IPTL/PAP: Hatuna kesi na TANESCO

IPTL/PAP: Hatuna kesi na TANESCO

Kuna watu hawajielewi kabisa nawaambia,kubishana nao ni kupoteza nguvu yako bure

VIP ndio waliomba kufunguliwa kwa ESCROW, hivyo kusema kwamba TANESCO na IPTL kuna kesi ni upotoshaji unaopaswa
kukemewa kwa hali juu kabisa.upotoshaji huu si mzuri kwa jamii maana unaweza kuleta chuki na mwishowe kukawa na machafuko ya hapa na pale.
 
KAMPUNI ya kufua umeme IPTL/PAP sasa imezidi kufahamika kuwa haina kesi au mgogoro wowote mahakamani baina yake na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), imefahamika.

Hali hiyo imekuja wakati kukiwepo na habari katika mitandao na baadhi ya vyombo vya habari(isipokuwa gazeti hili) kuwa IPTL/PAP haikustahili kulipwa malipo ya ESCROW kwa kuwa kuna kesi mahakamani.
Taarifa zaidi zinaeleza kesi hiyo inadaiwa imefunguliwa na TANESCO kuhusiana na ukubwa wa gharama za uendeshaji ‘Capacity charge’ unaofanywa na Kampuni ya IPTL.

Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusiana na suala hilo, zinasema kwamba kesi hiyo ilishatolewa hukumu yake tangu 2001, ambapo Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara ICSID iliagiza IPTL ishushe gharama zake kutoka dola milioni 4.2 hadi dola milioni 2.6 kwa mwezi.

Taarifa zilisema baada ya kumalizika kwa kesi hiyo, ndipo kukazuka mgogoro mwingine wa kimaslahi baina ya waliokuwa wabia wa IPTL, ambao ni Kampuni ya VIP na Mechmar ya nchini Malaysia uliopelekea VIP kuomba kampuni ifilisiwe na isilipwe hata thumni na TANESCO.

Kutokana na maombi hayo ya kampuni ya VIP, Mahakama Kuu iliamriwa kufunguliwa kwa akaunti maalumu itakayokuwa inatunza fedha zinazolipwa na TANESCO kwa ajili ya huduma ya umeme inayotumia.

Katibu na Mwanasheria wa Kampuni ya IPTL, PAP, Joseph Makandege alisema hawana kesi na TANESCO na anashangazwa na taarifa zinazotolewa.

“Si kweli kwamba ESCROW akaunti ilifunguliwa kutokana na maombi ya TANESCO kuhusiana na mgogoro wa capacity charge, Kesi ya TANESCO iliisha 2001, na akaunti ya ESCROW ilifunguliwa kwa hukumu ya 2006,’’alisema.

Aliongeza; “VIP ndio waliomba kufunguliwa kwa ESCROW, hivyo kusema kwamba TANESCO na IPTL kuna kesi ni upotoshaji unaopaswa kukemewa,’’.

Makandege, alisema kesi iliokuwepo kwa sasa ni ya mgogoro wa umiliki kati PAP/IPTL na benki ya Standard Chartered ya Hongkong inayodai kununua deni la Kampuni ya Mechmar ya Malaysia.

“Kesi kati ya Standard Chartered na IPTL/PAP haihusiani na TANESCO na wawaache TANESCO watimize wajibu wao na sisi tuyatimiza wajibu wetu kwa Watanzania na tutapambana mahakamani,’’alisema Makandege kwa kujiamini.

Hivyo, alisema wanaolalamika kwamba PAP/IPTL imelipwa kwa makosa wao ndio wanafanya makosa ya kupotosha ukweli wa suala hilo au labda waeleze kwamba Standard Chartered ni Shirika la Umma.

CHANZO: Majira
VIP ndio waliomba kufunguliwa kwa ESCROW, hivyo kusema kwamba TANESCO na IPTL kuna kesi ni upotoshaji unaopaswa
kukemewa kwa nguvu zote.
 
Tumia akili kufikiri na si tumbo!

Subiri Kikao cha Bunge utapata majibu kupitia taarifa ya CAG badala ya kubwabwaja na hawa waandishi makangaja wa baadhi ya magazeti ambao kwa mtumbo kwanza kuliko kazi husika ya kutoa taarifa iliyochambuliwa/utafiti.

kikao gani mkuu?mbona mambo yote yapo wazi kuwa kafulila anatumika juu ya hili suala la IPTL/PAP?
 
Tena huku uvinza kulikuwa na machimbo ya chumvi na kiwanda chake lakini vimekufa na huyu huyu Kafulila ndio kick alioingilia kwenye ubunge! lakini mpaka sasa hakuna chochote alichokifanya, na watu wameendelea kuteseka bila hata kulipwa mafao yao. sisi watu kigoma kusini tunashangaa huyu jamaa anapata wapi muda wa kufanya kazi ya uadalali kwa mafisadi dhidi ya Iptl, huku wananchi wake tukiwa na maisha nagumu na mbunge wetu hatumuoni kabisa jimboni..

