Ipi saini feki na orijino ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu??

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
10,912
13,230
Hii nimeikuta sehemu, Kuna nyaraka mbili kutoka makao mkuu (white house) ukiangalia saini zote ni za mtu mmoja lakini zinatofautiana, Sasa hapa nashindwa kuelewa ukweli uko wapi
da8a306539030b710ea16f44dadcec80.jpg

e3b25d14c12f7d25fe9eb52a83560f21.jpg
 
Saini Inatakiwa Mleta Mada Ujue Siyo Kama Muhuri!
Saini Inavyowekwa Inategemea Aina Ya Kalam Ulivyoishika Ila Hiyo Ni Ya Mtu Mmoja

Nakumbuka Siku Moja Nmb Bank Ilibaki Kidogo Nifunge Account Maana Nimeweka Saini Naambiwa Siyo Yangu
 
Hii nimeikuta sehemu, Kuna nyaraka mbili kutoka makao mkuu (white house) ukiangalia saini zote ni za mtu mmoja lakini zinatofautiana, Sasa hapa nashindwa kuelewa ukweli uko wapi
da8a306539030b710ea16f44dadcec80.jpg

e3b25d14c12f7d25fe9eb52a83560f21.jpg
Saini ya pili inaonekana kuna hitilafu kidogo. Nahisi kwa kuwa mantiki ya barua ilikuwa na ujumbe wenye ukakasi na ndi maana saini imekaa kiukakasi.
 
..inashauriwa tuwe na sahihi zaidi ya moja kutegemea na mazingira. Msigwa inawezekana hizo zote ni sahihi zake, ila anajaribu kutumia sahihi tofauti tofauti kuzuia watu wasimuige.
 
Hii hatari! Kuna haja ya kuchukua hatua! Ndani ya siku kumi sahihi tofauti kwa Ofisa wa Ikulu tena kitengo muhimu sana ya habari! Kutatumika utapeli kupitia huo mkanganyiko wa sahihi.
 
..inashauriwa tuwe na sahihi zaidi ya moja kutegemea na mazingira. Msigwa inawezekana hizo zote ni sahihi zake, ila anajaribu kutumia sahihi tofauti tofauti kuzuia watu wasimuige.

Nenda bank na sahihi zako mbili ndo utawajua vzr
 
Nenda bank na sahihi zako mbili ndo utawajua vzr
Unaweza kuwa na sahihi tofauti kulingana na bank. Yaani ukienda CRDB sahihi nyingine, ukienda NMB sahihi nyingine. Hizi mara nyingi wanatumia wahasibu (chief accountant) au mtu yeyote anayehusika na kuidhinisha malipo. Kuna mtu iliwahi tokea, walifoji sahihi yake wakijua anatumia hiyo hiyo ktk kila bank, na hao wezi walipofika hiyo bank kumbe jamaa anatumia sahihi tofauti, walikwama kwani alipigiwa simu muhusika.
 
Huenda kuna moja iko scanned inawekwa tu electronically ili hata kama hayupo, tamko linatoka tu. Ukizingatia yeye mwenyewe ana kaimu, sasa asipokuwepo aka saini mwingine ataandika kaimu wa kaimu?
 
Back
Top Bottom