haraka iwezekanavyo (Ndani ya Miezi Mitatu hukumu iweimekwisha tolewa.)
 
Baada ya kusikiliza clip hii, dhana ya Uzalendo wa Zitto nimeishtukia vikubwa.

Maswi anasema "Zitto hawezi kuchangia mijadala ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa kuwa anajua kuna siri zake....."

Wapumbavu kama wewe ndio mlipaswa kuuawa kwa kukosa uzalendo.

yaani Watu wanaibia nchi halafu wewe umekalia itikadi za kujadili majina ya watu?

Who is Maswi kama si mshirika wa singasinga katika kupiga pesa?

kwanini watanzania tunakuwa na akili nyembamba kiasi hiki?

Note kuwa Zitto hatafuti umaarufu maana ni maarufu tangu 2007 kwenye scandal ya Buzwagi,sasa Zitto ni msukuma agenda zenye maslahi kwa taifa.

Katika hili la IPTL naamini wapo viongozi wa serikali watafungwa kama alivyofungwa aliekuwa mkurugenzi wa TBS,wakati wanamtuhumu huyo jamaa kuna matahira kama wewe walisimama kumtetea lakini mwishowe ananyea ndoo.

Let wait time will tell
 
Kwanza hakuna haja ya kutoka povu.

Hayo maneno mekundu usingeyatumia hoja yako ingepungukiwa nini?

Lakini nikuhakikishie kuwa Zitto si msafi kama unavyodhani.

Zitto hasukumwi na maslahi ya Taifa bali kutafuta sifa na kutafuta vyeo hata kama ni kwa kuwagawa wananchi na kupandikiza chuki

"Usimwamini mwanasiasa yeyote, hata wa upinzani (hata Zitto)..." - Zitto Kabwe.

Huo ni ujumbe wake Zitto mwenyewe, na alijua kuwa kuna watu kama wewe ambao mnaamini mwanasiasa (Zitto) blindly...

Tujadiliane kwa hoja si kwa matusi (mekundu).
 
kwani unachotaka iweje?
 
Hili ndio tatizo kubwa sana la watanzania yaani hawabebeki kabisa na uelewa wao ni mdogo kiasi kwamba hawajui wamesimama wapi. Yaani IPTL imetuibia mabillioni na kutuingiza katika hasara, katokea mtu kutupa habari hizi kiasi kwamba hata PCCB wameendelea na uchunguzi usokwisha, leo wewe unadiriki kumsema mtu alosimama dhidi ya shirika hili kwa sababu yeye sii msafi? Kwanza hii hoja haikuwa ya chama pia ama kwa sababu Zitto ndiye msemaji na kashtakiwa yeye basi tumwachie afe nalo na hiyo kamati yake ya Bunge. Ndio ahaya niyasemayo siku zote, mnamshangilia mtu akifikwa na matatizo mtamkimbia nyote.

Hata huyo Maswi unamwamini kiasi gani? unajuaje kama yeye sii katika wale walolipwa fedha kutetea ufisadi kwa kutumia wadhifa walokuwa nao. Umepima kwa kiais gani hii hotuba ya mtu anayesimama mbele ya jukwaa kumsema mtu badala ya kupeleka ushahidi alokuwa nao mahakamani maana ndio njia rahisi kwa mwenye kumshuku mwingine. Jamani hili linchi hili ni gonjwa la Ukimwi.
 
Back
Top Bottom