Ipo wapi The Mwalimu Nyerere Foundation? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipo wapi The Mwalimu Nyerere Foundation?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kivumah, Oct 11, 2011.

 1. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ...Wanajamvi hivi hii Taasisi ya Mwalimu bado ipo??, na inafanya nini?
  Kuna kipindi kulikuwa na Mpango(Project) wa kujenga Investment House kwa ajili ya hii Taasisi sijui ulifikia wapi?
  Tujadili.
   
 2. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  unadhani baada ya Mchonga kumsababishia aibu mkuu wa kaya wa sasa kipindi kile monduli, m.k.w.e.r.e hawezi kihangaika nae, labda kama unataa ile R1 Foundation, hivi wewe ushamsikia jaah kaaya akisema 'bana wa taifa?' well kukujibu tu swali lako, foundation hiyo ipo kigamboni, choka mbaya.
   
 3. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  duh, typing ya leo, utadhani nimevuta bangi, duh lusinde lusinde leo looh!!!
   
 4. peri

  peri JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Subiri masiku machache watakapo fanya kumbukumbu ya kifo cha mwalim utaisikia.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Haina hela kabisaa.........
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ipo kama haipo
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Bora ingefutwa tu maana naona kama inashusha hadhi ya Hayati baba wa taifa,..
   
 8. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Interest za Viongozi wa wasasa siyo kum popularize Baba wa Taifa bali ku popularize maisha yao. Katika hali kama hii unadhani kuna innovation yoyote katika kuiendeleza The MN Foundation????
   
 9. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ​Mhh mi navyofahamu hiyo Foundation bado ipo tena iko strong. Ilikuwa wajenge kitega uchumi chao cha Ghorofa zaidi ya 15 pale karibu na Benki kuu, lakini kutokana na sababu za kiintelejensia walikataliwa na ba badala yake wakapatiwa kiwanja kile kalichokuwa kikitumiwa na Parking System wale jamaa wanaokusanya pesa town unapopaki gari lako. Hapo sasa ndio wanatarajia kuanza ujenzi huo.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  utawala umeimaliza
   
 11. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Usicheze na DR. JK (aka dr wa uchakachuaji)
   
 12. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Chanzo cha mapato cha hii Taasisi ni nini. Kuna kipindi Mzee Sabodo aliendesha bahati nasibu ambayo mapato yake yangetumika kuindesha hii Taasisi
   
 13. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Kwakweli inasikitisha, kwa Wenzetu Ulaya na Marekani Taasisi kama hizi za Viongozi wastaafu/waliofariki ambao walikuwa ni Visionery Leaders kama Mwalimu, ndio Taasisi kubwa na zinaendeshwa na watu makini wanaoendeleza zile falsafa za mwenye jina la Taasisi kwa Vitendo. Hili kwanini limeshindikana hapa kwetu. Badala yake zinazoshobokewa ni Taasisi za Wake wa Marais, WAMA, EOTF. bado nyingine itakuja baada ya Uchaguzi 2015
   
 14. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..cha kushangaza Viongozi waliowekwa kuiongoza hii Taasisi ndio wale wanasema walikuwa Wanafunzi wa Mwalimu, Mzee Butiku Joseph, Salim A. Salim?. Where have all leaders gone?
   
 15. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ...Well kama una uhakika ipo na ipo strong, vizuri. Lakini kwanini wanafanya mambo yao chini ya Carpet, kimya kimya. Tunataka kusikia nini wanafanya kuendeleza falsafa za Mwalimu kwa Vitendo, Tunataka kuisikia inatoa Scholarships za masomo kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliopikwa kuzienzi falsafa za Mwalimu ili wawe Viongozi wa Nchi hii baadae, tunataka kuisikia inakemea vitendo vya Rushwa na Ufisadi vilivyokithiri ktk Nchi hii sa hivi ambavyo Mwalimu alivikemea kwa nguvu zake zoote
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi mtendaji amekula pesa zoooote kazimaliza. Alipewa pesa na Sabodo ili achezeshe bahati nasibu zawadi hazikuwahi kutolewa!! Alipewa pesa na Museveni hazikujulikana zilipoenda!! Muulizeni si yupo?
   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  sasa hivi ndio kuna makontena ofisi ya NPS..
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Walifanya kosa na wao kuutaka utawala wa nchi badala ya kuwa kando na kusimamia sera za mwalimu kwa kukemea Rushwa na Ufisadi. Sasa baada ya kuingia kwenye kinyang'anyiro walijikosesha fursa ya ukemeaji kwa kuwa walinyanyaswa na mtandao. Sasa wakaanza kuonyesha hasira zao na hadi hivi sasa wana hasira wanakosa objectivity!
   
 19. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Sidhani kama MN Foundation ipo imara kama ilivyosemwa. Sometime back we used to hear or watch a number of activities done by the Mwalimu Nyerere Foundation but nowadays Mh Mh hata Joseph hasikiki.
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Kuna post mzee butiku amenena!
   
Loading...