Kafulila ni mpigaji nimesema hili mara nyingi tu
 
i)which was meant to support the country’s 2014/15 general budget, has been suspended pending the release of the IPTL probe reports.

(ii)The donors, said the Finland ambassador, would for the time being wait for the final CAG report before making any categorical commitment to support the national budget.

(iii) “Development partners are now awaiting the CAG report and information about its key findings, as well as a response from government, which will determine our decisions on further disbursements,” said the envoy.

USIPOTOSHE UMMA , DONORS WANASUBIRI RIPOTI YA CAG, THIS DOES NOT MEAN WAMECONCLUDE KUWA KUNA UFISADI. DONORS WANASUBIRI FINDS ZA CAG NA KAMA KUNA UFISADI KWELI NI HATUA GANI ZITACHUKULIWA. HIKI NDIO KAFULILA ALICHOFAULU KUKIFANYA, UJINGA WAKE YEYE WA MASLAHI YAKE UNALIUMIZA TAIFA. KAFULILA TUTAMUHUKUMU WATANZANIA KWA KUTUCHELEWESHEA WATANZANIA UTEKELEZAJI WA BAJETI YETU. UPUUZI WA KAFULILA UNAWAGHARIMU MPAKA SHANGAZI ZAKE KAKONKO KULE.

Huu utabaki kuwa ukweli
 
KAMPUNI ya kufua umeme IPTL/PAP sasa imezidi kufahamika kuwa haina kesi au mgogoro wowote mahakamani baina yake na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), imefahamika.

Hali hiyo imekuja wakati kukiwepo na habari katika mitandao na baadhi ya vyombo vya habari(isipokuwa gazeti hili) kuwa IPTL/PAP haikustahili kulipwa malipo ya ESCROW kwa kuwa kuna kesi mahakamani.
Taarifa zaidi zinaeleza kesi hiyo inadaiwa imefunguliwa na TANESCO kuhusiana na ukubwa wa gharama za uendeshaji ‘Capacity charge' unaofanywa na Kampuni ya IPTL.

Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusiana na suala hilo, zinasema kwamba kesi hiyo ilishatolewa hukumu yake tangu 2001, ambapo Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara ICSID iliagiza IPTL ishushe gharama zake kutoka dola milioni 4.2 hadi dola milioni 2.6 kwa mwezi.

Taarifa zilisema baada ya kumalizika kwa kesi hiyo, ndipo kukazuka mgogoro mwingine wa kimaslahi baina ya waliokuwa wabia wa IPTL, ambao ni Kampuni ya VIP na Mechmar ya nchini Malaysia uliopelekea VIP kuomba kampuni ifilisiwe na isilipwe hata thumni na TANESCO.

Kutokana na maombi hayo ya kampuni ya VIP, Mahakama Kuu iliamriwa kufunguliwa kwa akaunti maalumu itakayokuwa inatunza fedha zinazolipwa na TANESCO kwa ajili ya huduma ya umeme inayotumia.

Katibu na Mwanasheria wa Kampuni ya IPTL, PAP, Joseph Makandege alisema hawana kesi na TANESCO na anashangazwa na taarifa zinazotolewa.

"Si kweli kwamba ESCROW akaunti ilifunguliwa kutokana na maombi ya TANESCO kuhusiana na mgogoro wa capacity charge, Kesi ya TANESCO iliisha 2001, na akaunti ya ESCROW ilifunguliwa kwa hukumu ya 2006,''alisema.

Aliongeza; "VIP ndio waliomba kufunguliwa kwa ESCROW, hivyo kusema kwamba TANESCO na IPTL kuna kesi ni upotoshaji unaopaswa kukemewa,''.

Makandege, alisema kesi iliokuwepo kwa sasa ni ya mgogoro wa umiliki kati PAP/IPTL na benki ya Standard Chartered ya Hongkong inayodai kununua deni la Kampuni ya Mechmar ya Malaysia.

"Kesi kati ya Standard Chartered na IPTL/PAP haihusiani na TANESCO na wawaache TANESCO watimize wajibu wao na sisi tuyatimiza wajibu wetu kwa Watanzania na tutapambana mahakamani,''alisema Makandege kwa kujiamini.

Hivyo, alisema wanaolalamika kwamba PAP/IPTL imelipwa kwa makosa wao ndio wanafanya makosa ya kupotosha ukweli wa suala hilo au labda waeleze kwamba Standard Chartered ni Shirika la Umma.

CHANZO: Majira

Ukweli milele, mtapiga kelele, mpaka mtachoka.
 
Back
Top Bottom