Kwa muda wa miaka mitatu sasa tangu tukio la kuuawa watu watatu kule Arusha imekuwa kawaida kusikia matukio ya mauaji huku watuhumiwa wakiwa ETI ni chadema. Nakumbuka wakati huo tbc1 waliandaa kipindi maalum wakituonyesha watanzania jinsi chadema walivyofanya uhalifu huo. MUNGU AEPUSHE MBALI!
Yakaja matukio ya Zanzibar, padre akapigwa risasi, sheikh akamwagiwa tindikali, makanisa yakachomwa moto kabla ya padri Mushi kuuawa kwa kupigwa risasi. Kisha mambo yakarudi bara na ikawa mchuano kati ya wakristo na waislam. halafu yakaingia kwenye siasa za ccm na chadema. Watu wakafa kwa kupigwa vitu vizito kichwani huku wengine wakipigwa mabomu yaliyosemekana kurushwa na wafuasi wa chadema na kufumua utumbo wa wahanga.
Mungu atusaidie! Matukio yote hayo yanabaki bila mtu hata mmoja aliyekamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ukiacha DHAMBI mbaya ya kutaka kuwaaminisha watanzania kuwa matukio yote hayo yanafanya Rwakatare na CHADEMA. Hivi tutaangalia matukio mabaya yakitukia bila wahusika hadi lini? Dr ulimboka, mwangosi, katibu wa bakwata; nani mhusika?
Haya yakiachwa yaendelee kutokea huku wahusika wakifumbiwa macho kwa lengo la kupata ummarufu na kuwachafua wengine kisiasa tusishangae kusikia siku moja wale wanaodhani wanapanda mbegu njema kwao wakajikuta wanakumbana na mavuno ya kile walichokipanda.