BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Chanzo: Tanzania DaimaIPTL haponi mtu
- Makundi ya urais yatia mguu, watuhumiwa hofu tupu
- Profesa Muhongo ajipanga kulipua bomu la mwaka
![]()
KASHFA kuchota fedha kwenye Akaunti Maalum ya Escrow zaidi ya sh bilioni 200, zilizohifadhiwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), itang'oa idadi kubwa ya watendaji wakuu Serikalini na wanasiasa, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wiki moja iliyopita tangu kuanza kwa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge mjini hapa, umebaini kuwa joto la kashfa hiyo linazidi kupanda huku baadhi ya wabunge bila kujali vyama vyao, wakiungana kuhakikisha wahusika wanawajibishwa, ikiwemo kung'olewa madaraka yao.
Mjadala wa wabunge wengi, ndani ya viunga vya Bunge na nje ya eneo hilo ni kuhusu kashfa hiyo iliyotokana na mradi wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Independent Power Tanzania LTD (IPTL).
Watuhumiwa katika kashfa hiyo ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu Eliachiam Maswi ambao imeelezwa kuwa wanafanya kila aina ya ushawishi kuhakikisha wanaepuka kikombe hicho.
Wengine ni Gavana wa Benki Kuu (BoT), Benno Ndullu, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Felches Mramba.
Pinda anahusishwa kwenye kashfa hiyo kwa madai alishindwa kuchukua hatua za haraka kuzuia uchotwaji fedha hizo.
Baadhi ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wameungana na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na kambi nzima ya wabunge wa upinzani, kuishikia bango kashfa hiyo.
Mmoja wa wabunge maarufu wa CCM ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema hoja hiyo ni ya wabunge wote, wakiwemo wa CCM ambao wakati mwingine huwapa hoja mpya wenzao wa upinzani kuhusu kashfa hiyo.
Zaidi ya yote, hoja hiyo imekolezwa na baadhi ya makundi ya wataka urais ambao duru za siasa zinaelezea kuwa wanataka hoja hiyo ifike mwisho na hakuna namna inaweza kumwacha Waziri Mkuu Mizengo Pinda salama.
Pinda ambaye ameshaweka bayana kwamba ameanza mbio za kuwania urais kimya kimya katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani anaonekana ndiye mlengwa.
Pinda tayari ameshaonekana tishio kwa baadhi ya makundi ya urais hasa yale ya vijana ambao wanadhani kuchafuka kwake na kashfa hiyo, kutapunguza kasi yake ya kutaka kuwania urais.
Hata hivyo wabunge wanaotajwa kuwa kwenye kambi ya Pinda wamejipanga na kuweka mkakati wa kumnusuru kiongozi huyo.
Kambi ya Pinda inahofia kashfa hiyo inaweza kukifanya CCM kuzalisha makundi hasimu na hivyo kukosa mwelekeo kwenye uchaguzi mkuu kama ilivyotokea mwaka 2010 baada ya kashfa Richmond iliyomng'oa mtangulizi wake Edward Lowassa mwaka 2008.
Hofu hiyo ndiyo inayodaiwa kukikumba CCM kilichokuwa kikitaka mjadala huo usipelekwe bungeni lakini jitihada hizo zimegonga mwamba baada ya Bunge kutangaza kujadili wiki hii.
Shinikizo la kambi nzima ya upinzani, wabunge wa CCM na makundi ya urais, ndiyo yaliyofanikisha kuzima mkakati wa Serikali uliotaka kuizima hoja hiyo isije kwenye mkutano wa Bunge hili kwa madai kuwa ripoti ya uchunguzi wake kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), haijakamilika.
Tayari Kamati ya Uongozi baada ya mjadala mzito, imelijulisha Bunge kuwa hoja hiyo sasa itapelekwa bungeni Novemba 27 na 28.
Naibu Waziri kutolewa kafara?
Wakati ripoti ya CAG ikisubiriwa kwa hamu Bungeni, baadhi ya wabunge wamedokeza kuwa ripoti hiyo iko hadharani na imewataja baadhi ya vigogo wa wizara ya nishati na madini kuhusika.
Kutokana na hali hiyo, duru hizo za siasa zinadai kuwa Naibu Waziri mmoja wa wizara hiyo ameandaliwa kisaikolojia kutolewa kafara ili kuwalinda vigogo hao wasiaibike.
Wizara hiyo ina Manaibu Waziri wawili ambo ni Steven Masele (Madini), Charles Kitwanga (Mawe matatu ambaye anashughulika na Nishati.
Taarifa za kuwapo mpango wa kutoa kafara Waziri huyo mdogo, wili iliyopita ziliibuliwa Bungeni na Mbunge wa Nyamagana, Ezekie Wenje.
Bila kutaja jina, Wenje alidai kuwa mpango huo upo na tayari Waziri huyo aliitwa jijini Dar es Salaam ghafla kwenda kujengwa kisaikolojia.
Muhongo ajipanga kulipua bomu
Wiki iliyopita (JUMATANO) baada ya kiindi cha maswali na majibu kumalizika, Waziri Muhongo alikuwa akizungumza na baadhi ya wabunge kwenye eneo la viwanja vya Bunge, kwamba anataka kuomba nafasi ya kuzungumza bungeni kabla ya ripoti hiyo kuwasilishwa.
Alisema katika mazungumzo hayo, amepanga kufichua siri kubwa iliyojificha nyuma ya sakata hilo na kutaja majina ya wabunge na watendaji wengine aliodai wamepata mlungula kusukuma ajenda hiyo bungeni.
Mgogoro uliosababisha fedha kuwekwa katika akaunti hiyo ya Tegeta ya BoT ulitokana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kugoma kulipa gharama za uwekaji mitambo (Capacity Charge) kwa IPTL mwaka 2006 kwa vile ilibainika IPTL ilikuwa ikitoza gharama kubwa kuliko iliyopaswa.
Akaunti hiyo ya Tegeta ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi fedha zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya pande hizo mbili umalizike.
Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, iliagiza BoT kulipa fedha hizo kwa kampuni ya PAP mara baada ya kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kwamba mgogoro baina ya wamiliki wa IPTL na Tanesco umemalizika na hivyo Benki Kuu haina sababu ya kuhifadhi fedha hizo.
Uamuzi huo wa kulipwa ulizua upinzani mkali bungeni ambapo wabunge wawili wa kambi ya upinzani; Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe.
Wabunge hao walidai kuwa zoezi hilo limejaa ufisadi na Bunge liliazimia kwamba suala la kutolewa fedha katika akaunti ya Tegeta lifanyiwe uchunguzi wa kina na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).