Uchaguzi 2020 Ipi nafasi ya wanawake kwenye utawala wa Rais Magufuli?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,532
Habari za wakati huu;

Tunapoelekea kufanya uamuzi iwapo John Magufuli anafaa kupewa miaka mitano hebu tuitazame historia yake katika masuala ya Jinsi na Jinsia hasa mtazamo na misimamo yake kwa wanawake.

Swali la kujiuliza ni ipi nafasi ya wanawake katika UTAWALA wa Rais Magufuli? Je, hali na nafasi za wanawake zimekuwa BORA kwa kiasi gani katika KIPINDI cha MIAKA 5 hasi katika haki zao, fursa, usawa na uwezeshaji wa kiuchumi?

Je, wanawake wakifanya maamuzi kwa kuzingatia utendaji wake kwa miaka 5 anastahili kupewa Tano?

Mimi binafsi nafikiri hatapewa kura na wanawake hasa ukizingatia kauli zake kadhaa dhidi ya wanawake na namna anavyowachukulia. Tumjadili hapa tujue kama anastahili kupewa tano tena na wanawake
 
Sema ndio hivyo akili zetu sisi Watanzania tunajijua wenyewe.

Nakumbuka mwalimu Nyerere akiwa na mkutano na Umoja wa Wanawake (UWAT) Alisema "wanawake ni wengi kwa idadi kulinganisha na wanaume wenye viremba wakiamua kumsimamisha Rais wamtakaye ni rais sana wao kushinda".

1.Utawala huu wa Mkono wa chuma umembagua sana mwanamke
2. Umemdharilisha sana mwanamke.
3. Umemkandamiza mwanamke.
Mifano ifuatayo.
Wajaribu kuandamana waone Nitawapiga mashangazi zako waziri mkuu.

Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi imeteua idadi ya wanawake 18 tu kugombea ubunge kati yamajimbo 264.

Wanawake fanyeni uchaguzi sahihi 2020.
Vihurumieni vizazi vyenu na watoto wenu hatma ya maisha yao.
 
Magu amewadhalilisha wanawake mpaka kwenye mavumbi tusikubali udhalilishaji huu wa mama na dada zetu kamwe, tumkatae magu October.
 
Mmmh mwaka huu mtaropoka sana. Mama samia anatuwakilisha vizuri wanawake.
 
Back
Top Bottom