Ipo siku China na Urusi watazichapa sana

Ipo siku China na Urusi watazichapa sana

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,890
Reaction score
18,836
Urusi ilijitanua pole pole kuelekea mashariki kufuata biashara ya manyoya ya wanyama. Ikafika hadi bahari ya pacific, ikavuka hadi kufika Alaska. Katika kujitanua huko ikafika bonde la mto Amur ulio kaskazini mashariki ya China. Majeshi ya China wakati huo wa Qing dynasty yaliwapiga vibaya wavamizi hao wa Kirusi. Wakaandikishiana mkataba na Urusi ikatambua kuwa bonde la mto Amur ni mali ya China.

Baadaye Urusi akapata nguvu huku China ikidhoofishwa na Uingereza na Ufaransa. Basi Urusi akatumia fursa hiyo kurudi tena bonde la mto Amur na kumlazimisha China kusaini mkataba mpya. Bonde la Amur likaenda Urusi.

Eneo hilo wachina wanaliita Outer Manchuria. Kadri tunavyoona China akiimarika kijeshi na kiuchumi, huku Urusi akizidi kudhoofika, tutegemee China kuidai Outer Manchuria. Au hata kudai na sehemu ya Siberia pia, maana walikuwa wanadai kuwa mpaka halisi ni mto Lena.

Mwenye nguvu mpishe.
images.jpeg
 
Urusi ilijitanua pole pole kuelekea mashariki kufuata biashara ya manyoya ya wanyama. Ikafika hadi bahari ya pacific, ikavuka hadi kufika Alaska. Katika kujitanua huko ikafika bonde la mto Amur ulio kaskazini mashariki ya China. Majeshi ya Chini wakati huo wa Qing dynasty yaliwapiga vibaya wavamizi hao wa Kirusi. Wakaandikishiana mkataba na Urusi ikatambua kuwa bonde la mto Amur ni mali ya China.

Baadaye Urusi akapata nguvu huku China ikidhoofishwa na Uingereza na Ufaransa. Basi Urusi akatumia fursa hiyo kurudi tena bonde la mto Amur na kumlazimisha China kusaini mkataba mpya.

Eneo hilo wachina wanaliita Outer Manchuria. Kadri tunavyoona China akiimarika kijeshi na kiuchumi, huku Urusi akizidi kudhoofika tutegemee China kuidai Outer Manchuria. Au hata kudai na sehemu ya Siberia pia maana walikuwa wanadai kuwa mpaka halisi ni mto Lena.

Mwenye nguvu mpishe.
View attachment 3464062
Usoviet na Uchina walichapana mbona miaka ya 60s mpaka Soviet akatishia kutumia Nyuklia haaaaah
 
Tunako ENDA hata sisis huku atuko SALAMA sana, cha KUSHANGAZA badara viongozi wajipange vita nje wanakimnizana na lisu mtu Hana hata bastola utamfanya nini mtu mwenye ballistic akiitaka Tena kagera, na mto nyasa mkuu?

Fullstop, kwishaaa
 
Soviet ndie aliye changia mpaka Outer Mongolia[ hii Mongolia ya sasa ] kujitangazia uhuru wake toka China na kubaki inner Mongolia wakati huo China inapigana na Japan na Vita vya wenyewe kwa wenyewe
 
Soviet ndie aliye changia mpaka Outer Mongolia[ hii Mongolia ya sasa ] kujitangazia uhuru wake toka China na kubaki inner Mongolia wakati huo China inapigana na Japan na Vita vya wenyewe kwa wenyewe
Kesho, keshokutwa China ataidai Mongolia. Dunia hii mnaform alliance, mnasolve shida iliyopo. Kesho mnazichapa
 
Kesho, keshokutwa China ataidai Mongolia. Dunia hii mnaform alliance, mnasolve shida iliyopo. Kesho mnazichapa
Advantage aliyonayo Mongolia ni moja taifa lolote kati ya Urusi ama China likitaka kumvamia na kupora eneo lake Mongolia ana nafasi ya kuomba msaada kwa yoyote kati ya China ama Russia.

Hivyo China akitaka kumvamia Mongolia basi Mongolia ataomba support ya Russia vivo hivyo Russia akitaka kumvamia Mongolia huo ndio usalama Mongolia alionao maana kapakana na nchi mbili tu China na Russia.

Ili China aweze kumvamia Mongolia basi inabidi Russia awe dhaifu ili aweze kummudu pia Russia akitaka kumvamia Mongolia inabidi China awe dhaifu wa yeye kuweza kummudu kinyume na hapo mfupa wa Mongolia unakuwa mzito kwa wote wawili China na Russia labda kama washirikiane kuimega wote wawili
 
Tumsikilize Mmongolia The Mongolian Savage anasemaje kuhusiana na hili kwanza
 
Back
Top Bottom