covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,036
- 20,031
Kinachoendelea Mashariki mwa Congo DRC si mgogoro wa mbali kama wengi tunavyodhani. Huu ni mgogoro ambao hakuna nchi ya Afrika Mashariki itakayobaki salama. Kuna chaguo mbili tu: ama uwe sehemu ya mchezo na uchague upande, au ubaki mpweke kisha upokonywe hata kile kidogo ulichonacho.
Tukirudi nyuma kidogo, Tanzania haijawahi kuwa mgeni kwenye siasa na migogoro ya ukanda huu. Kwa muda mrefu jina la nchi yetu limetajwa kuhusishwa na kusaidia kuwapandisha madarakani baadhi ya viongozi wakuu wa eneo hili—kina Kagame, Museveni na wengineo. Hii peke yake inatosha kuthibitisha kuwa Tanzania ni mdau halisi wa kinachoendelea DRC, iwe tunapenda au hatupendi.
Kwa sasa hali inaonekana kama Tanzania imepunguza waziwazi ushiriki wake, au tuseme imechagua siasa ya ukimya. Hatueleweki tunavuta upande gani hasa:
- Upande wa (M23 + Rwanda + Uganda)
- au upande wa (Congo DRC + Burundi)
Kinachoonekana ni kwamba Tanzania inasaidia Congo na Burundi kwa tahadhari kubwa, huku ikimwogopa au kumuangalia Rwanda kwa jicho la kibiashara hasa kwa sababu Rwanda ni mdau mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam.
Kenya wao hawajifungi na upande wowote. Wapo pale kwa maslahi yao binafsi, biashara na ushawishi nothing else.
HATARI ILIYO MBELE YETU
Kama hali itaendelea hivi, kuna uwezekano mkubwa sana Tanzania ikajikuta iko chini ya ushawishi wa Rwanda huko mbeleni. Sio kwa vita ya moja kwa moja, bali kwa nguvu ya uchumi na masharti.
Mkakati wa Kagame uko wazi kwa anayefuatilia:
- Kupitia M23, Rwanda inameza mikoa ya Mashariki mwa Congo mkoa baada ya mkoa
- Ana silaha za kisasa, jeshi lililoandaliwa vizuri, na fedha nyingi
- Generali wa Congo wanahongwa waziwazi
- Maeneo yanayotekwa yanachimbwa rasilimali bila huruma
Mfano: kipindi Goma ilipotekwa, zaidi ya tani 300 za dhahabu ziliporwa hapo goma. Hii inaonyesha pesa zipo, na mpango ni mkubwa.
TARGET HALISI SI GOMA – NI HII:
Katanga – moyo wa migodi Africa mashariki
Lubumbashi – moyo wa biashara mashariki ya congo
Rwanda ikifanikiwa kufika Lubumbashi, hapo ndipo Tanzania itakapopoteza pakubwa sana. Kwa nini? Karibu nusu ya shehena ya Bandari ya Dar es Salaam inaelekea Congo kupitia Lubumbashi. Lubumbashi ikidhibitiwa na Rwanda/M23:
- Watadhibiti njia za biashara
- Wataweka masharti yao
- Tutahitaji pesa → tutalazimika kutii masharti yao
Hapo ndipo utawala wa kiuchumi unaanza, bila hata risasi moja kupigwa Dar es Salaam.
Kagame tayari:
Amejenga bandari kavu kubwa Kigali
Ameanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu
Kigali inajengwa kisasa isivyo kawaida Haya yote si bahati mbaya ni maandalizi ya jambo kubwa linalokuja.
Katika mazingira haya yote, Unafikiri Tanzania ifanye nini sasa?
Karibuni mchangie. Huu mjadala hauhitaji jazba, unahitaji akili, historia na ujasiri wa kusema ukweli.